Serikali ijifunze kwa hali ya Uchumi - Venezuela

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,372
6,074
Baada ya aliyekuwa kiongozi wa Venezuela Hayati Hugo Chaves kuchukua njia zote za kiuchumi na Serikali kuamua kufanya biashara kama kuuza mafuta na makampuni ya ujenzi kufanywa na Serikali uchumi wa nchi hiyo mbali na kuwa na utajiri mkubwa wa mafuta umeanguka kabisa

Hapa Tanzania ni dalili wazi tunafuata njia hiyo hiyo ya Venezuela kwani kwa mara ya Kwanza kwa kipindi cha miaka 30 hatujawahi kuona foleni au uhaba wa mafuta hapa nchini lakini kwasasa tunaanza kuona ukosefu wa mafuta ya diesel na petrol ukijitokeza sehemu mbali mbali hapa nchini.

Tayari sekta ya Ujenzi hapa nchini imeathirika kwa sehemu kubwa baada ya sehemu ya kazi kufanyika na serikali kupitia JKT Suma.

Huko kanda ya ziwa tumesikia Meli ya Mv Victoria ikianza kazi kwa kutoa ofa ya kusafirisha mizigo bure je hao wasafirishaji wenye magariwatalipaje kodi kama kazi zao zitakwama.

Serikali iangalie sekta binafsi kwa makini kuanguka kwa Sekta Binafsi ni anguko la kiuchumi.
 
Duh! Sasa Tz na Venezuela vinarelate vipi rafiki? Kwan uchumi wa Tz unategemea oil kama wa Venezuela? Nchi ambayo unaweza kulinganisha na Venezuela Africa ni Angola.Nao uchumi wao umeyumba sababu ya oil price.

Hiyo hoja yako ya pili kuhusu MV.Victoria sijaielewa kabisa!
 
Ujamaa na ubepari ni mifumo ya kiuchumi na kiutawala yenye faida na hasara. Athari za mifumo hii ni kama ifuatavyo.

Ujamaa unatengeneza taifa la watu waoga, legelege, wavivu wa kufikiri n.k, hapa ndio Venezuela wapo na sisi kwa kiasi.

Ubepari unatengeneza raia wakaidi, watukutu, wenye uhuru uliopita mipaka n.k. Hii ndio kesi ya ulaya na marekani, maandamano ya hivi karibuni ni moja ya ushahidi wa hili hadi wengine kuacha lengo kuu la maandamano na kufanya uhalifu.

Mifumo hii ikitekelezwa na kuunganishwa pamoja inaleta uwiano chanya kiuchumi na kijamii kwa kiasi. Mfano hai ni China.
 
Ninamaanisha ikiwa Venezuela na utajiri mkubwa wa mafuta imefilisika kwa Sera mbovu za kiuchumi (socialism) je sisi hapa Tanzania itakuwaje.
Kuhusu Mv Victoria ni kwamba serikali imetangaza itasafirisha mizigo kutoka Mwanza mpaka Bukoba je hao wasafirishaji walipa Kodi watafanya kazi gani.
 
Acha longo longo USA ndio wameharibu uchumi wa Venezuala kwa vikwazo lukuki na kuwafanya watengwe na dunia baada ya kuona vikwazo havimtoi madarakani wakaamua kumuua.

R.I.P El Commandante Hugo Chavez
 
Ujamaa na ubepari ni mifumo ya kiuchumi na kiutawala yenye faida na hasara. Athari za mifumo hii ni kama ifuatavyo.

Ujamaa unatengeneza taifa la watu waoga, legelege, wavivu wa kufikiri n.k, hapa ndio Venezuela wapo na sisi kwa kiasi.

Ubepari unatengeneza raia wakaidi, watukutu, wenye uhuru uliopita mipaka n.k. Hii ndio kesi ya ulaya na marekani, maandamano ya hivi karibuni ni moja ya ushahidi wa hili hadi wengine kuacha lengo kuu la maandamano na kufanya uhalifu.

Mifumo hii ikitekelezwa na kuunganishwa pamoja inaleta uwiano chanya kiuchumi na kijamii kwa kiasi. Mfano hai ni China.
Magufuli anaongoza serikali ya kijamaa na kujitegemea mbona amewafanya watanzania wasiwe WAVIVU WA KUFIKIRI,LEGELEGE NA DHAIFU km ulivyosema.

Ujamaa anaoufuata mh.magufuli NDIYO ujamaa Bora ZAIDI kuliko yaliyomo ndani ya mabuku yanayoelezea asili ya ujamaa. Magufuli anahimiza HAPA KAZI TU...
 
nadhani awamu ya pili ya magufuli kama atachaguliwa uchumi utakuwa wa vuta nikuvute hasa kwa makapuku wa fikra na makapuku wa fedha.
Rais Magufuli alishawaambia makapuku wa fikra kuwa WANAISHI ZAIDI YA MALAIKA KWA KUIKWIBA NCHI kwa kigezo Cha kukosekana SERIKALI YENYE KUZINGATIA MIIKO YA KULINDA WANANCHI,Sasa wajue wataishi vibaya ZAIDI ya SHETANI.
 
Duh! Sasa Tz na Venezuela vinarelate vipi rafiki? Kwan uchumi wa Tz unategemea oil kama wa Venezuela? Nchi ambayo unaweza kulinganisha na Venezuela Africa ni Angola.Nao uchumi wao umeyumba sababu ya oil price.
Hiyo hoja yako ya pili kuhusu MV.Victoria sijaielewa kabisa!
Zombie wa kijani umeelewa kilichopo?
 
Ninamaanisha ikiwa Venezuela na utajiri mkubwa wa mafuta imefilisika kwa Sera mbovu za kiuchumi (socialism) je sisi hapa Tanzania itakuwaje.
Kuhusu Mv Victoria ni kwamba serikali imetangaza itasafirisha mizigo kutoka Mwanza mpaka Bukoba je hao wasafirishaji walipa Kodi watafanya kazi gani.
Unasema socialism Ina sera mbovu ilihali katiba ya nchi yetu inachukua KIDOGO ya mfumo huo na kuufinyanga kuwa wa UJAMAA WA KIAFRIKA,NDIYO huu ujamaa na kujitegemea.

Swali langu kwako, je unapendekeza mfumo gani tuwe nao ZAIDI ya huu wetu wa UJAMAA NA KUJITEGEMEA..
 
Ninamaanisha ikiwa Venezuela na utajiri mkubwa wa mafuta imefilisika kwa Sera mbovu za kiuchumi (socialism) je sisi hapa Tanzania itakuwaje.
Kuhusu Mv Victoria ni kwamba serikali imetangaza itasafirisha mizigo kutoka Mwanza mpaka Bukoba je hao wasafirishaji walipa Kodi watafanya kazi gani.
Mtoa hoja hebu enenda vizuri ili watu tuchangie kwa kujua kuwa wewe mwenyewe UNAO UPEO MKUBWA JUU YA MASUALA YA VENEZUELA....
 
Kiongozi tuliyenaye hajali uchumi, anajitahidi kusaka kura za wenye uelewa finyu.

NI miaka michache iliyopita WAPIGAJI WA NCHI wakatengeneza skandali ya kupata fedha kwa sababu ya kutokuwa na UMEME WA KUTOSHA.
1.IPTL-ESCROW
2.Dowans
3.Richmond

MAGUFULI ANAJENGA MIUNDO MBINU YA UMEME WA UHAKIKA ILI UZIDI KUSISIMUA UCHUMI...wewe unadai HAJALI uchumi ha ha ha muwe mnakunywa maziwa baada ya kupata TATU MZUKA...
Karibu hapa mchupa mkubwa wa FARU JOHN hatimiliki ya mh.mwenyekiti😂😂
 
Hii Serikali yako ya sasa unadhani ni Sikivu Ndugu?
Serikali sikivu iliyoujenga UKUTA mbuguni mererani wilayani simanjiro ili kudhibiti wizi wa raslimali ZETU na kumfanya mzee LAISER awe bilionea kwa ule mzigo wa kilo 14 kwa ujumla.
 
Matatizo ya Venezuela na Iran yanasababishwa na nchi ya marekani kwa kuziwekea vikwazo vya kibabe nchi hizo.

Na so hizo tu bali hata Korea kaskazini ni same story.

Kuhusu MV victoria na impact ya uchumi ndio umejikoroga binafsi...
Unaweza kuniambia kwanini baadhi ya sehemu hapa Tanzania kuna uhaba wa mafuta ya diesel na petrol. Je hi ni hujuma dhidi ya serikali kuelekea uchaguzi mkuu ama ni sera mbovu ya uchumi.

Kuhusu Rais Magufuli kuchaguliwa kwa awamu ya pili hilo halina pingamizi kwani ni kiongozi pekee ndani ya CCM aliyeweza kuonyesha watanzania uwezo mkubwa tangu chama hicho kiasisiwe 1977.
 
NI miaka michache iliyopita WAPIGAJI WA NCHI wakatengeneza skandali ya kupata fedha kwa sababu ya kutokuwa na UMEME WA KUTOSHA.
1.IPTL-ESCROW
2.Dowans
3.Richmond

MAGUFULI ANAJENGA MIUNDO MBINU YA UMEME WA UHAKIKA ILI UZIDI KUSISIMUA UCHUMI...wewe unadai HAJALI uchumi ha ha ha muwe mnakunywa maziwa baada ya kupata TATU MZUKA...
Karibu hapa mchupa mkubwa wa FARU JOHN hatimiliki ya mh.mwenyekiti😂😂

Toa hizo herufi kubwa ndani ya sentensi zako, ili uje nikupe dozi sahihi.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom