Serikali iingilie kati ukatili dhidi ya Watanzania waishio Uturuki na nchi za Kiarabu

Mwingereza

JF-Expert Member
Jan 21, 2014
1,110
2,736
Nadhani mwaka jana, Serikali ilipata wakati mgumu sana kupitia balozi zake, kwani balozi hizo zilivamiwa na kesi nyingi za watanzania kunyanyasika nchi za kiarabu na China.

Kinachoendelea sasa ni ya kutisha kwani wadada wengi sana, wanakimbilia Dubai, Oman na Uturuki kujiuza. Siku ya Ijumaa, nikiwa Dubai, Polisi wa UAE walivamia sehemu moja ambayo ni pub maarufu na Wageningen wa Kizungu na kuwakamata wadada wa Kitanzania zaidi ya 30 waliokuwa wanajiuza eneo lile.

Swala kama hili nimeambiwa na rafiki yangu mmoja mfanya biashara anayeishi Istanbul Kwamba siku chache, alikutana na mdada wa Kitanzania aliyefanyiwa kitu kibaya na Waturuki kwani baada ya kufika, walinyang'anywa paspoti na kuingizwa kwenye Danguro.

Na haya mambo siyo tu Uturuki, Wadada wa Kitanzania wengi wanatumikishwa, Dubai, China (Macau na Gwanzhou) Uturuki na Oman.

Nadhani ni vyema serikali inaingilia kati hili swala la hawa vijana kabla halijawa bomu, maana wanaokimbia nchi ni wengi sana. Hasa sasa hivi, wadada ni wengi sana.
 
Kuna wadada walikwenda Arabuni na kufanikiwa kufanya kazi za utumishi wa ndani ma wamerudi katika nchi wakizotola wakiwa salama.

Ninadhani dhana muhimu ni kuwafahamisha wadada wanao kwenda huko kuhakikisha kuwa kila mkataba ni halali kisheria.

Kujiunga na mtandao wa telegram, ukianza kunyanyaswa post location ya mahali ulipo.
 
Yote haya yanaanza na sera mbaya za kiuchumi nyumbani zinazofanya watu wakahangaike nje.

Huo ndiyo mzizi wa fitina.

Kama nyumbani kungekuwa na nafasi nzuri nyingi za watu kufanya kazi na kutumia vipaji vyao, sifikiri kama watu wangeondoka kwa mafungu hivyo.

Sasa hivi ukianzisha kibiashara kidogo tu, utapigwa kodi na TRA mpaka ujute, kabla hata biashara haijaanza.

Ukisema uanzishe ki Youtube channel uangalie mingo mtandaoni ndiyo kabisa, unaanza kutozwa hela kabla hata hujaingiza.

Ajira za sekta rasmi chache na zinaenda kwa kujuana.

Kwa nini watu wasione bora wakajaribu maisha nje huko. Nako wanakutana na dhahama hizi.
 
Yote haya yanaanza na sera mbaya za kiuchumi nyumbani zinazofanya watu wakahangaike nje.

Huo ndiyo mzizi wa fitina.

Kama nyumbani kungekuwa na nafasi nzuri nyingi za watu kufanya kazi na kutumia vipaji vyao, sifikiri kama watu wangeondoka kwa mafungu hivyo.

Sasa hivi ukianzisha kibiashara kidogo tu, utapigwa kodi na TRA mpaka ujute, kabla hata biashara haijaanza.

Ukisemq uanzishe ki Youtube channel uangalie mingo mtandaoni ndiyo kabisa, unaanza kutozwa hela kabla hata hujaingiza.

Ajira za sektq rqsmi chache na zinaenda kwa kujuana.

Kwa nini watu wasione bora wakajaribu maisha nje huko. Nako wanakutana na dhahama hizi.
Kweli kabisa mkuu.
 
Waarabu co watu wazuri dada zetu hawasikii, unaendaje nchi ya mbali bila kua na info zozote. Nawaonea huruma lakn imeandikwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa . Yan hao waturuki wana roho mbaya sana sana
Waturuki siyo watu wazuri na wala hawana hisani au upendo kwa wageni. Mimi niliwahi kupanda Ndege yao toka USA hadi, nikaapa sitapanda ndege zao. Wasaidizi airport hawana msaada na ni kama wana dharau kwa wateja.

Baada ya kusema hayo, nirudi kwenye mada. Ni kweli wajukuu zetu wanateseka saana nje ya TZ. Wengi hutoka wakiahidiwa kazi na kipato kizuri, lakini huishia kulazimishwa kuwa machangudoa, wabeba dawa za kulevya, au wafanya kazi wa ndani.

Hili swala linaweza kutatuliwa na serikali, kwa sababu wahusika wanajulikana. Hawa madada wakikisha toka TZ na kuingia nchi za nje inakuwa kazi kuwasaidia kwa sababu mara nyingi hunyang'anywa passport na kuzuiwa kutoka nje. Kwa kifupi hawa ni watumwa. Kwa hiyo balozi siyo rahisi kuwapata na kuwasaidia.

Wengine huko huenda na madeni kama ya nauli n.k. Na deni hizo siyo pesa ndogo kwa maelfu ya watu. Serikali haiwezi kujiingiza kuwakomboa.

Mimi naona serikali ifanye mkakati wa elimu kwa umma kuhusu wale wanaotarajia kupata kazi nje. Ni vizuri watu wakubali kuhusisha vyombo vya serikali ili kubaini kama kweli hizo ajira n ajira salama au sivyo.

Ni jambo la maana iwepo sheria ya kujuwa hawa wajukuu zetu wameajiriwa na nani na pia kuwe na haki hawa wajukuu kupiga simu kujulisha wamefika na wanaendelea na kazi. Tatizo kubwa ni kuwa hii mipango ya ajira feki hufanyika kisirisiri. Hata kuondoka nako ni kisirisiri. Ila ukweli ni kuwa balozi za nje huhusika maana ndizo hutoa viza.

Kwa hiyo balozi za Kiarabu, China, na Uturki zinahusika moja kwa moja na hii mipango ya siri. Maana wasingehusika wangesaidia wakati wa matatizo. Hizo balozi zonajuwa wazi zinajihusisha na "human trafficking" ambalo ni kosa la jinai la kimataifa. Inatakiwa waambiwe na washirikiane na uhaniaji kukomesha tatizo hili. Lakini wao wamejikita katika kinga ya kibalozi kujihusisha na hii biashara haramu.

Watanzania, hasa wazazi wa wahusika nao wanatakiwa kuwapo somo hawa mabinti. Mabinti wengi, hudhania hizi ni ajira za kweli. Unajuwa tena kazi zimeadimika kwa hiyo mtu akiambiwa atalipwa $300-$500 anaona ameukat, na angekuwa ameukata kama ingekuwa kweli, lakini wengi huishia jela, wengine kufanya kazi bila mshahara na kuondoka huko hawawezi maana passport imefungiwa na mwajiri na hicho ndiyo kitambulisho pekee.
 
Yote haya yanaanza na sera mbaya za kiuchumi nyumbani zinazofanya watu wakahangaike nje.

Huo ndiyo mzizi wa fitina.

Kama nyumbani kungekuwa na nafasi nzuri nyingi za watu kufanya kazi na kutumia vipaji vyao, sifikiri kama watu wangeondoka kwa mafungu hivyo.

Sasa hivi ukianzisha kibiashara kidogo tu, utapigwa kodi na TRA mpaka ujute, kabla hata biashara haijaanza.

Ukisemq uanzishe ki Youtube channel uangalie mingo mtandaoni ndiyo kabisa, unaanza kutozwa hela kabla hata hujaingiza.

Ajira za sekta rasmi chache na zinaenda kwa kujuana.

Kwa nini watu wasione bora wakajaribu maisha nje huko. Nako wanakutana na dhahama hizi.
Ni sahihi. Hatupumui kwa mikodi isiyoangalia unapata kiasi gani.
 
Nadhani mwaka jana, Serikali ilipata wakati mgumu sana kupitia balozi zake, kwani balozi hizo zilivamiwa na kesi nyingi za watanzania kunyanyasika nchi za kiarabu na China. Kinachoendelea sasa ni ya kutisha kwani wadada wengi sana, wanakimbilia Dubai, Oman na Uturuki kujiuza. Siku ya Ijumaa, nikiwa Dubai, Polisi wa UAE walivamia sehemu moja ambayo ni pub maarufu na Wageningen wa Kizungu na kuwakamata wadada wa Kitanzania zaidi ya 30 waliokuwa wanajiuza eneo lile.

Swala kama hili nimeambiwa na rafiki yangu mmoja mfanya biashara anayeishi Istanbul Kwamba siku chache, alikutana na mdada wa Kitanzania aliyefanyiwa kitu kibaya na Waturuki kani baada ya kufika, walinyanganywa paspoti na kuingizwa kwenye Danguro. Na haya mambo siyo tu Uturuki, Wadada wa Kitanzania wengi wanatumikishwa, Dubai, China (Macau na Gwanzhou) Uturuki na Oman.

Nadhani ni vyema serikali inaingilia kati hili swala la hawa vijana kabla halijawa bomu, maana wanaokimbia nchi ni wengi sana. Hasa sasa hivi, wadada ni wengi sana
Kwani nani huwa anawapeleka huko?
 
Piganeni na hali zenu haya madanguro mbona hapa Tz yamejaa telee tena ya kila dizaini mnaonaje tukaanza kusafisha hapa ndani, kisha tukawakurupusha waendao huko, mleta mada tuwekee ushahidi wa hayo uliyotongoa iliingia fitina mpaka sasa madada zetu imekuwa mtihani kupata kuondoka kwa kwenda kufanya kazi ughaibuni kwa kisingizio cha kulazimishwa kufanya ukahaba, sasa nini kazi ya mabalozi wetu huko ?

Unajua kwenye kundi la mamba na kenge wamo.
 
Kuna wadada walikwenda Arabuni na kufanikiwa kufanya kazi za utumishi wa ndani ma wamerudi katika nchi wakizotola wakiwa salama.

Ninadhani dhana muhimu ni kwafahakisha wadada wanao kwenda huko kuhakikisha kuwa kila mkataba ni halali kisheria.

Kujiunga na mtandao wa telegram, ukianza kunyanyaswa post location ya mahali ulipo.
Hata hao makahaba wapost location?
 
Ni hivi Nje ya Tanzania kuna hizo kazi za ndani na kazi ya Umalaya!

Mabinti anapokuwa pale JKINA anakuwa anajua anaenda fuata nini India,China ,Uturuki n.k..mawakala wakubwa wanawauza malaya wa Kitanzania ni Wanaijeria wakisaidiana na wadada wa Kitanzania na wamejaa tele Dar na kila kukicha wapo wapya wanapelekwa. Wapo wanaokuja kupumzika na wapo wanaokuja na hela za kutafuta malaya wapya wa kuondoka nao.
 
Waarabu co watu wazuri dada zetu hawasikii, unaendaje nchi ya mbali bila kua na info zozote. Nawaonea huruma lakn imeandikwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa . Yan hao waturuki wana roho mbaya sana sana
Itoe akili yako shimoni, chuki yako itakuongezea umasikini tu issue ya human trafficking ni Dunia nzima, kuna wadada kibao Europe na America wameingizwa kwenye huu mtego, fanya kazi kijana ili familia yako isije ikaingia kwenye huu mtego coz hapa issue ni umasikini.
 
Back
Top Bottom