Serikali Ikiamua Kuilipa Dowans Sitta na Mwakyembe Lindeni Heshima Zenu kwa Kujiuzuru

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Wana JF,
Ni ushauri wangu tu kwa hawa jamaa wawili ambao walijitoa kimasomaso kuzungumza hadharani mbele ya vyombo vya habari kupinga kampuni ya dowans kulipwa mabilioni ya fedha zinazotokana na wananchi maskini. Najua serikali imejipanga kwa udi na uvumba kuilipa dowans. Endapo mpango huo utatekelezwa, nawashauri mzee sitta na mwakyembe wajiuzuru mara moja ili walinde heshima yao mbele ya umma wa watanzania. Kwa kufanya hivyo, siyo tu watakuwa wamejijengea heshima kubwa, bali itakuwa ni rekodi ya aina yake katika historia ya nchi yetu. Ni jambo ambalo halitakuja lisahaulike katika historia ya nchi yetu. Kuendelea kukaa kwenye serikali ya kidharimu isiyowajali wananchi wake, kutawavunjia heshima na hata RA mwenyewe atawadharu na kuwakebehi sana. Kazi kwenu sitta na mwakyembe. Yetu macho na masikio.
 
Hao pia ni mafisadi tuu kama wenzao sema tuu wamepata nafasi kuwanyooshea vidole wenzao. Waroho wa madaraka hawawezi kujiuzuru hata uwafunge kamba. Mafisadi tuuuuuu
 
hawana huo ubavu,viongozi wengi wa tanzania ni wasanii tu.

Sehemu ya baraza la mawaziri wasioafiki malipo ya kifisadi kwa Dowans kama sisi walipakodi ni lazima kulinda heshima zenu na maslahi yetu sisi Watanzania kwa kujiuzulu maramoja.

Hatua za kufuatia hapo mtuachie sisi kazi hiyo. Kuna shughuli pevu hapa.
 
Sehemu ya baraza la mawaziri wasioafiki malipo ya kifisadi kwa Dowans kama sisi walipakodi ni lazima kulinda heshima zenu na maslahi yetu sisi Watanzania kwa kujiuzulu maramoja.

Hatua za kufuatia hapo mtuachie sisi kazi hiyo. Kuna shughuli pevu hapa.

Tatizo la viongozi wetu wengi wao wanatumikia matumbo yao. Siyo rahisi kujiuzuru.
 
Back
Top Bottom