Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,007
- 9,873
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman amesema serikali ilikuwa tayari imejipanga kuongeza viwango vya mishahara kwa watumishi wa umma, lakini kutokana na janga la corona, utekelezaji wa mpango huo umesitishwa kutokana na nchi kuyumba kiuchumi
Alisema serikali imejipanga kuimarisha maslahi bora ya watumishi wote, ikiwemo kuongeza mishahara kwa kadri wakati unaporuhusu
Katika kujali maslahi ya watumishi wa umaa Waziri Suleiman amesema walimu wote waliokuwa wakifanya kazi kwa njia ya kujitolea kwa zaidi ya miaka kumi, wataajiriwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021
Waziri Suleiman alisema kutokana na uhaba wa walimu vijijini kuna baadhi ya watu waliosomea uwalimu walikuwa wanajitolea katika vijiji mbalimbali nchini kwa kulipwa ujira wa kujikimu na wanakijiji
Suleiman alisema hayo wakati akijibu hoja za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, waliotaka kupata ufafanuzi kwa nini wapo walimu wengi wanajitolea bila ya kuajiriwa hadi sasa
----
PIA WALIMU WALIOJITOLEA WAULA MWAKA WA FEDHA 2020/2021
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman amesema walimu wote waliokuwa wakifanya kazi kwa njia ya kujitolea kwa zaidi ya miaka kumi, sasa wataajiriwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021.
Suleiman alisema hayo wakati akijibu hoja za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, waliotaka kupata ufafanuzi kwa nini wapo walimu wengi wanajitolea bila ya kuajiriwa hadi sasa.
Akifafanua, alikiri kuwepo kwa suala hilo, ambalo limekuja kutokana na tatizo kubwa la uhaba wa walimu katika maeneo mengi ya vijijini. Alisema walimu hao walikuwa wakijitolea kufundisha wanafunzi bila ya kuajiriwa na kulipwa fedha kidogo za kujikimu zinazotolewa na wanavijiji.
“Spika napenda kuthibitisha kwamba walimu wote waliokuwa wakisomesha kwa njia ya kujitolea kwa zaidi ya miaka kumi, sasa serikali itawaajiri katika kipindi hichi cha mwaka wa fedha 2020/2021,” alisema.
Alisema serikali imejipanga kuimarisha maslahi bora ya watumishi wote, ikiwemo kuongeza mishahara kwa kadri wakati unaporuhusu. Kwa mfano, alisema serikali ilikuwa tayari imejipanga kuongeza viwango vya mishahara kwa watumishi wa umma, lakini kutokana na janga la corona, utekelezaji wa mpango huo umesitishwa kutokana na nchi kuyumba kiuchumi.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walipitisha makadirio, mapato na matumizi ya bajeti ya Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora kwa mwaka wa fedha 2020/2021 na kuidhinisha jumla ya Sh 15,617,500,000. Kati ya fedha hizo Sh 14,217,500,000 ni kwa kazi za kawaida na Sh 1,400,000,000 kwa kazi za maendeleo.
HABARI LEO