kishegheni
Member
- Mar 6, 2012
- 21
- 85
Nina kitu kinanishangaza,. kunsikitishai na kushindwa kuelewa sababu za serikali kuruhusu wanafunzi kusitisha masomo ili kuwasubiri na kuwashangilia wasanii wa muziki au filamu wanapofika mashuleni kutoa misaada.
Huu utaratibu umeendelea kwa.kipindi kirefu mpaka sasa. Hii leo tumeona kwenye Mitandao watoto wa shule wakiimba wimbo wa "Nyegezi" uliofungiwa na BASATA mbele ya Mkuu wa Wilaya na Diamond na team yake ya Wasafi wakati walipotembelea shule moja huko Iringa..
Mbona watu wengi wanatoa misaada mikubwa mikubwa kusaidia mashule na sehemu mbalimbali lakini hatuoni watotkowakitoka madarasani na kukusanyika ili kuwasubiri watoa misaada 'na wala hawajitangazi kwenye mitandao wala magazeti ka.wasanii. Hii tabia imekithiri kwa wasanii zaidi na sielewi wanafanya hivi kwa nia gani. Misaada yenyewe haijulikani ni misaada ya aina gan wanayotoa. Sana sana wanatafuta umaarufui.
Hata matamasha wanayofanya wasanii mikoani ndio kabisaaa shughuli zote ndio zinasimama kuanzia mkoani mpaka wilayani. Utasikia wanakutana na Mkuu wa Mkoa mara Mkuu wa Wilaya. Mbona watu wengine wakitembelea mikoani hawafanyi hivi.
Waziri wa Elimu na Waziri wa TAMISEMI tunaomba.mkomeshe tabia hii kwani inawadhalilisha viongozi, wazazi, walimu na kuwapotezea watoto wetu muda wa kusoma.
Kwa kweli jambl hili linatukera sisi wazazi.