Serikali ilegeze masharti ya kupata pasipoti ili watu wakatafute fursa nje ya nchi

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Messages
21,310
Points
2,000

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2015
21,310 2,000
Masharti ya kupata passport inatakiwa tu kitambulisho cha uraia zingine zote mbwembwe za kusumbuana tu sijui barua ya mwaliko sijui nini ujinga mtupu. Kwani mtu hawezi kwenda nchi nyingine kutafuta fursa hata kama hana mwenyeji?

Ona huyu kijana Mtanzania mwenye mgahawa China akipiga kazi baada ya kuona fursa China. Uhamiaji acheni ubahili wa kutoa passport.

jd41

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Messages
3,383
Points
2,000

jd41

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2015
3,383 2,000
Kijana kafanya jambo haswaa, hizo ndio akili jamani, tusikae tunawaza ajira tu ambayo hatujui itakuja lini, na itatatoka wapi, matokeo yake kila siku unakuwa mtu wa hasira, stress, inaweza kumfanya mtu akawa chizi.

Iruhusu akili taratibu ianze kuwaza plan B, wakati lile wazo la plan A ukiliweka pending kwa muda, siku ukiambiwa apply sehemu fulani nenda, ukirudi unaendelea na wazo lako la pili wakati unasubiri majibu ya ulipo apply. Hii itasaidia sana kurudisha amani na tumaini jipya kwa mtu, ni kufikiria tu nini cha kufanya kulingana na uwezo wako, hata kama biashara itaonekana ndogo, anza hivyo hivyo huwezi jua Mungu kakupangia nini mbele ya safari, au kama mko wawili watatu mnaweza changia nguvu ya mtaji, ajira ni ngumu watu wengi wanazihitaji, nafasi zilizopo ni chache, huu ni ukweli lazima tuukubali kuliko kuendelea kupoteza muda kusubiri ajira.

Kwa experience yangu Tz, watu wenye elimu kubwa ndio wagumu wa kujiajiri, tofauti na wenye elimu ndogo.Hivyo unakuta wengi wenye elimu ndogo wana maendeleo kuliko wenye elimu kubwa. Mawazo ya kufanya kazi ofisini, kulipwa mshahara mkubwa, kuishi kwenye nyumba nzuri, kuendesha gari zuri, ndio yametutawala sana wenye elimu za vyuoni, hii inafanya mtu kuwa mzito na mgumu kutafuta kazi nyingine tofauti na kusubiri ajira, but jinsi unavyochelewa ku transform your mind kwenye hili, ndivyo unavyozidi kujirudisha nyuma kimaendeleo, badilika, anza sasa hujachelewa, wakati ni huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
August

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2007
Messages
5,285
Points
2,000

August

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2007
5,285 2,000
YEHODAYA,
Masharti na vigezo ni vizuri vikazingatiwa , sasa kwa huyu alikwenda kama Mwanafunzi hatimaye akajiongeza, sasa kama wenyeji wameweza kumpa licence ya biashara basi wanatakiwa kuwa flexible kwa kukubali licence yake ya biashara kama mbadala wa invitation letter, lakini zaidi ya licence wanaweza kuuliza kama hiyo kiimanjaro restaurant imesajiliwa na wamiliki wake ni akinanani yeye pekee yake au ana mbia au wabia n.k
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Messages
21,310
Points
2,000

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2015
21,310 2,000
Masharti na vigezo ni vizuri vikazingatiwa , sasa kwa huyu alikwenda kama Mwanafunzi hatimaye akajiongeza, sasa kama wenyeji wameweza kumpa licence ya biashara basi wanatakiwa kuwa flexible kwa kukubali licence yake ya biashara kama mbadala wa invitation letter, lakini zaidi ya licence wanaweza kuuliza kama hiyo kiimanjaro restaurant imesajiliwa na wamiliki wake ni akinanani yeye pekee yake au ana mbia au wabia n.k
sisi tunafanya kazi kizamani mno vitu wanavyoomba uhamiaji ni vitu vya balozini unapoomba visa!!! naona uhamiaji wamechanganyikiwa wamejigeuza maafisa wa visa wa ofisi za ubalozi za nchi za nje

Nchi zote kenya,uganda,rwanda na burundi kote huko kuomba passport huombwi vitu vya kuomba visa! ni Tanzania tu pekee Africa mashariki ambapo muomba passport anatakiwa kupeleka vitu ambavyo huombwa na balozi za nje zikitaka kukupa VISA ambako mtu hutakiwa kupeleka barua ya mwaliko,leseni ya biashara kama ulivyosema nk ili wakupe VISA uende huko.UHamiaji umegeuka ofisi ya ubalozi wa nchi za nje!!!!!

Uhamiaji wao walitakiwa tu kutoa passport kwa kutumia kitambulisho cha uraia au birth certificate tu hayo mengine wamwachie muhusika akapambane na hali yake ubalozini kwenye nchi anakoenda!!

tunapolalamika kuwa uhamiaji hawako vizuri hatutanii wako nyuma mno na wakati
 
Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Messages
242
Points
500

Umkonto

JF-Expert Member
Joined Dec 27, 2018
242 500
Maoni yangu, serikali isiishie kulegeza masharti tu, bali inatakiwa ifanye passport kuwa chanzo cha mapato, kwa kuwahamasisha Watanzania wawe na passport.

Tatizo Tanzania tunaendekeza kaushamba fulani hivi wakati dunia ipo kasi sana.

Uhamiaji wawahamasishe Watanzania wapate passport wakatafute fursa kokote duniani.

Zipo baadhi ya nchi kwa sasa zimefikia hatua ya kuuza uraia. Yaani kuuza uraia imekuwa ni chanzo cha mapato kwa nchi.

Hali ni tofauti Tanzania. Raia anapambana kupata passport, badala ya uhamiaji kuwahamasisha raia wawe na passport.

Tazama nchi zinazouza uraia duniani;

Inagharimu pesa ngapi kununua pasipoti?

Antigua na Barbuda; kuanzia $100,000

St Kitt's na Nevis; kuanzia $150,000

Montenegro; kuanzia $274,000

Ureno; kuanzia $384,000

Uhispania; kuanzia $550,000

Bulgaria; kiuanzia $560,000

Malta; kuanzia $1m

Marekani; kati ya $500,000 na $1m iliwekezwa katika biashara hiyo katika biashara hiyo na kutoa nafasi 10 za kazi

Uingereza; kuanzia dola milioni 2.5Sent using Jamii Forums mobile app
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Messages
21,310
Points
2,000

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2015
21,310 2,000
Zipo baadhi ya nchi kwa sasa zimefikia hatua ya kuuza uraia. Yaani kuuza uraia imekuwa ni chanzo cha mapato kwa nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli Marekani unatakiwa tu kununua munipal bond ya dola laki 5 hadi dola milioni moja kutegemeana na jimbo unapewa uraia chap chap

hata passpri zenyewe ni biashara .Serikali ingehamasisha kila mtanzania acghukue passport akitaka tungepata pesa za kujenga reli bila kukopa popote

mfano passport moja bei yake ni shilingi 150,000

watanzania tuko milioni 50

ukitoa pasport kwa watu milioni 10 tu kwa kila passport shilingi 150,000 ni sawa na shilingi 1500,000,000,000 yaani shilingi bilioni 1500.Kungekuwa na uhamasishaji kabisa watu wachukue passport masharti kitambulisho cha uraia.Mtu anasafiri au hasafiri atajijua
 
Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Messages
242
Points
500

Umkonto

JF-Expert Member
Joined Dec 27, 2018
242 500
Maoni yangu, serikali isiishie kulegeza masharti tu, bali inatakiwa ifanye passport kuwa chanzo cha mapato, kwa kuwahamasisha Watanzania wawe na passport.

Tatizo Tanzania tunaendekeza kaushamba fulani hivi wakati dunia ipo kasi sana.

Uhamiaji wawahamasishe Watanzania wapate passport wakatafute fursa kokote duniani.

Zipo baadhi ya nchi kwa sasa zimefikia hatua ya kuuza uraia. Yaani kuuza uraia imekuwa ni chanzo cha mapato kwa nchi.

Hali ni tofauti Tanzania. Raia anapambana kupata passport, badala ya uhamiaji kuwahamasisha raia wawe na passport.

Tazama nchi zinazouza uraia duniani;

Inagharimu pesa ngapi kununua pasipoti?

Antigua na Barbuda; kuanzia $100,000

St Kitt's na Nevis; kuanzia $150,000

Montenegro; kuanzia $274,000

Ureno; kuanzia $384,000

Uhispania; kuanzia $550,000

Bulgaria; kiuanzia $560,000

Malta; kuanzia $1m

Marekani; kati ya $500,000 na $1m iliwekezwa katika biashara hiyo katika biashara hiyo na kutoa nafasi 10 za kazi

Uingereza; kuanzia dola milioni 2.5Sent using Jamii Forums mobile app
Nyongeza;

Kwa maoni yangu, uhamiaji watembelee vyuoni kuwahamasisha wanachuo wakate passport, na muwape mbinu za kusafiri kwenda nje kutafuta fursa.

Kuwarahisishia vijana kutafuta fursa nje ya nchi, ni njia mojawapo ya kupunguza kelele zao ndani ya nchi.

Uhamiaji, tuhamasisheni vijana tuwe na passport na ikibidi mtusaidie kwenda nchi za mbali, ili tupunguze mlundikano humu ndani ya nchi. Hii itawasaidia mliobahatika kula keki ya taifa kwa Uhuru, mkiendelea kutukwamisha kusafiri, ipo siku tutakuja kuwanyang'anya keki ya Taifa ikiwa midomoni mwenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Messages
21,310
Points
2,000

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2015
21,310 2,000
Maoni yangu, serikali isiishie kulegeza masharti tu, bali inatakiwa ifanye passport kuwa chanzo cha mapato, kwa kuwahamasisha Watanzania wawe na passport.

Tatizo Tanzania tunaendekeza kaushamba fulani hivi wakati dunia ipo kasi sana.

Uhamiaji wawahamasishe Watanzania wapate passport wakatafute fursa kokote duniani.

Zipo baadhi ya nchi kwa sasa zimefikia hatua ya kuuza uraia. Yaani kuuza uraia imekuwa ni chanzo cha mapato kwa nchi.

Hali ni tofauti Tanzania. Raia anapambana kupata passport, badala ya uhamiaji kuwahamasisha raia wawe na passport.

Tazama nchi zinazouza uraia duniani;

Inagharimu pesa ngapi kununua pasipoti?

Antigua na Barbuda; kuanzia $100,000

St Kitt's na Nevis; kuanzia $150,000

Montenegro; kuanzia $274,000

Ureno; kuanzia $384,000

Uhispania; kuanzia $550,000

Bulgaria; kiuanzia $560,000

Malta; kuanzia $1m

Marekani; kati ya $500,000 na $1m iliwekezwa katika biashara hiyo katika biashara hiyo na kutoa nafasi 10 za kazi

Uingereza; kuanzia dola milioni 2.5Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu hapo ulipoandika inagharimu pesa ngapi kununua passpoti badilisha pasomeke kununua uraia
 
Mkendo

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2013
Messages
2,434
Points
2,000

Mkendo

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2013
2,434 2,000
We unaongelea ugumu wa kupata Passport, vipi ugumu wa kupata kitambulisho cha Raia..?

Zaidi wanapewa namba tu wanaambiwa kitambulisho mwakani.

Bado hizi taasisi haziko makini katika kutoa huduma zao kwa raia.
 
Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Messages
12,051
Points
2,000

Red Giant

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2012
12,051 2,000
sisi tunafanya kazi kizamani mno vitu wanavyoomba uhamiaji ni vitu vya balozini unapoomba visa!!! naona uhamiaji wamechanganyikiwa wamejigeuza maafisa wa visa wa ofisi za ubalozi za nchi za nje

Nchi zote kenya,uganda,rwanda na burundi kote huko kuomba passport huombwi vitu vya kuomba visa! ni Tanzania tu pekee Africa mashariki ambapo muomba passport anatakiwa kupeleka vitu ambavyo huombwa na balozi za nje zikitaka kukupa VISA ambako mtu hutakiwa kupeleka barua ya mwaliko,leseni ya biashara kama ulivyosema nk ili wakupe VISA uende huko.UHamiaji umegeuka ofisi ya ubalozi wa nchi za nje!!!!!

Uhamiaji wao walitakiwa tu kutoa passport kwa kutumia kitambulisho cha uraia au birth certificate tu hayo mengine wamwachie muhusika akapambane na hali yake ubalozini kwenye nchi anakoenda!!

tunapolalamika kuwa uhamiaji hawako vizuri hatutanii wako nyuma mno na wakati
Nchi zenye ishu za kijamaa huwa na tabia ya kufungia watu kama watumwa au jela. Unafikiri kwanini walijenga ukuta wa Berlin. Inabidi tuachane na sera ya ujamaa. Sheria zetu na kodi na mipango na kanuni vinaongozwa na hiyo sera. Ni zimwi lisiloonekana.
 
Forum statistics

Threads 1,390,619
Members 528,218
Posts 34,056,582
Top