Serikali ifute VAT kwenye vitabu; Kuchochea waandishi na usomaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ifute VAT kwenye vitabu; Kuchochea waandishi na usomaji

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 4, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kati ya vitu ambavyo mtu unajifunza baada ya kujaribu ni hili la gharama la kuchapisha vitabu Tanzania. Kwa muda mrefu nimekuwa nikitatizika sana na changamoto ya watoto wetu kujisomea na waandishi wengi kujiingiza kwenye uandishi wa vitabu. Wakati niko katika hatua za mwisho za kuchapisha kitabu cha "Majeruhi wa Mapenzi" nimepewa quotes za kuchapisha kitabu hiki Tanzania ambapo nimekuta kuwa VAT ni asilimia 18!

  Mara moja nikaona mojawapo ya matatizo makubwa.

  a. Nikiamua kuchapa vitabu mia tano tu kila kitabu (chenye kurasa 288) kina gharimu 39,500 najiuliza nitauza kitabu hicho kimoja kwa shilingi ngapi ili kurudisha japo gharama za kuchapishia?

  b. Unapoweka gharama ya kodi kubwa kama hii ni watu wangapi wanaoweza kuchapisha vitabu Tanzania? Kwanini isiwekwe kwenye viwango vya chini na ikiwezekana 0% (zero rating protection0 kwenye vitabu vya lugha ya Kiswahili na vya masomo?

  c. Hivi hatuoni kwa kufanya gharama ya kuchapisha vitabu kuwa kubwa sana tunachochea ujinga kwani ama vitabu vinakuwa ni vya bei ya juu sana au watu wengi ambao wanataka kuchapisha vitabu wanajikuta wanakwama. Kwa mfano, invoice mojawapo ya makampuni ninayozungumza nayo nyumbani kwa vitabu 5000 ni shilingi milioni 39. Matokeo yake wengi wanaochapisha vitabu Tanzania inabidi yawe ni mashirika au taasisi ambazo zinapata ufadhili fulani au watu ambao wana uwezo mkubwa wa kifedha?

  d. Je, watawala wetu hawaoni umuhimu wa kupunguza au kuondoa kabisa VAT kwenye vitabu na badala yake waache kodi ilipwe wakati wa manunuzi kama (Sales Tax) ya kawaida badala ya kumpitishia mtunzi mzigo wa kodi?

  Ombi langu:

  Serikali ifute VAT kwenye vitabu visivyozidi kurasa 300 na kwa vile vinavyozidi basi VAT iwe kwa kiasi cha chini kinachowezekana. Ikumbukwe wachapishaji tayari wamelipa kodi kadhaa katika kuagiza malighafi mbalimbali na bado kuna gharama nyingine zinazoingia. Lengo ni kufanya vitabu vichapwe kwa urahisi na inaweza kuchochea ushindani mkubwa hata kwenye nchi za jirani ambako nako gharama ya kuchapisha vitabu ni kubwa au wameamua kuweka VAT (Kenya mwaka jana walitaka kuweka VAT ya 18% kwenye vitabu vya kiada).
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  This could be the 'game changing thread' kutoka kwako Mwanakijiji.....

  sio tu kodi za vitabu
  kodi zoote za nchi zinahitaji kutazamwa upya....

  kodi za wafanyakazi pia ni kubwa mno.....na nyingine nyiingi

  next time ukisikia wafanyabiashara wanafanya hila kukwepa kodi
  usikimbilie kuwaita mafisadi........hii nchi ina 'kiwango cha kodi cha kifisadi'
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Mkuu siyo wachapishaji vitabu tu wanashindwa kuchapisha vitabu vingi, bali VAT inasababisha hata wasomaji wa vitabu washindwa kununua vitabu hivyo!
  Nakumbuka nilinunua vitabu ambavyo vingegharimu sh.450,000 bila VAT, lakini nilikuja kulipa sh.531,000. Maana yake ni kwamba VAT imesababisha kujenga tabaka la wasomaji, yaani wasomaji wa vipeperushi, na wasomaji wa vitabu ambao standard yao ya maisha ni nzuri.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Yaani, kwa muda mrefu sana nilikuwa najaribu kujiuliza ni kwa vipi watu wetu watachochewa kuwa wasomaji; lakini sasa sehemu ya jibu iko wazi. Najiuliza watu kama HakiElimu wao wanachapa vitabu wao wenyewe au wanatumia makampuni ya pembeni?
   
 5. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Labda inaweza kusaidia watanzania wengi kusoma vitabu, lakini sina uhakika sana kama gharama ndio tatizo, watanzania hatuna utamaduni wa kusoma, hasa vitu vya maana, labda vitabu vya hadithi za shigongo ndio vipunguziwe kodi.
   
 6. Codon

  Codon JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Pole mwanakijiji!Nadhani umeliona hili baada kuwa muhanga eee?Watu wengi wanashindwa mambo mengi sababu nikodi tu!
   
 7. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2012
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Lakini waende zaidi ya hapo.. otherwise tunaendelea kusoma vichwa habari tu....
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280  Kuna wengine wamesema pia kodi ya makaratasi ni juu sana; hivi kwa anayejua kuna kodi ngapi zinalipwa kabla ya mtu kupata kitabu mkononi:

  a. Malighafi (total taxes???)
  b. Kuchapisha
  c. Kuuza (whole sale na retail wanalipa kodi tena???)
  d. Kusafarisha
   
 9. S

  Shiefl Senior Member

  #9
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nchi imejaa wahuni wasiofikiria.

  Halafu wanafurahia watoto wetu wakisoma maphotocopy ya vitabu na madesa (notes) za wenzao. Kinachotakiwa bwana Mwanakijiji ni kuaandaa hoja hii vizuri na kuwapa akina Mnyika wakaipeleke Bungeni halafu na sisi wananchi tupaze sauti zetu.

  Sijui ni hili watasema kama wale wakuu wanaona foleni za magari dar ni maendeleo halafu wanaweka kodi inayolingana karibu sawa na gharama ya kununulia gari.

  Watu wanatakiwa kushawishiwa kufanya kazi kama hizi za kuandika vitabu at 0 zero VAT and let the consumers pay at the sales tax. Yaani mtu uumize akili zako kuandika kitabu halafu watu wengine wanakupangia kodi kama wanavyojua wao...Mbaya zaidi hatuoni faida za hizi kodi zaidi kujinunulia midege inayokunywa mafuta kama walevi wa pombe za kienyeji.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  halafu kodi kubwa namna hiyo kwa uwezo gani wa sekta ya uchapishaji nchini? Hivi hadi hivi sasa inachangia kiasi gani kwenye GDP?
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Pengine nayo pia ni sababu ya watanzania wengi kutopenda kujisomea badala yake wanategemea zaidi kuhadithiwa hadithi ya karibu kila kitu.
   
 12. Voice of Wisdom

  Voice of Wisdom JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 541
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  as per VAT Act 1997 section 10
  10.-(1) A supply of goods or services is an exempt supply if it is of a description specified in the Second Schedule to this Act.
  (2) The VAT is not chargeable on an exempt supply, and deduction or credit of input tax is not allowable on purchases made in respect of the exempt supply.
  also check the second schedule of the same Act
  SECOND SCHEDULE
  (Section 10)

  EXEMPT SUPPLIES AND IMPORTS
  1.-Food, crops and livestock supplies

  1. Livestock - live cattle, swine, sheep, goats, game, poultry and other animals of a kind generally used for human consumption.
  2. Animal products - unprocessed edible meat and offal of cattle, swine, sheep, goats, game and poultry (including eggs), except – pate, fatty livers of geese or ducks and any other produce prescribed by the Minister by regulation.
  3. Unprocessed dairy products - cow or goat milk.
  4. Fish - all unprocessed fish, except shellfish, and ornamental fish.
  5. Unprocessed agricultural products - edible vegetables, fruits, nuts, bulbs and tubers, maize, wheat and other cereals, meal flour, tobacco, cashew nuts, coffee, tea, pyrethrum, cotton, sisal, sugarcane, seeds and plants thereof.
  Notes: 1 For the purposes of this item goods shall be regarded as unprocessed if they have undergone only simple process of preparation or preservation such as freezing, chilling, drying, salting, smoking, stripping or polishing.
  2. None of the above can be exempted when they are supplied in the
  course of catering by a restaurant, cafeteria, canteen or like establishment.
  6. Locally grown tea whether in the form of made tea, blended orpacked tea.
  (7) Locally grown coffee whether in the form of roasted, grounded orinstant coffee.

  2. Pesticides, fertilizers, etc.
  The supply of fertilizers, pesticides, insecticides, fungicides,rodenticides, herbicides, anti-sprouting products, and plant growth regulations, and similar products which are necessary for use in agricultural purposes.

  3. Health Supplies

  (1) Health and medical services by a registered medical practitioner,optician, dentist, hospital or clinic.
  (2) Human medicines, drugs and requirement which have been approved by the Minister responsible for Health upon recommendation of the Pharmacy Board.
  (3) [Deleted by Act No.2 of 1998, Sch.].
  (4) Articles designed for use by the blind or disabled.
  (5) Mosquito coils.
  (6) Sanitary pads.

  4. Educational supplies Educational services provided by an establishment registered by the Government.

  5. Veterinary supplies
  (1) The supply of veterinary services by a registered veterinary practitioner.
  (2) The supply of veterinary medicines, drugs and equipment which have been approved by the Minister responsible for Health upon recommendation of the Pharmacy Board.
  (3) The supply to a registered veterinary practitioner of equipment designed solely for veterinary use.

  6. Books and newspapers
  (1) Books, booklets, maps or charts.
  (2) Newspapers, journals, magazines or periodicals.

  list continues
  swali linakuja, unalipa VAT wakati gani? wakati wa kuchapisha au wakati wa kuuza/kununua?
  kwa kifupi vitabu havichajiwi VAT
  kwa wanaohitaji hiyo sheria ya kod na nyingine za kodi niachieni email zenu niwatumie ili tuweze kuingalia kwa upana zaidi
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Miye niko kwenye kuchapa; VAT nimenukuliwa kwenye invoice yangu kabla ya kuchapa. Hiyo sheria inaposema vitabu pia viko exempted ina maana kwa mnunuzi au hata wakati wa kwenda kuchapa maana kama ni kweli sijui watu wangapi ambao wameenda kuchapisha vitabu na wakalipia VAT.
   
 14. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Voice of Wisdom, kwa kawaida malipo yoyote yanayoingizwa kwa kampuni yanakatwa kodi.

  Mkjj, usiongelee kodi za malighafi na uchapaji, kuna gharama za serikali kama milioni za kuendesha biashara. Tbs, Osha, GCLA (wino ni sumu), NEMC, manispaa na mtaa just to name a few! How do u think we can afford governmental luxuries?
   
 15. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #15
  Jun 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu afadhali umeiweka hapa manake mimi nimekuwa nikinunua vitabu bila VAT pale Scholastic Bookshop Mlimani City lakini naona watu wanasema kuna VAT.
   
 16. mwakajila

  mwakajila Senior Member

  #16
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Vitabu vipo exempted as per VAT ACT 1997 R.E 2006 Second Schedule item number 6...gharama za kutengeneza kitabu hazipo exempted the issue ni kwamba jisajili VAT ili kodi unayotozwa wakati wa kutengeneza kitabu(Input Tax) uweze kuwa refunded kwasababu your Output Tax(kodi utakayo toza wakati wa kuuza)ni 0 then utakuwa refunded the whole Input Tax.
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  mtu anaponunua kitabu kwenye duka analipia gharama ya mimi kwani VAT ninayolipa wakati wa kuchapa naipitisha kwenye bei ya kitabu siyo?
   
 18. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #18
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Wabongo wengi hawapendi kusoma vitabu hata kama ni vya bure, hivyo hata ikiondolewa VAT na vitabu kuwa bure, watnganyika na wzanzibar wengi hawapendi kusoma vitabu, that why hata hii thread imekosa wachangiaji kwenye issue ya vitabu wabongo wanalala mitini
   
 19. mwakajila

  mwakajila Senior Member

  #19
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  .

  VAT inatozwa kwenye Value Added ya bidhaa..mfano wewe ni wholesaler umenunua kwa producer kwa 1000/= ukatozwa kodi ya VAT 152(18/118*1000) bidhaa hii ikifika dukani kwako hutoiuza kwa 1000/= lazima utaweka gharama zako za biashara kama usafiri pamoja na faida let say unauza kwa 1200/= then VAT inatozwa kwenye 1200*18%=216 tofauti ni 216-152=64 kwa vitabu sasa kodi uliyotozwa wakati wa kutengeneza ni 152 lakini ulipouza ni 0 hivyo hii tofauti(152) unapaswa kurudishiwa na serikali.
   
 20. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #20
  Jun 5, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Kweli mwamba ngoma ngozi huvutia kwake. Mkuu wewe umeona ni vitabu tu, mbona vipo vingi vya kuondolewa VAT. Ila ni gharama kubwa aisee sasa si wengine tutaweza kununua kitabu hicho? hafu ni cha mapenzi...wakati vitabu vya kina Ben Carsons, Robert Kayosaki vinavyozungumzia maisha tunavipata kwa bei ya chini ya 15000tsh. Serikali inabidi iangalie upya hili suala, kitabu cha mapenzi nikanunue ziadi ya tsh40000 khaaaa, hata haikubaliki.
   
Loading...