Serikali ikubali uraia pacha na kutoa likizo ya kodi kwa wawekezaji wazawa ili kuchochea ajira

iranna

Senior Member
Aug 4, 2021
149
617
Nchi yetu imebarikiwa maji, ardhi yenye rutuba, watu wenye afya, Rasilimali lukuki lakini 60% ya raia wanaishi katika umasikini wa kutupwa.

Kitu kinachowashinda wengi ni mitaji ya kuanzisha biashara. Hili si tatizo kubwa kama tukiwashirikisha diaspora. Diaspora anaweza kupata mtaji wa £100,000. Kukiwa na mipango mizuri, mtaji huu unaweza kuzalisha ajira 50 rasmi na zaidi ya hizi kama vibarua.

Hakuna diaspora atakae kuwa tayari kuwekeza pesa hizi bila usalama wake kisheria. Mkikubali uraia pacha mtawasaidia wengi kuwa na imani na uwekezaji nyumbani.

Diaspora wa Tanzania nchi za nje wanaweza kufika 5,000. Hawa wote wakijumlishwa wanaweza kuwa chachu ya maendeleo kwetu. Tatizo la kodi kuwa juu katika kuanzisha biashara linaumiza wengi. Kama mnaweza kuwapa likizo mpaka biashara ikae sawa, serikali itanufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na kodi ya kampuni na pia ya wafanyakazi wenye ajira rasmi.
 
Back
Top Bottom