Serikali ijiandae kukosa mapato

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,862
2,871
Habari za asubuhi wana jamvi!

Nimekuwa nikijiuliza hivi hawa wamachinga wanaotembeza vitu mitaani huwa hivi vitu wanavipata wapi na kwa mtaji gani? Maana unaweza kukutana na machinga ana vifaa vya thamani kubwa sana mikononi lakini ukiangalia hali yake kwa jicho la tatu utagundua huyu jamaa hivi vitu siyo vyake.

Baada ya kujiuza swali hilo niliamua kwenda kariakoo ambako kuna jamaa zangu wengi sana wanauza waduka ya nguo na vyombo vya nyumbani. Niliwauliza hivi hawa wamachinga wanapata hivi vitu wapi?. Walinipa majibu niliyokuwa nafikiri kwenye kichwa changu kwa sehemu kubwa.

1. Wapo wamachinga wa kweli kabisa waliotafuta mtaji kidogo ili kujitafutia riziki kwa kutembeza hayo wanayoyauza.

2. Wapo wamachinga wa kutengenezwa na wenye maduka makubwa, wanadai kuwa wanapunguza mzigo wa kodi kwa kutengeneza machinga kadhaa anaowapa mzigo kwenda kuuza kisha yeye anawalipa kiasi walichokubaliana.

Vijana hao wanadai kwenye duka lao wana machinga kadhaa ambao wanapewa mizigo kwenda kuuza, vijana hawa hutakiwa kupeleka pesa na mizigo iliyobaki. Hawa vijana hupeleka vitambulisho kutoka serikali ya mtaa , barua na picha ya mdahamini ili wapewe kazi ya kutembeza mzigo.

SERIKALI ITAPOTEZAJE KODI
1. Ni dhahiri kwamba machinga halipi kodi, kwa hiyo kitendo cha machinga kuruhusiwa kufanya biashara kwenye strategic areas za mji kutawavutia wengi sana. Wafanyabiashara watatumia fursa hiyo kuongeza idadi ya machinga wao sokoni. Kwa hali hiyo huyu mfanya baishara atabaki na kodi ya bidhaa anazouza dukani, lakini ile duka inayotembea hatalipa kodi. Kwa msingi huo makusanyo yatashuka.

2. Wale wafanyabiashara wasio na uwezo wa kuanzisha haya maduka yanayotembea watakosa wateja na hivyo kuwapelekea wao ama kupunguza mauzo yao au kufunga kabisa biashara na matokeo yake ni kushuka kwa kodi.

3.Matumizi ya magari binafsi hasa kwa miji yenye barabara finyu kama mwanza utapungua kwa kiasi kikubwa sana kutokana na wingi wa watu na kupanga mizgo kiholela barabarani. Wauza mafuta hawatauza kama zamani na hata lile pato linalopatikana kutokana na makosa barabarani litapungua.

4. Ilisemekana serikali inapoteza millions of shillings kwa uwepo wa foleni dsm na kwenye miji mingine, Kama ni kweli hali hiyo itarudi kwa kasi hasa kwenye miji mikubwa kama Mwanza dsm n.k.

FURSA KWA VIJANA
Sisi vijana tunapaswa kutumia fursa hii kuanzisha maduka yetu yanayotembea badala ya kulalamika. Ukweli ni kwamba kama utaamua kumchukua dogo huko kwenu ukamfundisha mitaa ya Dsm , Mwanza , Arusha , Mbeya nk then umpe nguo za kike au za kiume, ama vyombo vya nyumbani walau vya laki 2 mwisho wa mwezi utapiga hela ya maana tu issue hapa ni kuwa nao 5 hivi na kuwamanage vizuri. Tuwe wepesi kuchangamkia hizi fursa adimu japo zina athari kwa nchi.
 
Back
Top Bottom