Serikali 'ikisitisha' kila biashara watu wataishi vipi?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,229
116,840
Nimeshangaa kusoma kwenye media kuwa Waziri mkuu 'kasitisha uvunaji wa mbao'
na haiko clear kwa mda gani

Juzi nilikuwa natafuta kifusi maeneo ya Bunju nikakuta pia malalamiko
na maelezo kuwa 'serikali imesema Dar hakuna machimbo rasmi ya kokoto.mchanga,vifusi na kadhalika
hivyo zoezi la kuzuia shughuli hizo liko mbioni kuja

Kama una deal na shughuli za ujenzi utajua tu kila tangazo la 'kusitisha' chochote
hupelekea kwanza kupanda kwa bei ya bidhaa husika au kuadimika kabisa....

Sasa kwa mwendo huu very soon mbao za kujengea na bidhaa zingine za ujenzi kama kokoto,mchanga, mbao,vifusi zitapanda au kuadimika

na itapelekea baadhi ya watu kushindwa ama biashara zinazotegemea bidhaa hizo
au kushindwa ujenzi hata wa mtu mmoja mmoja.... na hilo litapelekea 'maafa' ya kiuchumi kwa watu wengi.....

Ushauri wangu serikali ingekuwa inatazama kwanza namna ya kukwepa kuleta 'panic'
kwenye biashara za watu....na kukwepa kuja na matamko yanayo changanya
au kuwaletea 'ulaji'

i hope saga ya sukari imetufundisha 'athari' za matamko kama haya....
biashara zikiharibika..na yenyewe serikali itakusanya mapato kutoka wapi?
 
dah umenena vyema mkuu, nadhani inshu yasukari ndio ingekuwa funzo lakutotoa kauli bila kuangalia faida zake nahasara zake nizipi, ila kwasasa kauli nyingi zaserikali zmekuwa nahasara kubwa kuliko faida.
 
La sukari halijawafundisha bado
 
Tulisema ni mwanzo labda hawajazoea ila hadi leo matamko yao hawajaona athari zake kwenye jamii?
 
Kumbuka falsafa mojawapo ya Raia Namba Moja wa Tanzania:

1.Kuwafanya wanaoishi kama Malaika waishi kama Mashetani.

Tafsiri isiyo rasmi: wengi wa walalahoi huishi maisha ya kishetani.

"Serikali 'ikisitisha' kila biashara watu waishi vipi?Jibu la swali lako ni :...ili waishi kama mashetani...
 
Nguvu ya soko inatakiwa kujiendesha kulingana na upatikanaji wa bidhaa na idadi ya wateja wenye mahitaji ya bidhaa husika.
Kama shida ni mbao,uhamasishaji wa zoezi la 'kata mti panda mti' ndio ingekuwa hatua ya kuchukua!
ATHARI YA KUWEKA MARUFUKU:

1.Sekta zinazotegemea bidhaa ya mbao katika uzalishalishaji zitaathirika
2.Mzunguko wa fedha na ajira utaathirika
3.Kuleta hofu kwa wafanyabiashara waliopo na wanaotaka kuwekeza katika sekta husika
4.Zoezi la utengenezaji wa madawati utachelewa.
Ufumbuzi:
1.bei ya soko iachwe,Serikali ibaki kusimamia sheria na kanuni
2.Kabla ya kuchukua hatua kuna haja ya kuwashirikisha wadau.
 
wangekuwa wanaongea na wadau wa sekta kabla ya matamko ingesaidia sana
 
52b538722cd21ee9c173bbd636fc7914.jpg
 
Nimeshangaa kusoma kwenye media kuwa Waziri mkuu 'kasitisha uvunaji wa mbao'
na haiko clear kwa mda gani

Juzi nilikuwa natafuta kifusi maeneo ya Bunju nikakuta pia malalamiko
na maelezo kuwa 'serikali imesema Dar hakuna machimbo rasmi ya kokoto.mchanga,vifusi na kadhalika
hivyo zoezi la kuzuia shughuli hizo liko mbioni kuja

Kama una deal na shughuli za ujenzi utajua tu kila tangazo la 'kusitisha' chochote
hupelekea kwanza kupanda kwa bei ya bidhaa husika au kuadimika kabisa....

Sasa kwa mwendo huu very soon mbao za kujengea na bidhaa zingine za ujenzi kama kokoto,mchanga, mbao,vifusi zitapanda au kuadimika

na itapelekea baadhi ya watu kushindwa ama biashara zinazotegemea bidhaa hizo
au kushindwa ujenzi hata wa mtu mmoja mmoja.... na hilo litapelekea 'maafa' ya kiuchumi kwa watu wengi.....

Ushauri wangu serikali ingekuwa inatazama kwanza namna ya kukwepa kuleta 'panic'
kwenye biashara za watu....na kukwepa kuja na matamko yanayo changanya
au kuwaletea 'ulaji'

i hope saga ya sukari imetufundisha 'athari' za matamko kama haya....
biashara zikiharibika..na yenyewe serikali itakusanya mapato kutoka wapi?
Mkuu wee unaonea huruma Watz!!!.,,ni watu Hovyo sana kama walikurupuka ishu ya Sukari mpaka Leo tunanunua zaidi ya elf3 kwa kilo kutoka 1800 na watz hadi Leo wanashangilia kwamba Nchi inaenda vyema unadhani hata Bidhaa zinazohusu Ujenzi zikipanda nani atajali watu wataelendelea kuimba utukufu kama kawaida...Nchi ina wajinga wa viwango vya kutiliwa Mfano Duniani...maana MTU hajionei huruma hata yy mwenyewe Sababu chama duh...!!
 
Inasikitisha sana
 
Back
Top Bottom