GODZILLA
JF-Expert Member
- Dec 26, 2014
- 5,902
- 10,502
Nimetembea humo majumbani unakuta katoto ka kike kana miaka tisa eti kanaitwa "house girl".
Katoto kadogo kanatumikishwa kazi nzito kuanzia alfajiri mpaka saa sita usiku. Eti "ameajiriwa".
Natambua, serikali imepitisha sheria mbalimbali za kuzuia kazi za watoto, kama vile sheria za kazi, sheria za shule na mikataba mbalimbali ya kimataifa!
Lakini sheria hizi sio rafiki na hazijatibu kabisa tatizo la watoto wadogo kutumikishwa majumbani.
Sheria zinazungumza kuhusu kuzuiwa kufanyishwa kazi nzito nzito za migodini nakadhalika. Lakini hazijasema ni namna gani watoto wadogo wa kike wanaweza kutwezwa majumbani kupitia hichi kinachoitwa "house girl".
Ni sheria legevu mno na hazitiliwi maanani.
Wakati mwingine najiuliza kama kuna vyombo vinavyosimamia kwa dhati hizi sheria za kuwalinda watoto! Pamoja na ulegevu wake, lakini huenda zingeweza kudhibiti huu udhalilishaji kwa kiwango fulani.
Hawa watoto wanalawitiwa na kunajisiwa, licha ya madhara mengine mengi ya kisaikolojia, traumatization, kukosa fursa ya elimu, kuadhibiwa vikali, kunyanyaswa, kufanywa watumwa na hata kuuwawa.
Kazi za majumbani zifanywe strictly na mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka kumi na nane na hata juu zaidi ya hapo. Hii iwe criminalized kwa kiwango cha adhabu kali.
Futa kabisa hizi 'housegirl'. Wanatumia watoto wa watu vibaya mno na kwa namna ya kudhalilisha kulikopindukia.