ibesa mau
JF-Expert Member
- Sep 17, 2015
- 2,109
- 1,692
Wakati akifanya ziara nchini za kuwaaga watanzania mwaka 2015 aliwahi tamka kwamba ameajiri walimu wengi katika sekondari na tatizo analoliacha ni upungufu wa walimu shule za msingi na walimu wa sayansi masekondarini. Alisema kwamba hata ajiri tena walimu wa arts katika sekondari na walimu hao watapelekwa shule za msingi, katika hotuba yake alitolea mfano nchi ya kenya mtu mwenye mastars kufundisha darasa la awali, na akasema kwamba hayo ndio maendeleo.
Sasa hii serikali hii inashindwa nini kuwaajiri hao walimu wa arts wakafundishe shule za msingi ambako kuna upungufu mkubwa wa walimu. shule nyingi za msingi zilizopo vijijini zina walimu watatu hadi watano.
Naishauri serikali iwaajiri walimu hao katika shule zetu za msingi baadala ya kuwaacha mitaani wakizurula tu bila kazi.