Serikali iingilie Kati Wamiliki wa Shule binafsi wameamua kuwa wababe

kanyembwe

Member
Apr 17, 2017
94
222
Niliona clip moja Waziri wa Elimu akishauri Wamiliki wa Shule Na Wazazi waridhiane issue ya malipo ya ada, ni ushauri nzuri, lakini nimefuatilia magroup yalioanzishwa Na Shule mbalimbali wazazi wakiomba kupunguziwa ada kidogo,has a kutoa gharama za Chakula ambacho wanafunzi hawakula wakati wa likizo ya Corona, Wamiliki hao wamegoma kupunguza ada hiyo Na wamekuwa wakali jambo linaloashiria kuwafuatilia wanafunzi ambao wazazi wao walikuwa mstari wa mbele kudai punguzo ya ada,Kimsingi nafkiri in wakati muafaka serikali itoe tamko kuwaokoa wazazi ili maisha yaendelee kama ilivyokuwa awsli, Mungu ibariki Tanzania
 
mkuu lipa ada acha kuisikiliza serikali itakupoteza, haiwezi kuishinda hili suala
 
Ila wabongo uelewa wetu una mushkeri,

Hivi unaombaje upunguziwe ada wakati huo huo mwanao anaenda kufundishwa contents na competences zote alizotakiwa kufundisha katika mwaka wa kawaida wa masomo.

Unaposema upunguziwe ada kwa lugha nyingine unamaanisha mwanao apunguziwe masomo ya kufundishwa.

Think critically.
 
Swala hili haliwekani.Fanya namna ulipe ada au uombe kuongezewa muda wa malipo ili watoto wasirudishwe.Kwa kifupi tuko meli moja bro
 
Huu ni ubinafsi uliotukuka, hizo ndizo gharama za kuamua kumpeleka mtoto shule ya Private ukaacha government. Hivi unadhani wapishi waliacha kupokea mshahara kwa vile mwanao alikuwa likizo ya corona? Ungelalamika kama wameongeza karo, ningekuelewa. Karo ni mkataba wa mwaka na ilikuwa ni msamaha wa kuruhusu ulipe kwa mafungu. By the way mie ni mkulima lakini mwanangu wa mwisho yupo form two hapa Dar shule ya Private
 
Ila wabongo uelewa wetu una mushkeri,

Hivi unaombaje upunguziwe ada wakati huo huo mwanao anaenda kufundishwa contents na competences zote alizotakiwa kufundisha katika mwaka wa kawaida wa masomo.

Unaposema upunguziwe ada kwa lugha nyingine unamaanisha mwanao apunguziwe masomo ya kufundishwa.

Think critically.
Tatizo la watu kutafuta kiki wakati hawana hela. Ukiamua kula nguruwe tafuta mnono
 
Mzazi kama huna uwezo wa kumsomesha mtoto private muache asome shule za serikali, kama janga hili linaleta mgongano ukiwa na uzima je ulitafakari kuwa ikitokea nimeondoka mwanangu atakua na uhakika wa kuendelea kupata hii elimu kwa kiwango cha shule ninayompeleka?
 
Lea hiyo

Kwa hiyo ndio upore pesa wazazi wakati chakula watoto hawakula Wala kulala mabwenini kwa miezi mitatu huo wizi

Miezi hiyo hawakuoga maji hivyo sehemu ya bili maji inatakiwa kuondoka nk
 
Hakuna namna mkuu tulipe tu ada, mm nachokifurahia ni mabadliko ya uelewa Wa mtoto wangu suala la ada ntalipa hata Kwa kukopa Kwa liba.
 
Tuambie kwanini unasema serikali iokoe wazazi, kwako ni wazazi tu ndo wanastahili kuokolewa.?
 
Ila wabongo uelewa wetu una mushkeri,

Hivi unaombaje upunguziwe ada wakati huo huo mwanao anaenda kufundishwa contents na competences zote alizotakiwa kufundisha katika mwaka wa kawaida wa masomo.

Unaposema upunguziwe ada kwa lugha nyingine unamaanisha mwanao apunguziwe masomo ya kufundishwa.

Think critically.
Mkuu vipi kuhusu kulipia usafiri ambao hajawahi kutumia kwa miezi 3? Ada sawa atafidia masomo lkn pia kuna lower classes ambazo wao muda wao ni uleule.
 
Shule za Serikali ziko za kutosha; kama huna uwezo wa kulipa ada huko kwenye mashule binafsi basi wapeleke watoto kule ambako kodi yako inatumika. Shule za binafsi hawapati ruzuku yoyote hivyo uendeshaji wa shule unategemea wazazi walipe ada.
 
Tambua watoto watasoma hadi December non stop
ile miezi mitatu ambayo hawakusoma ada inatakiwa ipelekwe Mbele yaani
carried Forward miezi mitatu us Merle ya September, October na December simple mathematics!!! Au wa carry forward miezi ya July, August na September ikiisha shule iombe wazazi walipe ada ya October, November na December
 
Mkuu vipi kuhusu kulipia usafiri ambao hajawahi kutumia kwa miezi 3? Ada sawa atafidia masomo lkn pia kuna lower classes ambazo wao muda wao ni uleule.
Kuhusu tozo ya usafiri, hapo mnaweza kuwekana chini na wenye shule ili mfikie muafaka wa malipo.
 
Lea hiyo
Kwa hiyo ndio upore pesa wazazi wakati chakula watoto hawakula Wala kulala mabwenini kwa miezi mitatu huo wizi

Miezi hiyo hawakuoga maji hivyo sehemu ya bili maji inatakiwa kuondoka nk
wengi wanaojibu hapa labda ni wamiliki wa shule au walimu shule binafsi ,shule ni za kibiashara nanunua huduma na kulipia siwezi lipia huduma ambayo hukunipa nalipiaje chakula ambacho mwanangu hakukitumia wasipoangalia baadhi ya shule zitapoteza wateja maana kama taasisi ya kibiashara inapata faida inatakiwa kuwa na contingency plan ndio maana kuna shule ziliona hilo zikaendelea kutoa masomo kwa mtandao shule kama hizo kwa nini nisilipe lakini kama muda wote wa kolona ulikuwa kimya na ninatumia gharama kumtafutia mtoto material halafu ghafla nirudi uniambie nilipe kigezo kwa kigezo gani?
 
Ahsanteni sana wachangiaji, ikumbukwe kuwa mzazi kumpeleka mtoto Shule ya private sio dhambi, hivi mnajua kuwa Madaktari wengi vijana wamesoma Shule za private, muhimbili wanachukua wanafunzi wenye point 3 mpaka 6 Tu, hizi point hazipo zana katika Shule za Serikali, chunguzeni, natumaini hata kada nyingine wamepitia Shule za private, wahandisi, Mwanasheria nk, hivyo sio dhambi, issue hapa ni khaki itendeke kwa wote, kuwe Na uhalisia wa ada inayolipwa, Covid imekula kote, hivi mnajua kuna wazazi wamesimamishwa kazi kutokana Na Covid, kuna wanafunzi hawana wazazi kutokana Na Covid, Covid haikula shuleni tu, hata wazazi wameathirika, pia katika kipindi hicho cha miezi Mitatu, wazazi waliingia gharama za matunzo kwa watoto wao, Narudia tena kuisihi Serikali kuingilia kati swala hili
 
Back
Top Bottom