Serikali ikumbukeni shule ya Sekondari Ihungo

majambota

JF-Expert Member
Dec 1, 2015
237
225
Salam kwenu wakuu,

Kama mkereketwa wa masuala ya elimu, Nina imani serikali inaitambua vyema shule hii yenye historia maridhawa.
Ikiwa imeanzishwa Mwaka 1929 na ikijulikana kama st.Thomas more kipindi hicho, imeweza kuzalisha watu wenye upeo mkubwa na dhamana mahususi hapa nchini.
Lakini ni jambo kubwa la kushangaza kusikia shule hii ikiwa ni miongoni mwa shule zenye migomo ya Mara kwa Mara na mazingira mabovu sana kwa mwanafunzi kuweza kupata elimu bora.
Chakula kisicho bora, walimu wachache na miundombinu iliyozeeka hasa vyoo na mabweni na ikikumbukwa kuwa imeanzishwa Mwaka 1929. Hii yote hupelekea shule hii iliyobeba historia ya bukoba na mkoa wa kagera kutokufanya vizuri.
Hivyo ni jukumu la serikali kuitilia maanani shule hii ya "advance" na kuweza kuondoa kero zinazowakabili wanafunzi na walimu katika utoaji wa elimu bora.

Mwisho napenda kuwahamasisha wale wote waliopitia katika shule hii na wale wenye mapenzi na elimu ya nchi yetu kuweza kuichangia kwa chochote walichonacho ili kuweza kuboresha hali ya shule hiyo. Ahsanteni..
 

am 4 real

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
570
1,000
Umenikumbusha mbali sanaaa.. Kuna mengi sana kila nikikumbuka ihungo boyz... Moja ya shule kongwe sana tz
Nafrai kua product ya ihungo.... Japo ume eleza "maswahibu"
Tulikua tuna iita "jkt ihungo" pale watoto walio pitia good life walikua hawakai kutokana na hardships kama ulivyo eleza hapo juu.
Ile shule ingepata wasimamiz wazur.. Ingetisha sanaa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom