Serikali ihamasishe ulaji wa nyama ya kunguru ina faida kiafya

Mbona mtaani ilisemekana nyama ya kunguru ni chungu na hailiwi wala haiozi na hakuna bakteria wa kuisogolea na kuila, kunguru anakaukiana tu wala haozi.
kwa sisi watafiti hii ni fursa ya kitafiti huenda akawa na substance zitakazomsaidia binadamu kuishimiaka 150 mpaka 200
 
Kama lengo ni kuwatokomeza ni heri
kutafuta njia nyingine mbadala kuliko hiyo ya kuwala ya kuhatarisha afya zetu..

Kunguru haieleweki kwann amekuwa si kitoweo halali kwa jamii zetu nyingi za kitanzania kama sio yote..

Ndege wengine kama njiwa,chorwe,kuku nk wanaliwa ikawaje huyu asiliwe kama ilivyo kwa paka?nadhani iko namna,mana kwa wabongo wanavyopenda vitoweo angekuwa hana madhara wala shida ya aina yeyote kunguru angeshaisha ktk USO wa nchi yetu..
Ni kinyaa tu ndiyo kinachosumbua nzengo.

Mbona kobe, kenge, mamba, mijusi, popo, paka, mbwa, kimilanzoka, nyange nyange,panya nk nk, jamii zingine zinawalamba kama kawaida na hakuna madhara yoyote.

Sembuse huyo kunguru ashindikane, kwa madhara gani aliyonayo?

Ikihamasishwa kuliwa kwa kupitia njia ya tiba asili, kwa mfano kuongeza bahati ya kupata pesa, kupendwa, kurejesha mpenzi aliyetoroka, kuolewa haraka, nguvu za kiume na vitu kama hivyo vihusuzo mapenzi na mahusiano, ndege hao wataadimika kama siyo kuangamia kwa muda mfupi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua tunapitwa na hii fursa?Kunguru ana nyama nzuri balaa, ina protein nyingi sana, calories ndo usiseme,halafu haina colesterol kabisa

Hawa ndege wanakua tishio kwa hapa mjini, tungeanzisha kampeni ya kuwala nadhani wangeisha ama sio kupungua

Kumeanzishwa operesheni kibao za kuwaangamiza kunguru lakini zimefeli kula ndo suluhisho

Nadhani serikali ihamasishe hawa ndege waliwe maana tunakosa vingi tena kwa sasa nyama zilivyopanda bei ni muhimu sana.View attachment 2002056


Anza kuuza nyama kuchoma , kwa bei rahisi sana lakini uwaambie hawa ni kuku labda itasaidia
 
Huu ulaji wa aina ya kichina ambao hawaachi kitu chochote chenye mwendo ndo yanatuletea mabalaa yote haya ya magonjwa duniani.........kimsingi hayo magonjwa wanayapata kwa kula minyama na mindege ya porini ambayo haieleweki chanzo na inakuwa imebeba vimelea vingi hatari vya magonjwa.....tuachane na uroho wa wachina.​
 
Back
Top Bottom