Serikali ihimize ongezeko la watu isilipige vita

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,286
hivi karibuni nimekuja kutambua kwamba kuna faida nyingi sana kwa taifa kuwa na population kubwa.

1: nimetambua kuwa watu wengi siyo zao la umasikini, bali umasikini hutokana na kushindwa kutumia rasilimali zilizopo, kushindwa kutumia nguvu, maarifa na tija ili kuproduce wealth.

2:Nimetambua kuwa serikali haipo responsible kuwapa watu ajira(isipo kuwa zile za serikalini), bali ipo kujenga mazingira ya watu kutumia vipawa vyao ili kujiajiri. kwa hivyo hoja ya kuwa serikali itashindwa kuwapatia watu ajira ni invalid.

3: nimetambua kuwa huduma za jamii kama vile shule, hospitali,barabara ni necessity, no matter watu wakiwa wengi au wachache binadamu ata struggle ili kuzipata. kwa hiyo hoja ya kwamba kama kuna watu wengi huenda huduma zitakwama au hazitawatosheleza watu nadhani ni invalid.

Kwa taifa kama la Tanzania kwa nini tunahitaji watu wengi?
1.Life span ya mtanzania ni ndogo haifiki miaka 60, tunahitaji watu wengi ili kubalance population kati ya wale wanaotutoka na wale wanaobaki kusukuma mbele gurudumu la ujenzi wa taifa

2:Watu wengi ni nguvu ya kiuchumi, ni soko kuu la bidhaa za ndani,na nje pia, watu wengi ni chimbuko la vipaji tofauti tofauti n,k

wanabodi mnaionaje hoja hii?
 
Back
Top Bottom