Serikali ijitathimini, kuna wimbi kubwa la vijana kuacha kazi ndani ya kipindi hiki cha miaka 7

DustBin

JF-Expert Member
Jun 3, 2021
544
558
Nina washkaji zangu kadhaa nilisoma nao wameacha kazi za serikali. Na jana nimekutana na mwanangu nilikua nae room moja chuo ameniambia ameacha kazi aliyokua anaifanya huko serikalini.

Nilipomhoji akanambia ishu ni maslahi ilihali muda mwingi anautumia kazini, hata muda wa kufanya shuguli binafsi za kumuingizia kipato hana, ameamua aache kazi afanye ishu zake.

Swali la kujiuliza, ni kweli hawa wote wana tamaa na hawaridhiki na mshahara wao? Au ni kweli huko serikalini maslahi hamna na unatoil vya kutosha??
 
Miaka 6 bila nyongeza ya mishahara aliumia roho sana. hivi hawana imani ya mungu watawala?
 
Nina washkaji zangu kadhaa nilisoma nao wameacha kazi za serikali. Na jana nimekutana na mwanangu nilikua nae room moja chuo ameniambia ameacha kazi aliyokua anaifanya huko serikalini. Nilipomhoji akanambia ishu ni maslahi ilihali muda mwingi anautumia kazini, hata muda wa kufanya shuguli binafsi za kumuingizia kipato hana, ameamua aache kazi afanye ishu zake.

Swali la kujiuliza, ni kweli hawa wote wana tamaa na hawaridhiki na mshahara wao? Au ni kweli huko serikalini maslahi hamna na unatoil vya kutosha??
wote wanaojitambua wanaacha
 
Waswahili wanasema utamu wa ngoma uingie ucheze kiukweli ukiwa nje ya ajira za serikalini unakuwa na shauku sana ya kuajiriwa ila ukiajiriwa ukafanya kazi hata miaka 2 tu unatamani uache kazi na ujiajiri kutokana na maslahi madogo Tanzania wanaofaidi nchi ni wanasiasa tu mkija kugundua mmechelewa
 
Serikalini inabidi uwe mvumilivu, afisa utumishi tu anaweza kukupiga danadana usipande cheo hata miaka 10, hata kukaa kwenye position utafanyiwa kila figisu uonekane hufai hadi ma ushirikina yanatumika humo, huko waachieni waliotoka familia duni wakakanyagane. Ambao wapo comfortable ni wenye connection ya kukaa sehemu nyeti, mfano BOT, TRA na kwingineko.....
 
Waswahili wanasema utamu wa ngoma uingie ucheze kiukweli ukiwa nje ya ajira za serikalini unakuwa na shauku sana ya kuajiriwa ila ukiajiriwa ukafanya kazi hata miaka 2 tu unatamani uache kazi na ujiajiri kutokana na maslahi madogo Tanzania wanaofaidi nchi ni wanasiasa tu mkija kugundua mmechelewa
Msichielewa ni kwamba maslahi ya serikalini yanakuwa madogo kutokana na mindset tu. Siku zote mfanya kazi unapigia mahesabu pesa ambayo haujaishika mkononi ila unauhakika utaipata japo ni kwa muda mrefu, so unaipangia matumizi yote hata kwa miaka mitano inayo, so as time goes on inaanza kuchoka kusubiri na unaona walio mtaani wanaraha kuliko wewe.
Lakini mtu aliyejiajili anapanga mahesabu kwa pesa aliyonayo mkononi ingawa kuipata kwake alichukua risk nyingi. Imagine mtu anapeleka bidhaa sehemu Hana uhakika ila anapofanikiwa ku make money ndipo anapanga matumizi.

Lakini ukikaa chini ukafanya mahesabu Hawa watu unakuta wanapata pesa sawa au hata kama wako tofauti basi ni kidogo sana ila wa kwenye ajira anakuwa amepiga mahesabu ya muda mrefu na kujiona kasha win maisha.
 
Nina washkaji zangu kadhaa nilisoma nao wameacha kazi za serikali. Na jana nimekutana na mwanangu nilikua nae room moja chuo ameniambia ameacha kazi aliyokua anaifanya huko serikalini.

Nilipomhoji akanambia ishu ni maslahi ilihali muda mwingi anautumia kazini, hata muda wa kufanya shuguli binafsi za kumuingizia kipato hana, ameamua aache kazi afanye ishu zake.

Swali la kujiuliza, ni kweli hawa wote wana tamaa na hawaridhiki na mshahara wao? Au ni kweli huko serikalini maslahi hamna na unatoil vya kutosha??
Wakiacha kazi ndio vizuri wawaachie wengine.

Ukipata sehemu wanayolipa vizuri kuliko serikalini wewe nenda.

Juzi tu hapa serikali imetangaza ajira 9000 wameomba watu 130,000.

Kwahiyo database yao ina replacement ya kutosha tu.
 
Concern yangu ni kwamba ifike wakati serikali iboreshe mazingira ya kazi kwa kuzitatua changamoto za wafanyakazi ambazo zinawafanya waache kazi au wafanye kazi bila ya kuifurahia hivyo kusababisha udhaifu wa huduma bora kwa wananchi. Mazingira ya kazi yakiwa safi na mfanyakazi akiifurahia kazi yake hata kama maslahi ni kidogo, atafanya kazi kwa moyo..!
 
Back
Top Bottom