Serikali ifute VAT kwenye vitabu; Kuchochea waandishi na usomaji

Kweli mwamba ngoma ngozi huvutia kwake. Mkuu wewe umeona ni vitabu tu, mbona vipo vingi vya kuondolewa VAT. Ila ni gharama kubwa aisee sasa si wengine tutaweza kununua kitabu hicho? hafu ni cha mapenzi...wakati vitabu vya kina Ben Carsons, Robert Kayosaki vinavyozungumzia maisha tunavipata kwa bei ya chini ya 15000tsh. Serikali inabidi iangalie upya hili suala, kitabu cha mapenzi nikanunue ziadi ya tsh40000 khaaaa, hata haikubaliki.

Mapenzi ndiyo yanafanya mambo mengine ya kina Carson na Kayosaki yawezekane.. think about it.. na siyo kitabu cha mapenzi ni cha saikolojia!
 
Voice of Wisdom, kwa kawaida malipo yoyote yanayoingizwa kwa kampuni yanakatwa kodi.

Mkjj, usiongelee kodi za malighafi na uchapaji, kuna gharama za serikali kama milioni za kuendesha biashara. Tbs, Osha, GCLA (wino ni sumu), NEMC, manispaa na mtaa just to name a few! How do u think we can afford governmental luxuries?

Hapo umenena.
Kodi ni nyingi na zinaumiza sana. nadhani kunahitajika review kubwa sana ya kodi zetu,
Hiyo itasaidia kupunguza wakwepa kodi
 
Tuweke mambo sawa
ili uruhusiwe ukutoza vat lazima uwe unauza bidha zinazotozwa vat na mauzo yako kwa mwaka yawe zaidi ya 40m.
Hakuna mtu anayeruhusiwa kutoza vat kwenye "exemp supplies" vitabu vikiwemo. Hata kama kuna malighafi zilizotozwa vat wakati wa kutengeneza kitabu inabidi yule mtengenezaji(printing co) ajiandikishe kama "partial exempt" ili mwisho wa mwezi aombe kurudishiwa vat aliyolipa wakatai ananunua malighafi i.e karatasi, wino hata umeme na kodi ya jengo kama ipo,ila kukuchaji wewe vat kwa ajili ya kitabu haruhusiwi.
Ila kwa sababu wafanya biashara wetu ndo hivyo na sisi hatujui utaratibu unakuta unachajiwa vat kama mteja na bado wanaenda kuidai serikali vat waliyolipa wakata wananunua maligafi za kutengenezea vitabu.
(kwa ufupi hakuna vat kwenye vitabu ama unapochapa au unaponunua )
Vitabu vipo exempted as per VAT ACT 1997 R.E 2006 Second Schedule item number 6...gharama za kutengeneza kitabu hazipo exempted the issue ni kwamba jisajili VAT ili kodi unayotozwa wakati wa kutengeneza kitabu(Input Tax) uweze kuwa refunded kwasababu your Output Tax(kodi utakayo toza wakati wa kuuza)ni 0 then utakuwa refunded the whole Input Tax.
 
Tuweke mambo sawa
ili uruhusiwe ukutoza vat lazima uwe unauza bidha zinazotozwa vat na mauzo yako kwa mwaka yawe zaidi ya 40m.
Hakuna mtu anayeruhusiwa kutoza vat kwenye "exemp supplies" vitabu vikiwemo. Hata kama kuna malighafi zilizotozwa vat wakati wa kutengeneza kitabu inabidi yule mtengenezaji(printing co) ajiandikishe kama "partial exempt" ili mwisho wa mwezi aombe kurudishiwa vat aliyolipa wakatai ananunua malighafi i.e karatasi, wino hata umeme na kodi ya jengo kama ipo,ila kukuchaji wewe vat kwa ajili ya kitabu haruhusiwi.
Ila kwa sababu wafanya biashara wetu ndo hivyo na sisi hatujui utaratibu unakuta unachajiwa vat kama mteja na bado wanaenda kuidai serikali vat waliyolipa wakata wananunua maligafi za kutengenezea vitabu.
(kwa ufupi hakuna vat kwenye vitabu ama unapochapa au unaponunua )

Asante kwa jibu hili; maana sijui wangapi wanafahamu hili. Maana kama kampuni kubwa ambayo nataka kuitumia wanaamua kuchaji VAT kwa mteja anayechapisha vitabu halafu watakaporudishiwa fedha na serikali wao wanarudisha kwa yule mteja au ndio inakuwa zawadi yao? Maana isije kuwa ni namna nyingine ya kutukamua wenzangu na miye?
 
kweli kabisa watu mnaamini hivyo? isije kuwa hata watoto wetu tunawalea kwa mawazo hayo. Tunaamini kuwa Waafrika ni wazuri katika mambo ya ngoma na sanaa!

Mzee Mwanakijiji,

..labda Raisi atakayekuja mwaka 2015 atabadilisha mwelekeo.

..hivi umesahau amri aliyotoa JK alipotembelea wizara ya elimu kwamba shule zote zitumie text book moja kwa kila somo??

..kwa mtizamo wa JK mwalimu kutumia kitabu zaidi ya kimoja ktk kufundishia ni jambo baya linalopaswa kupigwa marufuku.
 
[FONT=palatino linotype [USER=33296]mwa[/USER]kajila (poti) na Voice of Wisdom....
Bado hamjatuambia ni msaada gani mwandishi kama Mwanakijiji (na wengine ) anaweza kuupata katika mazingira haya ambapo lengo la TRA ( kuasaidia na kuboresha usomaji linahujumiwa) linaweza kubakia kama sheria inavyotaka!!
Mwanakijiji nipo tayari kukupa namba ya afisa pale TRA (ye ni principal officer) yupo idara ya "huduma kwa walipa kodi na elimu" pale TRA ili uje na jibu linaloeleweka na hueanda wakakupa msaada zaidi sababu pia wao wanafanya sana machapisho ya majarida yao na vijitabu!! Kama utataka tukutane PM.

Pia nikubaliane na mjumbe mmoja hapa kuwa its high time kama wadau wausomaji tuandae hoja tuipenyeze kwa wabunge wetu juu ya zengwe lililopo juu ya tasnia ya uandishi wa vitabu na uchapishaji (wa hata magazeti)....

Mi ni miongoni mwa watu tunaopinga kuwa sio kweli eti watz sio wasomaji ila, hamna juhudi za wazi katika kuwa fanya watz wawe wasomaji na zikashindikana, kwa mfano hizi za kufuta VAT cheki data za wadau (Mwakajila na Voice) zinavyoonyesha kuwa kuna wajanja weshapiga fitna ila hamna plan B ya serikali.......

Leo hii hamna hata gazeti la sh 300....

Ukitoa machache ya sh 400 na 500...

Magazeti yote makini yanaanzia sh 800......

Hebu mtu anitajie kitabu kinachouzwa chini ya sh 5000 na mimi kesho nkakitafute na ntawasimulia hapa!

Watz ni wasomaji ambao hawajaandaliwa na kujengwa ndio maana tunalalama hapa ila watz ni raia bora kama walivyo wazungu tu na tena naamini wana-inteligent kubwa sana ila dooooo bahati mbaya sana wamekuwa chini ya serikali hii ya vilaza isiyo na ndoto juu ya watu wake kuwa inataka kujenga watu wa namna gani!!!!!!
[/FONT]
 
Last edited by a moderator:
Tambua exempt supplie ikiwemo vitabu hutakiwi kulipia kodi kwani sheria inawaruhusu wafanyabiashara kudai kodi ya vat walipolipa kwenye maligafi mfano umeme wino maji usafirishaji n.k na jinsi ya kudai ipo wazi ktk sheria ya vat, sasa hawa wafanyabishara wanapokudai vat ktk kitabu ni wizi mkubwa.
Voice of Wisdom, kwa kawaida malipo yoyote yanayoingizwa kwa kampuni yanakatwa kodi.

Mkjj, usiongelee kodi za malighafi na uchapaji, kuna gharama za serikali kama milioni za kuendesha biashara. Tbs, Osha, GCLA (wino ni sumu), NEMC, manispaa na mtaa just to name a few! How do u think we can afford governmental luxuries?
 
Tuweke mambo sawa
ili uruhusiwe ukutoza vat lazima uwe unauza bidha zinazotozwa vat na mauzo yako kwa mwaka yawe zaidi ya 40m.
Hakuna mtu anayeruhusiwa kutoza vat kwenye "exemp supplies" vitabu vikiwemo. Hata kama kuna malighafi zilizotozwa vat wakati wa kutengeneza kitabu inabidi yule mtengenezaji(printing co) ajiandikishe kama "partial exempt" ili mwisho wa mwezi aombe kurudishiwa vat aliyolipa wakatai ananunua malighafi i.e karatasi, wino hata umeme na kodi ya jengo kama ipo,ila kukuchaji wewe vat kwa ajili ya kitabu haruhusiwi.
Ila kwa sababu wafanya biashara wetu ndo hivyo na sisi hatujui utaratibu unakuta unachajiwa vat kama mteja na bado wanaenda kuidai serikali vat waliyolipa wakata wananunua maligafi za kutengenezea vitabu.
(kwa ufupi hakuna vat kwenye vitabu ama unapochapa au unaponunua )

Naomba nisahihishe hili..

Gharama za uchapishaji wa Vitabu haipo exempted kwa mujibu wa sheria ya VAT 1997 R.E 2006 kinachoweza kufanyika ni ile input tax(VAT) inayotokana na gharama za kuchapisha kitabu inakuwa part of cost ya kutengeneza vitabu hivyo Mzee Mwanakijiji kama wewe ni mfanyabiashara wa vitabu na unatambulika na Mamlaka husika unaiweka ile input tax as part of cost na utaionesha kwenye financial statement(statement of comprehensive income )kama expense when arriving at profit or loss..Basis trader yoyote anayedeal na exempted supplies only input tax anayochajiwa ina form as part of expense in financial statements.
 
nadhani hapa tunapotezana kidogo; mimi sijioni kama mfanyabiashara wa vitabu; ni mtunzi tu. Lakini pia kuna element za biashara vile ville kwani nataka kupublish kitau mimi mwenyewe. Ninapolipa VAT kwa printer (as a publisher) hilo suala la kuwa exempted lipo au halipo? Mwisho wa siku imi na printer nani ataweza kuclaim ili kuwa refunded?
 
ok nadhani naelewa kidogo maana yeye kasema ni Output VAT... ambayo nawalipwa printer karibu 750,000 hivi..
 
Tuweke mambo sawa
ili uruhusiwe ukutoza vat lazima uwe unauza bidha zinazotozwa vat na mauzo yako kwa mwaka yawe zaidi ya 40m.
Hakuna mtu anayeruhusiwa kutoza vat kwenye "exemp supplies" vitabu vikiwemo. Hata kama kuna malighafi zilizotozwa vat wakati wa kutengeneza kitabu inabidi yule mtengenezaji(printing co) ajiandikishe kama "partial exempt" ili mwisho wa mwezi aombe kurudishiwa vat aliyolipa wakatai ananunua malighafi i.e karatasi, wino hata umeme na kodi ya jengo kama ipo,ila kukuchaji wewe vat kwa ajili ya kitabu haruhusiwi.
Ila kwa sababu wafanya biashara wetu ndo hivyo na sisi hatujui utaratibu unakuta unachajiwa vat kama mteja na bado wanaenda kuidai serikali vat waliyolipa wakata wananunua maligafi za kutengenezea vitabu.
(kwa ufupi hakuna vat kwenye vitabu ama unapochapa au unaponunua )

Mkuu, naona kama unachanganya mambo hapa.

Kilichokuwa exempted katika jedwali la pili ni bidhaa (vitabu) na sio huduma ya uchapishaji vitabu. Kama nimemwelewa Mwanakijiji vema ni kuwa amepewa tax invoice ili kuweza kulipia huduma ya kuchapiwa vitabu vyake. Kwa hiyo kisheria mchapaji anawajibika kutoza VAT kwenye huduma anayotoa ya uchapishaji. Mchapishaji kama yeye mwenyewe hauzi vitabu (au exempt product/service nyingine) kabisa hawezi kuwa partially exempt. Kama anachouza mchapaji ni hiyo huduma tu ya uchapishaji then anaweza ku claim inputa tax (VAT aliyochajiwa kwenye manunuzi yake) yote. Mfanyabiashara anakuwa partially exempt endapo tu anauza bidhaa/huduma mchanganyiko (exempt na taxable).

Mfanyabiashara ambaye anauza vitabu tu (in this case Mzee Mwanakijiji) hawezi kusajiliwa kwa VAT - labda kama ana export vitabu vyake/ au sehemu ya vitabu hivyo (na export hiyo inaweza kufikia sh 10m kwa miezi mitatu au sh 40m kwa mwaka). Kama asiposajiliwa kwa VAT, Mfanyabiashara huyu wa vitabu hataweza kudai marejesho ya VAT alizolipia katika uaandaji wa vitabu vyake (ikiwemo ile aliyomlipa mchapishaji). Hivyo kama anafanya analysis ya business case au pricing ya vitabu ni vema akatilia maani kuwa VAT itakuwa ni gharama ya ziada kwake.

Kwa hivyo bado nadhani hoja ya Mwanakijiji ya kutaka kuondoa VAT (zero rate) kwenye huduma ya uchapaji wa vitabu ni valid kwani uwepo wa VAT kwenye huduma hizo unaongeza gharama za vitabu kwa wateja (kama mfanyabiashara atataka kumantain margin yake).
 
Last edited by a moderator:
nadhani hapa tunapotezana kidogo; mimi sijioni kama mfanyabiashara wa vitabu; ni mtunzi tu. Lakini pia kuna element za biashara vile ville kwani nataka kupublish kitau mimi mwenyewe. Ninapolipa VAT kwa printer (as a publisher) hilo suala la kuwa exempted lipo au halipo? Mwisho wa siku imi na printer nani ataweza kuclaim ili kuwa refunded?
Biashara ni shughuli yeyote ya kununua au kuuza au kujishughulisha na shughuli yoyote kwa lengo la kupata au kutengeneza faida kama una lengo la kutengeneza faida basi wewe si mfanyabiashara then ile kodi uliyotozwa wakati wa kutengeneza kitabu itaform part ya gharama zako when calculating selling price ya hicho kitabu to arrive at zero profit since huna lengo la faida.lakini kama una lengo la faida then wewe ni mfanyabiashara hivyo utafuata yale ya hapo juu kuhusu financial statements..kwa upande wa mchapishaji yeye kwake ni output tax(kodi aliyotoza katika mauzo yake)then atafananisha na input tax(ile aliyotozwa katika kupata material kwa ajili ya shughuli yake ya uchapaji)then either atalipa the difference if output tax>Input tax au ataomba refund if input tax>output tax kwa mwezi husika wa biashara...publishing is not exempted fro VAT...
 
Back
Top Bottom