Serikali iingilie kati Wizi unaofanyika kwenye Kumbi za Sherehe. Ni Wizi Mkubwa sana.....

Tatizo wabongo mnapenda sana sherehe na kujionyesha. Fedha mnapata kwa taabu sana ila ukiibahatisha unasahau taabu za jana unajifanya mfalme na matumizi ya hovyo kama masherehe ili ujichukulie maujiko. Acha wenye maukumbi wawapige na vitu vizito utosini
 
Unaonaje ukaenda kwenye kumbi zisizo na hayo masharti?
Hizi bei na kulazimisha ukichukua Ukumbi wao lazima utumie chakula,vinywaji na mapambo yao.

Huu ni wizi. Bei wanazoweka kwa mambo hayo ni kubwa sana kwa makusudi kwa kujua huna namna isipokuwa kufuata wanachotaka. Wanatengeneza faida kubwa sana kiwizi.

Huu ni Ukumbi mmoja upo Tabata nmekutana nao wakati nikitafuta Ukumbi kwa ajili ya sherehe ya ndoa.

View attachment 2026073
 
Yaani regulations za time unataka kufananisha na price capping na procurement ya vitu vyako vya harusi ? Seriously serikali iweke masharti utavyompata mc, mziki, upambaji na vyakula na magari plus picha..nchi ngumu hii kwa kweli
Bado hujamwelewa mleta mada. Kinacho-control price ya goods or services ni demand and supply na still kuna baadhi ya bidhaa au huduma bado pia demand na supply haitumiki na serikali tu ndiyo ita-fix prices ya hivyo vitu, mfano mafuta, maji, umeme etc. Mleta mada ameelezea kwa ufasaha kabisa kuhusu wenye kumbi kumlazimisha mteja kukodi hall na huduma nyingine ambazo siyo lazima nihudumiwe na hizo halls. Iweje umlazimishe mteja kupata huduma nyingine apart from your hall? Ilihali anao uwezo wa kuzipata huduma nyingine tena zilizo bora at reasonable cost?
 
Kaeleweka toka mwanzo hoja yake ni rahisi mno. Ndio umejibiwa kuwa ni matakwa na utashi wa vendor anauza huduma ya ukumbi wake kwa package..sasa kama hukubaliani nae tumia uhuru wa soko kwenda kwa vendors wengine.
 
Regulations bado zipo sehemu nyingi ila hazihitajiki na zaidi zinakwamisha biashara.
Ni ushamba tu.
Don't miss the point bwashee, regulations zipo as long as serikali itaona kuna ulazima. Ndiyo maana kuna kipengele hapo kimeandikwa "muda wa kufanya sherehe ni saa 6:00 usiku kwa mujibu wa sheria za Halmashauri za miji". Kama serikali haihusiki mbona Halmashauri/Municipal zimeweka hizo sheria?
 
Regulations zipo kwenye mazingira/usafi na usalama wa ukumbi. Bei kila mtu apange atakavyoona inafaa, ukiona huwezi tafuta ukumbi mwingine au fanyia sherehe nyumbani kwako.Kwenye soko huria nguvu za soko"market forces" ndizo zinaamua bei.
Lazima ziwe regulated watoe huduma kulingana na thamani ya huduma wanazotoa. Yani mtu utoe huduma kulingana na gharama, haiwezekani vitu viwe vulululu vulululu tu
 
Fursana ya 500 inauzwa 1500?

Anyways, sahizi watu wenye resources wanajifanyia wnanachotaka, as if hakuna regulator
 
Bado hujamwelewa mleta mada. Kinacho-control price ya goods or services ni demand and supply na still kuna baadhi ya bidhaa au huduma bado pia demand na supply haitumiki na serikali tu ndiyo ita-fix prices ya hivyo vitu, mfano mafuta, maji, umeme etc. Mleta mada ameelezea kwa ufasaha kabisa kuhusu wenye kumbi kumlazimisha mteja kukodi hall na huduma nyingine ambazo siyo lazima nihudumiwe na hizo halls. Iweje umlazimishe mteja kupata huduma nyingine apart from your hall? Ilihali anao uwezo wa kuzipata huduma nyingine tena zilizo bora at reasonable cost?
Mbaya zaidi unakuta hizo kumbi hawajulikani kwenye mamlaka za kodi kama wanafanya biashara ya kuuza vinywaji
 
Regulations zipo kwenye mazingira/usafi na usalama wa ukumbi. Bei kila mtu apange atakavyoona inafaa, ukiona huwezi tafuta ukumbi mwingine au fanyia sherehe nyumbani kwako.Kwenye soko huria nguvu za soko"market forces" ndizo zinaamua bei.
Its simple, mbona mitandao ya simu ikipandisha hamsemi mtu achague mtandao anaoona ni nafuu kwake?

Biashara lazima ziwe regulated ili watu wasitumie monopoly vibaya
 
Hizi bei na kulazimisha ukichukua Ukumbi wao lazima utumie chakula,vinywaji na mapambo yao.

Huu ni wizi. Bei wanazoweka kwa mambo hayo ni kubwa sana kwa makusudi kwa kujua huna namna isipokuwa kufuata wanachotaka. Wanatengeneza faida kubwa sana kiwizi.

Huu ni Ukumbi mmoja upo Tabata nmekutana nao wakati nikitafuta Ukumbi kwa ajili ya sherehe ya ndoa.

View attachment 2026073

Mkuu, nenda Johari Rotana au Hyatt Regency bei zao ni nafuu mno mno
 
Huelewei maana ya monopoly.
Biashara kuwa regulated ni tofauti sana na kupanga bei. Biashara inakuwa regulated kwenye masuala ya usafi, usalama, umri(kwa pombe na sigara), ufungashaji n.k ila sio kupanga bei za bidhaa au huduma tena ambazo serikali haina mkono wake kabisa.
Its simple, mbona mitandao ya simu ikipandisha hamsemi mtu achague mtandao anaoona ni nafuu kwake?

Biashara lazima ziwe regulated ili watu wasitumie monopoly vibaya
 
Baadhi ya mitandao inatumia mkongo wa mawasiliano wa serikali, Serikali ina hisa Airtel ndio maana bado inaingilia katika kupanga bei za mitandao. Siku mitandao ikija kujitegemea na ikawa ya binafsi kwa asilimia 100 serikali itabidi iache huo mfumo wa kuipangia bei.

Pia watu wengi hawaelewi madhara ya kupenda kuiingiza serikali kila mara katika kuamua namna biashara zinafanyika na kupanga bei za bidhaa au huduma.
Its simple, mbona mitandao ya simu ikipandisha hamsemi mtu achague mtandao anaoona ni nafuu kwake?

Biashara lazima ziwe regulated ili watu wasitumie monopoly vibaya
 
Harusi ni sherehe,
Sherehe ni STAREHE.

SERIKALI haiwezi kuingilia Sherehe au STAREHE za watu.

Serikali inaweza ingalia ndoa lakini sio harusi.

Serikali haipangagi masuala ya ANASA au STAREHE za watu wake.

Ndio maana huwezi sikia serikali ikiingilia bei ya pombe au sigara Kwa maana ni STAREHE hizo ambazo mtu anaweza kuifanya au asifanye.

Ila serikali inaweza ingilia vitu basic na lazima Kama vile maji, Mafuta, umeme, vocha(bando) Kwa maana hizo ni muhimu na basic.

Kuiingiza serikali kwenye STAREHE zako ni ukosefu wa Akili.

Ni Sawa na masuala ya Hoteli, au Lodge, au Guesthouse,

Au masuala ya kwenda Disco au kuangalia Wasanii.

Msanii anauwezo WA kukuambia kiingilio milioni moja l. Sasa wewe utajipima Kama unauwezo huo au laa, pia utaangalia huyo msanii anatoa Huduma ya viwango hivyo au ni geresha tuu.

Usitake kila kitu serikali ikufanyie hasa mambo ya ANASA.

Harusi sio lazima.
Ndoa ndio lazima.
 
Serikali inaweza kuingilia na huwa inaingilia wakati mwingine ila haipaswi kuingilia isipokuwa kwa njia kama ya kodi.
Harusi ni sherehe,
Sherehe ni STAREHE.

SERIKALI haiwezi kuingilia Sherehe au STAREHE za watu.

Serikali inaweza ingalia ndoa lakini sio harusi.

Serikali haipangagi masuala ya ANASA au STAREHE za watu wake.

Ndio maana huwezi sikia serikali ikiingilia bei ya pombe au sigara Kwa maana ni STAREHE hizo ambazo mtu anaweza kuifanya au asifanye.

Ila serikali inaweza ingilia vitu basic na lazima Kama vile maji, Mafuta, umeme, vocha(bando) Kwa maana hizo ni muhimu na basic.

Kuiingiza serikali kwenye STAREHE zako ni ukosefu wa Akili.

Ni Sawa na masuala ya Hoteli, au Lodge, au Guesthouse,

Au masuala ya kwenda Disco au kuangalia Wasanii.

Msanii anauwezo WA kukuambia kiingilio milioni moja l. Sasa wewe utajipima Kama unauwezo huo au laa, pia utaangalia huyo msanii anatoa Huduma ya viwango hivyo au ni geresha tuu.

Usitake kila kitu serikali ikufanyie hasa mambo ya ANASA.

Harusi sio lazima.
Ndoa ndio lazima.
 
Mbona Msibani Tukitoka Msikitini au Kanisani Mambo Yanaishia Nyumbani Vizuri Tu Na Hakuna Lawama,Tujikune Mkono Unapofikia,Ukiona Huwezi Afford Hizo Bei,Funga Turubai Hapo Nyumbani Kwako.
 
Hizi bei na kulazimisha ukichukua Ukumbi wao lazima utumie chakula,vinywaji na mapambo yao.

Huu ni wizi. Bei wanazoweka kwa mambo hayo ni kubwa sana kwa makusudi kwa kujua huna namna isipokuwa kufuata wanachotaka. Wanatengeneza faida kubwa sana kiwizi.

Huu ni Ukumbi mmoja upo Tabata nmekutana nao wakati nikitafuta Ukumbi kwa ajili ya sherehe ya ndoa.

View attachment 2026073

Umelazimishwa kufanya sherehe? Je ni matumizi muhimu au kupenda anasa na kujionyesha ndo kunawagharimu hivyo?

Hakuna cha serikali kuingilia kati. Kama huna hela acha tamaa. Nenda ukafunge ndoa na sherehe andaa kwenu kwa gharama unayoimudu.
 
Back
Top Bottom