Serikali ikague utendaji Mamlaka ya Afya na USalama Kazini (OSHA)

Mamboleo

Member
Oct 15, 2008
69
38
Pamoja na Waziri wa Sera,Ajira ,Kazi vijana na walemavu Mh.Jenista Mhagama kutoa maagizo kwa waajiri nchi kuhakikisha maeneno yao ya kazi yawe yamesajiliwa na OSHA,kumekuwa na usumbufu na urasimu mkubwa kutoka kwa watumishi wa idara hiyo ya serikali dhidi ya waajiri wanaotaka kutimiza leongo na agizo la kusajili maeneo yao ya kazi.

Ukiacha usajili wa eneo la kazi " Registration of Workplace" pia kuna ukaguzi wa maeneo ya kazi unaofanywa na wakaguzi wa OSHA kwa ajili ya kupata "Compliance Licence" endapo mwajiri atakidhi matakwa yote kwa mujibu wa taratibu na sheria.

Katika eneo hili la compliance licence ndipo urasimu unapokuwepo ili kumfanya mwajiri atoe rushwa kwa wakaguzi.Kwa mfano..utakuta ripoti ya ukaguzi wa afya kwa wafanyakazi-medical examination.wakaguzi wengi huchelewesha ripoti na hivyo kufanya zoezi zima kuchukua hata zaidi ya mwezi.Pia taratibu za ndani za Mamlaka kupitia ripoti za ukaguzi kwa ajili ya kutoa compliance licence zinakuwa na ukiritimba na kuchukua muda mrefu kwa ajili ya kujenga mazingira ya utoaji rushwa.Inakuwaje maombi ya cmpliance license yachukue zaidi ya miezi 2 au 3?

Pamoja na utendaji mzuri wa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hii..ni wakati muafaka kwa serikali kukagua utendaji wa OSHA kwa sababu wafanyakazi wengi na hasa wa ofisi ya ukanda wa Dar es salaam na Pwani umejaaa ubabaishaji na ukiritimba.

Pia ni wakati muafaka kwa serikali kuangalia namna ya kufanya maombi na taratibu za kutoa compliance licence na certificate of registration kufanyika kwa njia ya mtandao ili kupunguza ukiritimba.Pia mamlaka hii inapaswa kuajiri wafanyakazi wao kwa sababu baadhi ya wafanyakazi wake sio waajiriwa wa kudumu na wao pia ni chanzo cha tatizo.

Ni muhimu serikali ichukue hatua madhubuti kuondoa vikwazo vya OSHA kwa wawekezaji wa nchi hii wanaokwazika kwa utendaji mbovu kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka hii.
 
mimi naona osha wako vizuri, labda kuna jambo jingine. wao husimamia matakwa ya kisheria jambo ambalo wadau hawajalizoea, pia wengi wanataka njia za mkato hawataki utaratibu wa kisheria ndio maana wanapokataliwa hifikiri ni rushwa inatakiwa....
 
Back
Top Bottom