Serikali ijipange kuwapunguzia wananchi ugumu wa maisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ijipange kuwapunguzia wananchi ugumu wa maisha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Apr 26, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Serikali ijipange kuwapunguzia wananchi ugumu wa maisha

  Ugumu wa maisha ni kilio kinachosikika kila kona ya nchi hivi sasa. Na hasira za wananchi zinachochewa zaidi na tofauti kubwa iliyopo kati ya walionacho na

  wasionacho. Na zaidi pia ufisadi uliojikita katika ngazi mbalimbali za uongozi.
  Sauti zinazolilia hali ngumu ya maisha ya wananchi siyo toka kwa wananchi pekee

  bali hata viongozi wa dini nchini wameshika bango kuhoji watawala wana mikakati gani kupatia ufumbuzi kelele hizo.

  Wiki hii, kiongozi mmoja wa dini, Mchungaji wa Kanisa la Kilutheri Tanzania(KKKT), Kanisa la mjini Iringa, Enock Mlyuka, amesema kuwa kasi ya viongozi kujilimbikizia mali na kusahau watu maskini inatisha na akatahadharisha kuwa isipodhibitiwa inaweza kuliingiza taifa mahali pabaya.

  Akabainisha wazi kwamba viongozi walio wengi wameweka kando wajibu wao na kusahau hali ngumu inayowakabili wananchi, jambo ambalo ametoa mwito kwa

  watawala kuangalia namna ya kupatia ufumbuzi na hasa kwa kuondoa tofauti ya matabaka kati ya walionacho na wale wasionacho.

  Kwamba mgawanyiko huo kama hautadhibitiwa, unaweza kuligawa taifa kutokana na viongozi kushindwa kutekeleza majukumu yao na badala yake kujikita katika maslahi binafsi.

  Ni faraja kubwa kwamba serikali kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM) imeonyesha dhamira ya dhati kushughulikia kero kuu za wananchi likiwemo la ufisadi ambao unaitafuna nchi kiasi cha viongozi wengi kuendekeza ubinafsi badala ya kuwatumikia wananchi.

  Malalamiko mengi ya wananchi yanatokana na viongozi waliopewa dhamana katika ngazi mbalimbali kutowajibika vile ipasavyo. Ni jukumu la serikali sasa kuzinduka na kufuatilia nyendo za watumishi wake katika ngazi zote na kupima utendaji wao kulingana na kanuni za utumishi na maadili ya uongozi.

  Ukianzia ngazi za chini kwenye serikali za mitaa, yapo maagizo mengi ya serikali wanayopewa wenyeviti wa serikali hizo kuyasimamia lakini hayatekelezwi. Wakishachaguliwa mchezo unakuwa umeishia hapo hapo.

  Kwa mfano, agizo la kuanzisha ulinzi shirikishi ambao ni muhimu katika maeneo ya makazi kujilinda dhidi ya uhalifu. Wenyeviti wa Mitaa katika baadhi ya maeneo tangu wamechaguliwa hawajakutana na wananchi kusikiliza kero zao. Na hata kama wamekutana nao, hakuna mrejesho kwamba nini kinachoendelea. Kwingine ulinzi huu haujaanzishwa.

  Maeneo mengine hayapitiki, madaraja mabovu, barabara hazipitiki ili mradi tu wananchi wanataabika mbali na kilio chao kukitoa muda mrefu. Kwa ujumla maeneo mengi wananchi hawasikilizwi japokuwa viongozi wapo. Watu wamekuwa wabinafsi hawashughulikii kero za wananchi.

  Zipo kelele za bei za vyakula, vijana wengi hawana kazi, wizara inayohusika na eneo hilo ipo, dawa hospitalini, zahanati na vituo vya afya ni haba. Wagonjwa wengi huishia kuelekezwa wakanunue maduka ya dawa ambayo mengi ni ya watumishi wa

  umma. Bohari ya madawa ya serikali hutoa dawa kwa hospitali zote za serikali.
  Sasa kwanini uhaba uwepo mkubwa kiasi hicho? Lipo tatizo la usimamizi hapa ambalo serikali inafaa ilivalie njuga na kudhibiti wezi wanaovuruga zoezi hilo la kupeleka dawa hospitalini. Yapo mapungufu mengi katika utoaji wa huduma hata

  kwenye sekta ya kilimo. Serikali inajitahidi kusimamia usambazaji wa pembejeo za kilimo lakini bado wapo mafisadi wasioitakia mema nchi hii huvuruga zoezi hilo. Serikali ijipange kuondoa wasaliti hawa.

  Imulike watendaji wake serikalini hasa wale ambao wanatakiwa kuwa karibu na wananchi. Mawaziri pamoja na majukumu ya kiofisi, wanapaswa pia kuwatembelea wananchi kusikia malalamiko yao siyo kuwaachia viongozi wakuu wa nchi kama vile Rais au Waziri Mkuu ndio waende huko. Wananchi wangependa kumuoa waziri

  anayesimamia wizara fulani na hakika watakuwa na maswali ya kumoji. Huyo ndiyo kiongozi wa watu.
  Wakuu wa mikoa na wilaya siyo kusubiri taarifa tu ofisini. Nendeni kwa wananchi mkazungumze nao kwani wanayo mengi ya kuwaeleza na bila shaka kwa utaratibu

  huo itakuwa rahisi kujua ukubwa wa tatizo na namna ya kulipatia ufumbuzi mapema. Huo ndio utawala bora.
  Vinginevyo wananchi wanafikia mahala wanajiona wako peke yao hakuna viongozi

  wanaowatembelea kuona hali ya maisha wanayoishi. Na hicho ndicho kinachowasikitisha wananchi walio wengi kwamba wameachwa hawasikilizwi na mikakati ya kuwapunguzia umasikini hawaioni kivitendo.
  Ndio maana tunasema ni busara sasa serikali yetu ijipange upya na kuona wapi imekwama na kurekebisha mambo ili kurejesha imani ya wananchi.
  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
Loading...