Serikali ijikite kukusanya kodi, iachane na mikopo ya kubembelezewa na Benki ya Dunia kuhusu COVID 19

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,371
7,141
Lazima kutambua wakati wote benki ya dunia ni benki tu kama zingine kipaumbele chake ni faida. Wenye hisa wakubwa ni marekani na nchi za ulaya. Kwa mfumo wa kibepari wafaidika namba moja na benki ya dunia ni mabepari wakubwa wa nchi hizo.

Kutokana na hivyo nchi changa sio rahisi kupata maendeleo kwa kukopa benki ya dunia kwa vile benki hiyo inataka iwapangie wakope kwa miradi yenye maslahi na nchi kubwa za kibepari na sio kuwaletea wananchi maendeleo.

Kuna kila dalili ugonjwa wa covid 19 umeundwa kama fursa kubwa kwa mabepari wa madawa ya binadamu marekani na ulaya kutengeneza fedha.

Fursa pia imechukuliwa na mabepari wa kigeni na wenyeji kutengeneza mahitaji yasio lazima kwa umma wa kimataifa kwa kusambaza hofu ili kuuza bidhaa mbalimbali.

Kutokana na hivyo mpango ili nchi kununua bidhaa zao umefungamanishwa na wateja kukopeshwa fedha na mabenki ndio maana benki ya dunia tangu awali ikatenga fedha za kukopesha kwa faida wakiita ni msaada.

Mwendazake Magufuli alijua hila za nchi za mabepari kuendelea kufukarisha nchi zetu ndio maana akawa makini na mwangalifu ili tusiharibiwe au kuhujumiwa maendeleo na ujenzi wa uchumi wetu.

Yafaa Rais Samia awe mwangalifu kurukia mikopo tunayobembelezewa na benki ya dunia. Tukope tu kwa yale yenye manufaa tuliyopanga wenyewe.
 
Raia hatuna pesa ngoja akope ziongeze mzunguka ndio akusanye kodi, hatushi reli, bwawa, wala busisi, napita tu na cheko la upako wa asubuhi
 
Lazima kutambua wakati wote benki ya dunia ni benki tu kama zingine kipaumbele chake ni faida. Wenye hisa wakubwa ni marekani na nchi za ulaya. Kwa mfumo wa kibepari wafaidika namba moja na benki ya dunia ni mabepari wakubwa wa nchi hizo
Hii nchi ni masikini tu ,tena masikini wa kutupwa wanaoshindia mlo mmoja ..

Kukomaa na kodi wakati wabunge hawatoi kodi ni kunyanyasa sisi masikini bila sababu ....

Mama samia kopa ,kopa hasa ,leta wawekezaji maisha ni magumu sana ...

Achana na hao manyang'ao wanaosema nchi ni tajiri ..
 
Tatizo muda hausimami hivyo inabidi akope atatue changamoto zilizoachwa na muda alafu akusanye kodi kwa kutatua changamoto za muda huu.
 
Ukisikia CCM wanakwambia fedha za ndani , ujue huko nje washaharibu, sasa wanakuja kuumiza wananchi
 
Mama samia kopa ,kopa hasa ,leta wawekezaji maisha ni magumu sana ...

Achana na hao manyang'ao wanaosema nchi ni tajiri ..
Atusaidie basi ili wote wanaostahili kulipa kodi wakiwemo wabunge na yeye mwenyew walipe kodi.
 
Lazima kutambua wakati wote benki ya dunia ni benki tu kama zingine kipaumbele chake ni faida. Wenye hisa wakubwa ni marekani na nchi za ulaya. Kwa mfumo wa kibepari wafaidika namba moja na benki ya dunia ni mabepari wakubwa wa nchi hizo...
Wanao shangiliaga serikali ikomae na kodi, wengi ni wala kodi, siyo walipa kodi! Labda Wewe ni mbunge unataka sisi tukamuliwe, Wewe ule kwa urahisi!
 
Lazima kutambua wakati wote benki ya dunia ni benki tu kama zingine kipaumbele chake ni faida. Wenye hisa wakubwa ni marekani na nchi za ulaya. Kwa mfumo wa kibepari wafaidika namba moja na benki ya dunia ni mabepari wakubwa wa nchi hizo.

Kutokana na hivyo nchi changa sio rahisi kupata maendeleo kwa kukopa benki ya dunia kwa vile benki hiyo inataka iwapangie wakope kwa miradi yenye maslahi na nchi kubwa za kibepari na sio kuwaletea wananchi maendeleo.

Kuna kila dalili ugonjwa wa covid 19 umeundwa kama fulsa kubwa kwa mabepari wa madawa ya binadamu marekani na ulaya kutengeneza fedha.

Fulsa pia imechukuliwa na mabepari wa kigeni na wenyeji kutengeneza mahitaji yasio lazima kwa umma wa kimataifa kwa kusambaza hofu ili kuuza bidhaa mbalimbali.

Kutokana na hivyo mpango ili nchi kununua bidhaa zao umefungamanishwa na wateja kukopeshwa fedha na mabenki ndio maana benki ya dunia tangu awali ikatenga fedha za kukopesha kwa faida wakiita ni msaada.

Mwendazake Magufuli alijua hila za nchi za mabepari kuendelea kufukarisha nchi zetu ndio maana akawa makini na mwangalifu ili tusiharibiwe au kuhujumiwa maendeleo na ujenzi wa uchumi wetu.

Yafaa Rais Samia awe mwangalifu kurukia mikopo tunayobembelezewa na benki ya dunia. Tukope tu kwa yale yenye manufaa tuliyopanga wenyewe.

Heee!

"Mwendazake Magufuli alijua hila za nchi za mabepari kuendelea kufukarisha nchi zetu ndio maana akawa makini na mwangalifu ili tusiharibiwe au kuhujumiwa maendeleo na ujenzi wa uchumi wetu."

Akaja na kodi na tozo za dhuluma na kisha akatuachia deni kiasi gani?

Mama akomae na uwajibikaji. Wote wenye kulipa kodi wakiwamo wabunge walipe kodi stahiki.

Mikopo ya benki haiepukiki katika jitihada yoyote ya maendeleo pale inapotumika vizuri. Si katika miradi ya kupendezesha majiji.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom