Serikali ijitathimini, kuna wimbi kubwa la vijana kuacha kazi ndani ya kipindi hiki cha miaka 7

Wakiacha kazi serikali kamwe haiwezi kuhuzunika..kuna majobless kibao mtaani ambao hata kwa nusu mshahara watafanya kazi.
Kumbe hata wewe unaviji akili kidogo vimesalia kichwani kwako ,nilidhani ni zero kabisa.leo kwa mara ya kwanza nimeona kiji akili kichwani mwako
 
Miaka 6 bila nyongeza ya mishahara aliumia roho sana. hivi hawana imani ya mungu watawala?
Magufuli alipunguza mfumuko wa bei na kupunguza mzigo kwa masikini kama umeme wakati wa kikwete kila siku ulikuwa unapanda na bado tanesco ilikuwa wanadai inapewa rudhuku ,bei ya mafuta ilikuwa vizuri ,elimu bure sijui mlikuwa mnalalamika bila ya kutumia akili viwanja vilishuka bei ,vyumba na nyumba za kupanga bei ikashuka na kubaki tulivyu tofauti na kipindi cha kikwete.
Sasa mtajua amjui maana magu hayupo tena gharama za maisha zitapanda sana elimu bure kwisha kikao kimefanyika kuwa iondolewe kimtindo mtindo ,dhamani ya hela inakwenda kudondoka kilimo kinapolomoka kwa kasi nauli ya mabasi zinakwenda kupanda zaidi,
 
Concern yangu ni kwamba ifike wakati serikali iboreshe mazingira ya kazi kwa kuzitatua changamoto za wafanyakazi ambazo zinawafanya waache kazi au wafanye kazi bila ya kuifurahia hivyo kusababisha udhaifu wa huduma bora kwa wananchi. Mazingira ya kazi yakiwa safi na mfanyakazi akiifurahia kazi yake hata kama maslahi ni kidogo, atafanya kazi kwa moyo..!
Mkuu umewahi kukaa Jobless kwa muda gani ?

Umewahi kufanya kazi sekta binafsi ?

Umewahi kujiajiri ?

Anyway, kama huifurahii kazi ACHA KAZI ukatafute utajayoipenda, maisha yenyewe ndio haya haya.

Usiingie kwenye Ajira na matamanio yako ambayo hayapo, utakuwa dissappointed sana.

Mfano: Mimi kama graduate kwenye graduate kwenye kampuni za ulinzi, hata siku moja huwezi kunikuta nalalamika kwasababu sekta niliyopo naijua vizuri IN&OUT.

Huwezi kufanya kazi hii, halafu ukategemea utajenga ghorofa. Utakuwa zuzu.

Fanya kazi yako kwa wakati husika, ukichoka unaacha tu, unakaa nyumbani.

Na hakuna kitu rahisi kama kuacja kazi. Hakuna Mwajiri atakayehangaika na wewe au kukufuata nyumbani uende kazini kwa nguvu.
 
Halafu kazi Serikali zinaenda kwa Wahamiaji haramu, hii Nchi itakuja kuwa Koloni la Burundi
Ili ni tatizo kubwa sana sijui usalama wa taifa wanafanya kazi gani ,rain feki kuingia kwenye system za serikali ni dharau na hatari sana
 
Nina washkaji zangu kadhaa nilisoma nao wameacha kazi za serikali. Na jana nimekutana na mwanangu nilikua nae room moja chuo ameniambia ameacha kazi aliyokua anaifanya huko serikalini.

Nilipomhoji akanambia ishu ni maslahi ilihali muda mwingi anautumia kazini, hata muda wa kufanya shuguli binafsi za kumuingizia kipato hana, ameamua aache kazi afanye ishu zake.

Swali la kujiuliza, ni kweli hawa wote wana tamaa na hawaridhiki na mshahara wao? Au ni kweli huko serikalini maslahi hamna na unatoil vya kutosha??
wanaofanya kazi serikalini wengi ni wale uwezo wao wa kufikiri upo chini.

Sio Mimi ni CAG Assad.
 
Serikalini inabidi uwe mvumilivu, afisa utumishi tu anaweza kukupiga danadana usipande cheo hata miaka 10, hata kukaa kwenye position utafanyiwa kila figisu uonekane hufai hadi ma ushirikina yanatumika humo, huko waachieni waliotoka familia duni wakakanyagane. Ambao wapo comfortable ni wenye connection ya kukaa sehemu nyeti, mfano BOT, TRA na kwingineko.....
Sure kabisa
 
Nina washkaji zangu kadhaa nilisoma nao wameacha kazi za serikali. Na jana nimekutana na mwanangu nilikua nae room moja chuo ameniambia ameacha kazi aliyokua anaifanya huko serikalini.

Nilipomhoji akanambia ishu ni maslahi ilihali muda mwingi anautumia kazini, hata muda wa kufanya shuguli binafsi za kumuingizia kipato hana, ameamua aache kazi afanye ishu zake.

Swali la kujiuliza, ni kweli hawa wote wana tamaa na hawaridhiki na mshahara wao? Au ni kweli huko serikalini maslahi hamna na unatoil vya kutosha??
Waondoke tu,mbona wanaotafuta ajira ni wengi.Na hata hivyoo,mbona kuacha kazi ni kawaida,ukipata a
better alternative you go.
 
Kuacha kazi sio dhambi na wala sio kuvunja sheria. Lakini kwa nini kwa kipindi hiki kifupi hili limeongezeka kwa kasi? Kuna wengine hata miaka 5 ya kazi haijafika mtu anaacha..! Ndio maana nikasema kuna haja ya serikali kujitathimini
 
Back
Top Bottom