kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,418
- 7,206
Lazima kutambua wakati wote benki ya dunia ni benki tu kama zingine kipaumbele chake ni faida. Wenye hisa wakubwa ni marekani na nchi za ulaya. Kwa mfumo wa kibepari wafaidika namba moja na benki ya dunia ni mabepari wakubwa wa nchi hizo.
Kutokana na hivyo nchi changa sio rahisi kupata maendeleo kwa kukopa benki ya dunia kwa vile benki hiyo inataka iwapangie wakope kwa miradi yenye maslahi na nchi kubwa za kibepari na sio kuwaletea wananchi maendeleo.
Kuna kila dalili ugonjwa wa covid 19 umeundwa kama fursa kubwa kwa mabepari wa madawa ya binadamu marekani na ulaya kutengeneza fedha.
Fursa pia imechukuliwa na mabepari wa kigeni na wenyeji kutengeneza mahitaji yasio lazima kwa umma wa kimataifa kwa kusambaza hofu ili kuuza bidhaa mbalimbali.
Kutokana na hivyo mpango ili nchi kununua bidhaa zao umefungamanishwa na wateja kukopeshwa fedha na mabenki ndio maana benki ya dunia tangu awali ikatenga fedha za kukopesha kwa faida wakiita ni msaada.
Mwendazake Magufuli alijua hila za nchi za mabepari kuendelea kufukarisha nchi zetu ndio maana akawa makini na mwangalifu ili tusiharibiwe au kuhujumiwa maendeleo na ujenzi wa uchumi wetu.
Yafaa Rais Samia awe mwangalifu kurukia mikopo tunayobembelezewa na benki ya dunia. Tukope tu kwa yale yenye manufaa tuliyopanga wenyewe.