Serikali ilichapisha fedha bila mpangilio? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ilichapisha fedha bila mpangilio?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuko, Nov 16, 2010.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Nov 16, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Inasemekana kupungua kwa thamani ya Tsh, kunakoakisiwa na kupanda kwa bei ya bidhaa siku za karibuni kumetokana na serikali kuchapisha fedha nyingi bila kujali tija ya taifa katika kipindi hiki cha uchaguzi. Inasemekana kuwa fedha hizo zilichapishwa ili CCM iweze kupata fedha kwa ajili ya kukisaidia kushinda, lakini pia ili serikali iweze kugbharamia matumizi mengine ikiwemo mishahara na posho mbalimbali za watendaji wake. Hali hii imesababisha mwangwi mkubwa wa mfumuko wa bei hasa baada ya uchaguzi kutokana na kupungua thamani ya shilingi pale inahitajika kwa ajili ya kuagiza bidhaa na malighafi kutoka nje.

  Wataalamu wa uchumi wanatabiri ugumu mkubwa wa maisha wakati seriakali ikijitahidi kujitoa katika hali hii, na inasemekana kuwa benki zitaathirika zaidi endapo watanzania na watu wengine waliopo nje ya nchi wataamua kuweka fedha za kigeni benki na kuzibadilisha kuwa shilingi, kwani kwa wakati huu shilingi itakuwa na thamani ndogo, hali ambayo itaathiri benki pale shilingi itakapopanda thamani (Hii ina maana kuwa kwa mfano kama ukiweka uro moja benki kwa sasa itahesabiwa kama labda tsh 2000. Miezi michache ijayo pengine shilingi itapanda bei na kuwa tsh 1800 kwa uro 1, then benki itakuwa na hasara ya tsh 200 kwa kila uro ambayo itakuwa imepokea kwa sasa).
   
Loading...