Serikali ijayo itafuata " kikamilifu" itikadi ya Ujamaa na Kujitegemezi. Je, CCM kuna vijana wazalendo wa kumsaidia Rais Magufuli?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,914
141,863
Maandalizi yote ya kuirejea itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea kivitendo kama ilivyokuwa enzi za Mwalimu Nyerere yamekamilika.

Kwa sasa tuna ATCL ni yetu 100&, tunamiliki TTCL 100%, Tanesco 100%, Mamlaka za maji 100%, TRC 100%.

Tunakwenda kuwa na benki yetu ya biashara kubwa mbadala wa NBC, TPDC inakwenda kufungua vituo vya mafuta kila wilaya, SUMA JKT imeanzisha viwanda vya kutosha vya bidhaa mbalimbali na ndio mkandarasi mkuu wa ujenzi.
Haya ni kwa uchache.

Ni wazi Rais Magufuli amefanya kazi kubwa na ya kizalendo kutufikisha hapa tulipo na niwazi serikali ijayo itakuwa ya vitendo zaidi na zaidi ili haya yaliyoanzishwa yakawe msaada mkuu kwa wananchi wa kawaida.

Je, CCM imeshaandaa vijana wazalendo wa kutekeleza sera zake kupitia itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea?

Ijumaa Kareem.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kama nyerere aliyekaa miaka 21 ikulu wakati watu hawajaonja kama Leo utamu wa ubepari mwisho akashindwa sembuse magufuli?

Magu anafuta sifa aonekane anamuenzi nyerere ila ulimwengu huu na ujamaaa 100% ni ndoto ya mchana

Ulimwengu huu lazima ufikiri sana so kama mambo yanavyokwenda hapa kwetu

Ninachoona ni maandalizi ya kumbakiza madarakani miaka mingine kumi kwa kisingizio cha miradi hilo nitakuelewa
 
Unasapoti serikali kufanya biashara yani serikali ijimilikishe njia zote za uchumi wa nchi wakati sekta binafsi ndio inayotoa ajira kwa wengi zaidi, matokeo yake ukosefu wa ajira utaongezeka na maisha yatazidi kuwa magumu kwa mtanzania wa kawaida.

Hiyo serikali yako ndio itakuwa tajiri.
 
Kuhusu ajira tayar kafeli Vijana wengi wako kitaa hawana ajira kila Sikh ni kupiga maneni
 
Unasapoti serikali kufanya biashara yani serikali ijimilikishe njia zote za uchumi wa nchi wakati sekta binafsi ndio inayotoa ajira kwa wengi zaidi, matokeo yake ukosefu wa ajira utaongezeka na maisha yatazidi kuwa magumu kwa mtanzania wa kawaida.

Hiyo serikali yako ndio itakuwa tajiri.
Nyerere aliweza lakini...... Sema vita ya Kagera ndio ikaleta sintofahamu!
 
ujamaa aina ya utawala wa kuacha wananchi wote wamkabidhi mtu mmoja akili na ufikiri ndiyo uzalendo au utumwa wa fikra?
 
Back
Top Bottom