Serikali Ifuate Mwaka Wa Fedha Kupandisha Bei Ya Huduma Zake Kwa Wananchi.

augustino ameri

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
267
170
Serikali Iliweka Kuwa Kila Mwezi Julai,katika Kipindi Hicho Hupandisha Mishahara Ya Watumishi Wake Na Kupanga Bajeti Yake.Sasa Inakuwaje Serikali Ipandishe Gharama Za Maji ,Umeme Katikati Ya Mwaka.Wadau Mnaonaje Hilo.
 

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
7,135
2,000
Hili linaathiri sana uchumi wa mtu mmojammoja na wa nchi kwa ujumla wake.
Hawa wenye kupanga bei nafikiri hawawasiliani na vyama vya wafanyakazi ili wasikilize mawazo ya wafanyakazi. Tunaumizwa sana na maongezeko ya bei katikati ya bajeti ya serikali. Na hili litazidisha mateso kwa familia na hivyo kupelekea ufanisi na utendaji kazi kushuka kwa kasi. Sijui wachumi wa nchi hii kama wana mchango wowote katika kulisemea hili zaidi ya ndiyo mzee ili waendelee kula!
Mwisho wa yote ni wizi, rushwa na ubadhirifu wa kiwango cha juu utatamalaki.
Inasikitisha sana kiukweli kwa namna wanavyotutenda.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom