SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 6,221
- 9,940
Naamini nimewahi kuleta walau uzi mmoja kuhusiana na mada ya Utalii wa Michezo, ila leo nitakuja na angle tofauti kidogo kutokana na kile ambacho nimekishuhudia siku za hivi karibuni.
Bila kueleza mengi na kuzungukazunguka, kiufupi Utalii wa Michezo au Sports Tourism unahusiana na kuandaa matukio ya kimichezo inayoweza kuvutia watu wasafiri kutoka miji au nchi tofauti kuja kuhudhuria au walipie kuyaona katika TV. Hapa tunaongelea mifano kama Kombe la Dunia, AFCON, Olympics, nk. na hata mashindano ya ndani ya nchi kama yamenadiwa ipasavyo.
Siku za hivi karibuni nimesikia watu wanahusisha kwenda mbuga za wanyama kama sehemu ya sports tourism, hili siyo kweli na siyo sahihi hata kama walioenda huko wanajihusisha na michezo. Ukienda mbuga ya wanyama unapromoti aina tofauti ya utalii, hili ni muhimu tulielewe ili tujua kama tunasonga mbele au tumegota sehemu moja.
Uwanja wa Mkapa umekaa zaidi ya miaka 20 toka umejengwa kama sikosei ila sina uhakika kama uliwahi kuandaa mashindano yoyote ya riadha ya kimataifa hadi zile running tracks zimeozeana inabidi gharama kubwa iingiwe kuzibadilisha huku zikiwa hazijawahi kuingiza hata senti.
Tuna milima kibao nchi nzima ila sijawahi kusikia tumeandaa mashindano yoyote ya kimataifa ya mbio za baiskeli au pikipiki ya kwenye maeneo magumu (rough terrain). Hii ni baadhi tu ya maeneo tunayoweza kukuza utalii wa michezo na naweza kutoa mifano mingi ya fursa zilizopo.
Nikihitajika napatikana kwa ushairi zaidi.
Mada nyingine inayohusiana na hii niliyowahi kuandika:
- Tunajengaje "Utalii wa Michezo" kwa kupiga marufuku na kutishia mashabiki wasisapoti timu fulani?