Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 17,038
- 22,714
Juzi asubuhi kwa mara ya kwanza hapa ninapoishi niilisikia Radio Tanzania.Nikajiuliza maswali mengi,lakini moja ni kwamba, hivi serikali yetu haielewi nguvu iliyoko kwenye "soft power? "Soft power" ni uwezo wa nchi kushawishi wengine kufanya wafanye inavyotaka bila kutumia nguvu." Nchi kama Marekani imefanikiwa sana kwa kutumia Hollywood na vyombo vyake vya habari kuifanya dunia iisujudie! Uingereza imetumia sana BBC na British Council.China inajaribu sana sasa hivi kutumia CGTN, Marshal Arts, Confucius Institute nk.
Hakuna mtu atakayepinga kwamba sasa hivi tuko kwenye collision course au vita kali na watawala wa dunia,hasa baada ya Rais kupewa ripoti ya mchanga wenye madini ya aina mbali mbali uliokuwa unasafirishwa nchi za nje, na Rais kutoa misimamo wake.
Katika hali hii hatuna budi kuwaandaa wananchi wetu for the uncertain future, lakini pia kuwashawishi ili waiunge mkono serikali yao katika vita kali iliyoko mbele yetu.Tuliona lililojitokeza baada ya Mwalimu kubinafsha mashamba ya Mkonge.
Ili kuweza kufanya hivyo ni lazima tuviboreshe vyombo vya habari vya serikali ili viweze kufanya kazi hiyo muhimu. Ili kufanikiwa katika hilo, ni lazima sasa kuifanya TBC radio na television visikike nchi nzima na viwe na wahudumu wazalendo na mahiri wenye uwezo mkubwa wa ushawishi.
Hatuwezi kuviachia kazi hii vyombo vya habari binafsi kwa kuwa tunajua vina mahusiano ya moja kwa moja ya kimaslahi na "watawala wa dunia," hawa hawa ambao makampuni yao ndiyo yanayotuhujumu kwa kutuibia rasilimali zetu.
Kiukweli hatuna muda wa kupoteza,we have to start now. Hawa watu maslahi yao yamegushwa, and they will leave no stone unturned.They are so cruel.