Hot bird
Member
- Jan 18, 2021
- 56
- 100
Wakuu habari zenu hapa ndani?
Nimeandika uzi huu kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya taifa na ustawi wa jamii kwa ujumla, hii ni kutokana na ukweli kuwa taasisi nyingi za serikali zinaendeshwa kwa utendaji mbovu, sasa leo naandika machache kuhusu chuo cha kilimo cha sokoine (SUA), kilichopo Morogoro.
1. Ndio chuo chenye umaskini wa hali ya juu, yaani ni kawaida kabisa kukuta wahadhiri wake wakilalamika kukosa pesa za kuendelezwa sababu tu chuo hakina pesa wakati huohuo vyuo vingine mambo yanaenda vizuri tu.
2. Miundombinu ya chuo hasa kufundishia ni mibovu na imechoka sana (nitaambatanisha picha ya wanafunzi wakisomea nje ilhali lecturer yuko ndani).
3. Chuo kina wakufunzi WENGI ambao wamesoma hapohapo na hata mkiitwa interview wengi watachukua wanafunzi waliosoma hapohapo,hii imesababisha hali ya kutohoji utendaji wa viongozi wa chuo.
4. Magari ya chuo yana hali mbaya,na uongozi haujali wala haufatulii hili (kiambatanisho kipo).
5. Kuna rushwa kubwa ya ngono chuoni, hasa kwa wahadhiri na wale watu wa hostel, wanataka sana rushwa kwa wanafunzi hasa wa kike.
6. Barabara za chuo hazikidhi vigezo vya chuo kikuu, tena hapa uongozi umejinasibu kuwa umetengeneza barabara ila ni kwa kiwango duni sana pesa itakua imeliwa.
7. Vitendea kazi (mfano projector) vya kufundishia havipo kwa baadhi ya vitivo na kwa wenye navyo basi vipo vichache sana.
Naandika uzi huu kuomba serikali ifatilie utendaji kazi wa chuo hiki, yawezekana kabisa VC wa chuo anafanya kazi nzuri sana ila kuna utaratibu mbovu wa watu wa chini yake.