Serikali iingilie kati suala la kadi za NHIF vyuoni. Inasikitisha wanapotupeleka

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
46,606
2,000
Nimepokea baadhi ya message inbox zingine zikinitisha nani kakwambia zingine utaratibu unakamilika kuwapatia kadi soon. Na nyingine ikishukuru kwa kufikisha ujumbe hadharani pengine wakubwa walikuwa hawajui. Tunaiomba serikali tukufu ya Mh. Magufuli iingilie kati upatikanaji wa kadi za bima vyuoni.

Huwezi ukapokea pesa za mtu ukaaa miezi zaidi ya minne ukisubiria kadi na wengine hata semister ya pili imefika hawana kadi. Ndugu zangu wapendwa hili jambo la kusikitisha sana sana limekuwa siri sasa nahisi lifike tamati. Wanapolipa MNS wanahitaji msaada wa kadi waweze kujiuguza.

Haipendezi wengine ada tunawalipia na bima tumelipa halafu unakuja kuomba pesa za dawa za malaria uti, gono. Kaswende nk. Mapenzi yangu kwa mungu serikali yetu pendwa iliyopo kwa ajili ya wananchi na watanzania kwa ujumla itatatua hili jambo.

Na ushauri kama NHIF hawapo tayari kutengeneza kadi wapewe bima zingine wala sio muda wa kulazimishana.
 
Hardbody

JF-Expert Member
Jan 25, 2017
2,271
2,000
Pdidy tatizo hasa ni nini me nmeshindwa kuelewa concept hasa ni ipi. Jitahid tulia uandike vizuri watakuelewa tu
 
Mtambwe

JF-Expert Member
Apr 14, 2014
715
1,000
Wewe ulieandika pia ni msomi wa chuo kikuu? Mbona umeandika kama umemaliza darasa la 10? Ulikuwa unakimbilia wapi mzee? Kama hawa ndio wasomi wetu bado tatizo lipo
 
mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
3,680
2,000
Wewe ulieandika pia ni msomi wa chuo kikuu? Mbona umeandika kama umemaliza darasa la 10? Ulikuwa unakimbilia wapi mzee? Kama hawa ndio wasomi wetu bado tatizo lipo
Huyo ndiye Pdidy miaka nenda rudi hapa JF huo ndio uandishi wake iwe masika iwe kiangazi keshasomeka, OVA.
 
Mnyaluhala.

JF-Expert Member
Jul 28, 2012
1,331
2,000
Kuna watoto makongo sekondari wamelipa Tsh. 54000 ya bima ya afya lakini hawajapewa tangu Januari hadi Desemba hii. Na mwakani wameambiwa walipe upya maana hii ni bima ya mwaka mmoja moja.
 
Keynes

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
531
225

Hili ni swala ambalo kwa mujibu wa utaratibu wa Bima ya Afya haliwezekani kutokea.

Michango ya Bima ya Afya ya wanafunzi wa shule ya Makongo hulipwa shuleni na Uongozi wa shule una jukumu la kuwasilisha michango NHIF ili vitambulisho viweze kutengenezwa. Kama kuna mzazi ambaye mwanaye hajapewa kitambulisho cha Bima ya Afya na michango alishalipa anatakiwa kuwasiliana na uongozi wa shule.

Nawa hakikishia michango ikiwasilishwa NHIF kitambulisho ni ndani ya siku 9. Ila kama michango haijawasilishwa ni dhahiri kwamba kitambulisho hakiwezi kutengenezwa.
 
Randy orton

JF-Expert Member
Apr 29, 2019
357
1,000
kuna ndugu yangu anasoma chuo cha mipango kila meaka analipia na kadi hapewi..

wanafunzi wakiandamana wanaonekana wakorofi wakati haki za msingi kama hizi zinaminywa na uongozi wa chuo ukishirikiana na serikali ya wanafunzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Coaster2015

JF-Expert Member
Aug 21, 2018
2,451
2,000
Hili ni swala ambalo kwa mujibu wa utaratibu wa Bima ya Afya haliwezekani kutokea.

Michango ya Bima ya Afya ya wanafunzi wa shule ya Makongo hulipwa shuleni na Uongozi wa shule una jukumu la kuwasilisha michango NHIF ili vitambulisho viweze kutengenezwa. Kama kuna mzazi ambaye mwanaye hajapewa kitambulisho cha Bima ya Afya na michango alishalipa anatakiwa kuwasiliana na uongozi wa shule.

Nawa hakikishia michango ikiwasilishwa NHIF kitambulisho ni ndani ya siku 9. Ila kama michango haijawasilishwa ni dhahiri kwamba kitambulisho hakiwezi kutengenezwa.
Nashauri watanzania tujenge tabia ya kuwa tunaungana mkono pale yanapotokea malalamiko dhidi ya taasisi ambazo chini ya serikali, kimsingi hapo mimi naamini kuna tatizo, kwa sababu name nina mwanafunzi chuoni, hao jamaa wa nhif ni wapuuzi sana, naona hapa mkuu unajaribu kuwatetea, hao jamaa kuna namba yao ya simu imewekwa kwenye matangazo yao, ile simu ukipiga inaita tuuu haipokelewi, utawasilianaje nao sasa ?, ukiangalia kwa makini hiyo itakuwa ni janja yao, mtu amelipa hela halafu wanajikalisha kimya bila kutoa kadi, unajua bila kadi maana yake huwezi kupata matibabu, hiyo ni janja yao, wanavuta muda ili ile hela iliyochangwa ibakie kwao, huduma zenyewe za ovyo na dhaifu sana kupiti hiyo bima
 
Keynes

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
531
225
Nimepokea baadhi ya message inbox zingine zikinitisha nani kakwambia zingine utaratibu unakamilika kuwapatia kadi soon. Na nyingine ikishukuru kwa kufikisha ujumbe hadharani pengine wakubwa walikuwa hawajui. Tunaiomba serikali tukufu ya Mh. Magufuli iingilie kati upatikanaji wa kadi za bima vyuoni.

Huwezi ukapokea pesa za mtu ukaaa miezi zaidi ya minne ukisubiria kadi na wengine hata semister ya pili imefika hawana kadi. Ndugu zangu wapendwa hili jambo la kusikitisha sana sana limekuwa siri sasa nahisi lifike tamati. Wanapolipa MNS wanahitaji msaada wa kadi waweze kujiuguza.

Haipendezi wengine ada tunawalipia na bima tumelipa halafu unakuja kuomba pesa za dawa za malaria uti, gono. Kaswende nk. Mapenzi yangu kwa mungu serikali yetu pendwa iliyopo kwa ajili ya wananchi na watanzania kwa ujumla itatatua hili jambo.

Na ushauri kama NHIF hawapo tayari kutengeneza kadi wapewe bima zingine wala sio muda wa kulazimishana.
Hallo Pdidy.
Kama JF expert member nilitarajia uweke majina ya chuo husika ambacho una uhakika kwamba michango ya wanafunzi imeshawasilishwa NHIF na bado wanafunzi hawajapata kadi kwa muda mrefu ili NHIF waweze kuchukua hatua mara moja.

NHIF kwa sasa ina mfumo mzuri sana kwa wanafunzi. Wanafunzi wote wanaomba vitambulisho katika mfumo wa online student registration portal Service Portal na vitambulisho vinatoka kwa haraka sana bila kujaza form.

Hapa jambo ninaloliona ni kwamba kuna vyuo ambavyo michango ya Bima ya Afya imeunganishwa na ada za wanafunzi hivyo baada ya malipo kufanyika chuoni Uongozi wa chuo unatakiwa kuwasilisha michango NHIF wanafunzi wapewe vitambulisho. Uongozi wa Vyuo vingi unajitahidi kufanya hivyo na vitambulisho vinatoka mapema sana.

Sasa kwa kuwasaidia NHIF na wanafunzi husika tunaomba utaje majina ya chuo husika kwa ufuatiliaji zaidi.
 
Keynes

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
531
225
Nashauri watanzania tujenge tabia ya kuwa tunaungana mkono pale yanapotokea malalamiko dhidi ya taasisi ambazo chini ya serikali, kimsingi hapo mimi naamini kuna tatizo, kwa sababu name nina mwanafunzi chuoni, hao jamaa wa nhif ni wapuuzi sana, naona hapa mkuu unajaribu kuwatetea, hao jamaa kuna namba yao ya simu imewekwa kwenye matangazo yao, ile simu ukipiga inaita tuuu haipokelewi, utawasilianaje nao sasa ?, ukiangalia kwa makini hiyo itakuwa ni janja yao, mtu amelipa hela halafu wanajikalisha kimya bila kutoa kadi, unajua bila kadi maana yake huwezi kupata matibabu, hiyo ni janja yao, wanavuta muda ili ile hela iliyochangwa ibakie kwao, huduma zenyewe za ovyo na dhaifu sana kupiti hiyo bima
Jitahidi kuandika ujumbe kwa uvumilivu ukijua hili ni jukwaa la kuelimishana na siyo kutukana.

Utaratibu wa NHIF ni lazima fedha zifike kwao ndo kadi za matibabu zitatolewa. Sasa wewe umelipa fedha ya matibabu shuleni na siyo NHIF. Hao NHIF watakupaje kadi?? Embu jiongeze as great thinker.
 
wa ukae

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
1,870
2,000
Hallo Pdidy.
Kama JF expert member nilitarajia uweke majina ya chuo husika ambacho una uhakika kwamba michango ya wanafunzi imeshawasilishwa NHIF na bado wanafunzi hawajapata kadi kwa muda mrefu ili NHIF waweze kuchukua hatua mara moja.

NHIF kwa sasa ina mfumo mzuri sana kwa wanafunzi. Wanafunzi wote wanaomba vitambulisho katika mfumo wa online student registration portal Service Portal na vitambulisho vinatoka kwa haraka sana bila kujaza form.

Hapa jambo ninaloliona ni kwamba kuna vyuo ambavyo michango ya Bima ya Afya imeunganishwa na ada za wanafunzi hivyo baada ya malipo kufanyika chuoni Uongozi wa chuo unatakiwa kuwasilisha michango NHIF wanafunzi wapewe vitambulisho. Uongozi wa Vyuo vingi unajitahidi kufanya hivyo na vitambulisho vinatoka mapema sana.

Sasa kwa kuwasaidia NHIF na wanafunzi husika tunaomba utaje majina ya chuo husika kwa ufuatiliaji zaidi.
Mkuu Chuo Kikuu Dodoma(Udom) mpaka sasa kuna vijana wengi wamelipa lakini mpaka sasa hawajapewa kadi kila wakifatilia wanapigwa danadana tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Coaster2015

JF-Expert Member
Aug 21, 2018
2,451
2,000
Jitahidi kuandika ujumbe kwa uvumilivu ukijua hili ni jukwaa la kuelimishana na siyo kutukana.

Utaratibu wa NHIF ni lazima fedha zifike kwao ndo kadi za matibabu zitatolewa. Sasa wewe umelipa fedha ya matibabu shuleni na siyo NHIF. Hao NHIF watakupaje kadi?? Embu jiongeze as great thinker.
Usiwatetee hao stupid, wanafunzi wanahangaika kwa uzembe wao, mleta mada amesema wapo wanafunzi waliosubiri kwa miezi zaidi ya sita, ni uzembe wa nhif, hela za Bima huwa tunaagizwa tulipe tofauti na Fees, chuoni anakosoma mwanangu kwa mfano huwa zinapelekwa chuoni na si kulipa benki, sasa kama nhif wapo wamekaa tu wanasubiri mpaka wafuatwe, maana yake ni kwamba hawana hata Utaratibu wa kufuatilia, we must be smart ili kufanya haya mambo yaende, wewe una uhakika gani kwamba pesa hizo za bima hazijapelekwa nhif ?, au unawatetea tu, tusipokuwa kuwa na utayari wa kusema tutakuwa tunaishia kujutia tu matokeo, ungekuwa na mwanafunzi chuoni aliyewahi kukumbana na karaha hii ungenielewa, ni jumkumu lao nhif kuhakikisha wanaweka mfumo rahisi wa kuhakikisha pesa zinazo wahusu wao zinafikishwa kwao ASAP, watanzania sijui tuna shida gani.
 
Coaster2015

JF-Expert Member
Aug 21, 2018
2,451
2,000
Shukrani sana Wa Ukae. NHIF wanakusikia na utaona hatua zinachukuliwa kuanzia muda huu na tatizo litakwisha.
Haya ndio mambo ya kienyeji, ina maana yasingesemwa hapa JF wangeendelea kukaa na ku relax huku wakilipwa mishahara ya bure ?, kodi zetu zinatumika ovyo sana kwenye nchi hii hasa utawala huu wa srikali ya awamu hii
 
Keynes

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
531
225
Haya ndio mambo ya kienyeji, ina maana yasingesemwa hapa JF wangeendelea kukaa na ku relax huku wakilipwa mishahara ya bure ?, kodi zetu zinatumika ovyo sana kwenye nchi hii hasa utawala huu wa srikali ya awamu hii

Wao NHIF wamelipokea hili kama lalamiko lakini haina maana kwamba wapo Kimya. UDOM ina wanafunzi Zaidi ya elfu 30 na wote wanahudumiwa na NHIF. Sasa ni jukumu la NHIF kufuatilia na kujua hili lalamiko ni la kweli? Na utaratibu wa upatikanaji wa vitambulisho kila upande ….yaani chou na NHIF wametimiza wajibu wao?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom