Serikali ikae meza moja na Vyama vya upinzani

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Mimi ni mtu wa kawaida na ni Mtanzania. Kesi ya Mbowe ndiyo sasa imechukua nafasi kubwa katika mijadala baina ya wanannchi, kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya ndani na nje.

Sisi sote ni Watanzania na tunatakiwa tupendane, tushikamane, tuwe wamoja bila kujali itikadi za vyama. Leo Mhe. Mbatia amezungumza jambo la maana sana kuwa Serikali ikae meza moja na Vyama vya upinzani iwasikilize wanachotaka kwa mustakabali ya nchi hii.

Tangu Mbowe atiwe nguvuni Serikali imekwishatumia gharama kubwa katika shauri hili gharama ambayo ingeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo. Chonde chonde Mhe. Rais chukua muda ukutane na vyama vya upinzinzani usikilize hoja zao kuliko sasa hivi kuna mgawanyiko mkubwa wa wananchi kitu ambacho hakileti afya.

Salamu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Waache washupaze shingo zao na mwisho wa siku zitavunjika tu.

Wanadhani watakuwa na nguvu hizo hizo walizonazo siku zote na hata milele.

Hawajui kuwa wao kama wao hawa kina Samia Suluhu Hassani na wenzake, wanaweza kuepuka adhabu ya sasa.

Lakini watoto wa watoto wao wanaweza kuwajibika kwa haya wafanyayo sasa baba na mama zao.
 
Mimi ni mtu wa kawaida na ni Mtanzania. Kesi ya Mbowe ndiyo sasa imechukua nafasi kubwa katika mijadala baina ya wanannchi, kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya ndani na nje.

Sisi sote ni Watanzania na tunatakiwa tupendane, tushikamane, tuwe wamoja bila kujali itikadi za vyama. Leo Mhe. Mbatia amezungumza jambo la maana sana kuwa Serikali ikae meza moja na Vyama vya upinzani iwasikilize wanachotaka kwa mustakabali ya nchi hii.

Tangu Mbowe atiwe nguvuni Serikali imekwishatumia gharama kubwa katika shauri hili gharama ambayo ingeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo. Chonde chonde Mhe. Rais chukua muda ukutane na vyama vya upinzinzani usikilize hoja zao kuliko sasa hivi kuna mgawanyiko mkubwa wa wananchi kitu ambacho hakileti afya.

Salamu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Inaonekana washauri wa mama ni wale wale wa JPM.
 
Back
Top Bottom