Serikali ikimulike kiwanda cha nguo cha urafiki. Huu ni ushauri wa bure kwa waziri wa viwanda atakayeteuliwa

Pepe kale

Member
Jul 16, 2020
11
4
Baada ya uchaguzi kuisha na uteuzi wa Waziri Mkuu na uundwaji wa Baraza la Mawaziri kukamilika, ninaishauri SERIKALI kupitia kwa Waziri wa VIWANDA, biashara na uwekezaji akimulike kiwanda cha NGUO cha urafiki kinachojulikana Kama (TANZANIA-CHINA FRIENDSHIP TEXTILES CO) kilichopo Ubungo jijini Dar es Salaam.

Naibu meneja Mkuu wa kiwanda hicho Bw. Nkelebe pamoja na marketing manager wa kiwanda hicho bi.selina wamekua na ushirikiano wa kukihujumu kiwanda hicho wakishirikiana na walinzi wasio waaminifu kiwandani happy pamoja na baadhi ya wafanyakazi wachache, akiwemo estate manager wa kiwanda hicho Bw. Sunday , kupakia mizigo ya vitenge gari ya Bi.Selina kila siku kinyume cha utaratibu, kisha Bi. Selina huvigawanya katika mafungu vitenge hivyo alivyovichukua kiwandani kwa njia ya magendo , ambapo baadhi huvihifadhi katika kibanda chake alichokiweka pembezoni mwa moja ya majengo ya kiwanda hicho, ambapo katika kibanda hicho huwa anazuga Kama anauza juice huku nyuma ya pazia akikitumia Kama maficho ya muda ya vitenge hivyo alivyokwapua kiwandani hapo akishirikiana na maofisa niliowataja hapo juu. Baada ya mzigo huo kutofuatiliwa kwa muda Fulani, kila ifikapo muda wa jioni huupakia mzigo huo wa vitenge na kuupeleka kuuza kwa Bei ya jumla kwa wafanyabiashara wa rejareja na Pesa zinazopatikana anagawana na mnyororo wote unaofanikisha wizi huo, kila siku.

Ndio maana biashara katika kiwanda hicho imeonekana kuyumba Sana lakini cha kushangaza maafisa hao wanaendelea kunawiri na kunenepa ikiwa kundi kubwa la wafanyakazi kiwandani hapo hawalipwi stahiki zao miaka nenda-rudi.

Ufisadi mwingine Ni katika malipo ya wafanyabiashara waliopanga kwenye majengo ya kiwanda hicho, naibu meneja Mkuu wa kiwanda hicho Bw. Nkelebe amemuelekeza muhasibu kutotoa risiti za EFD kwa wanaolipia pango, Bali wao hutoa risiti za kuchora na mkono, Kisha baadhi ya Pesa hupelekwa bank kugawanywa katika akaunti ya kiwanda na akaunti binafsi ya naibu meneja Mkuu wa kiwanda hicho. Hali hiyo imepekelea kwa kiasi kikubwa kiwanda hicho kupoteza mapato ambayo hupotelea mifukoni mwa watumishi hao wasio waaminifu.

Ufisadi mwingine ni kwenye malipo ya wafanyakazi kiwandani hapo, kinachofanyika Ni kuruhusu mishahara ya baadhi ya wafanyakazi bila wafanyakazi hao kujua, Kisha mishahara hiyo ambayo naibu meneja wa kiwanda hicho huipanga ilipwe kwa cash, huiweka katika akaunti yake binafsi na kuendelea kujineemesha huku akiwalimbikizia mishahara wafanyakazi hao.

Mimi Ni mwanaharakati binafsi niliejitolea kufanya uchunguzi wangu' binafsi kiwandani hapo baada ya kuomba kazi na Kisha kufanikiwa kuwahoji baadhi ya watumishi katika kiwanda hicho na kufichua uozo huo.

Ninakushauri Waziri wa VIWANDA utakayeteuliwa, hatua ya Kwanza ufike kiwandani hapo Kama ambavyo serikali ilimshughulikia aliekua meneja Mkuu wa kiwanda hicho Bw.Swai.

MAENDELEO YANALETWA NA MIMI NA WEWE. TUSHIRIKIANE KUUTOKOMEZA UMASIKINI KWA KUFANYA KAZI KWA BIDII.
 

Attachments

  • download.jpeg
    download.jpeg
    9.9 KB · Views: 12
Hivi ukienda pale kiwandani ukataka khanga kwa Bei ya jumla wanauza kwa sh ngapi kwa kila pic na zinaanzia pic ngapi..?

Samahani kwa kutoka nje ya mada.
 
Ƨɛяικαℓι ʏα мαʝιʓι нαтα мαƨнιяικα ʏακɛ ʏαиαɛи∂ɛƨнωα κιʝιʓιʝιʓι тʋ.
 
Back
Top Bottom