Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,274
- 23,050
Miaka ya hivi karibuni kumetokea upungufu mkubwa wa maembe dodo katika soko la Dar es Salaam na pengine sehemu nyingine.
Maembe haya matamu yasiyo na mfanowe kiasi cha kutungiwa wimbo wa "embe dodo,embe dodo limelala mchangani" yamekuwa adimu baada ya kutokea mbegu nyingine ambayo imekuwa ikitoa embe ambazo kwa nje zinafanana na dodo lakini kwa ladha na harufu ni tofauti sana.
Nliamua kufanya utafiti kisa cha kupotea kwa maembe dodo asili na badala yake kuwa na embe hizi zisizo na taste wala harufu tamu. Wengi wanasema kumekuwa na tabia ya kukata miti ya maembe dodo na kuchoma mkaa au kukata mbao.
Jambo hili limekuwa likinihuzunisha sana kila unapofika msimu wa maembe sababu najua sitopata kwa urahisi embe dodo asili.
WITO KWA SERIKALI
Miti hii ya Maembe Dodo ilindwe na igeuzwe kuwa ni moja ya Nyara za Serikali kama ilivyo miti ya Mikoko n.k
Isiruhusiwe kuchomwa mkaa wala kukatwa mbao. Maembe pia ikiwezekana yawe ni tunda la Taifa. Embe dodo ni moja ya the best maembe ambayo nimewahi kula duniani.
Tunapopoteza hazina hii kwa kuleta maembe ya kisasa au ambayo yamekuwa grafted.kiuhalisia tunawatendea makosa sana hata wazazi wetu na wakale.maana haya matunda yamekuwa yakipewa sifa nyingi sana.