Serikali ifuate mawazo ya Kikwete katika kuwaajiri walimu wa arts.

ibesa mau

JF-Expert Member
Sep 17, 2015
2,113
2,000
Wakati akifanya ziara nchini za kuwaaga watanzania mwaka 2015 aliwahi tamka kwamba ameajiri walimu wengi katika sekondari na tatizo analoliacha ni upungufu wa walimu shule za msingi na walimu wa sayansi masekondarini. Alisema kwamba hata ajiri tena walimu wa arts katika sekondari na walimu hao watapelekwa shule za msingi, katika hotuba yake alitolea mfano nchi ya kenya mtu mwenye mastars kufundisha darasa la awali, na akasema kwamba hayo ndio maendeleo.

Sasa hii serikali hii inashindwa nini kuwaajiri hao walimu wa arts wakafundishe shule za msingi ambako kuna upungufu mkubwa wa walimu. shule nyingi za msingi zilizopo vijijini zina walimu watatu hadi watano.

Naishauri serikali iwaajiri walimu hao katika shule zetu za msingi baadala ya kuwaacha mitaani wakizurula tu bila kazi.
 
Puyet Babel

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
3,596
2,000
Serkali haina pesa ya kuajiri!
Zaid wanatupigia porojo tu za sayansi na hisabati
 
Radicalist

Member
Jan 22, 2015
22
45
Mimi nina kadigrii kangu hapa kamoja namshauri Magu atupeleke huko hata primary tukafanye mapinduzi ya Elimu.
 
balimar

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
5,033
2,000
Mimi nijuavyo shule za msingi kuna maoungufu makubwa ya walimu kwa takriban miaka kumi ninayofanya kazi ya kufunza. Ila nadhani ni mjadala wa pamoja unahitajika kwani sekondari kuna walimu wengi sana mpaka inafikia hata kugawana baadhi ya mada katika somo moja mf. geograph mwl A anafundisha Map reading mwl B Physical geograph mwl C photograph lakini huku misingi walimu mpo watano wanafunzi mia nne.
Halafu nyie ambao hamjaajiriwa wala msijidanganye primary kuna walimu ni MA holders na wengine ni PhD candidates sasa hizo degree ni walimu wa darasa tu. Karibuni muone hata kupata ualimu wa zamu utakua unaomba poo.
Shule za msingi walimu wanajiendeleza kwa kasi kubwa kuliko secondary nadhani ingawa wengi wanadhani primary ni walimu vilaza
Mwisho wala usiogope kuajiriwa primary, serikali hailipi mshahara kutokana na shule unayofundisha bali kwa kiwango chako cha elimu. Hivyo ukiwa cheti mshahara ni wa cheti halikadharika kwa diploma hata degree.
karibuni msangamano wa wanafunzi huku primary plus elimu bure walimu primary wanahitajika acheni mzaha
 
ILAN RAMON

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
7,137
2,000
This administration has failed in everything mwaka 1 wamejenga barabara moja tu daresalama sitimbi sijui pakoje no wonder Nyerere alisema kuna makabila hayafai kupewa urais kumbe kweli
 
Hyungnim

JF-Expert Member
Sep 25, 2016
301
500
Huku mtaani si rafiki!Hali ya uchumi haitutendei hisani waalimu wa masomo ya sanaa tuliohitimu mwaka Jana.

Matumbo yamesinyaa,nyuso zimenywea na kujawa na chuki!hakuna tabasamu angavu.Viatu vimeisha upande,nguo za ndani zilizobatizwa jina la chupi na bokusa zimeunguzwa na joto kali!mpya ntazitoa wapi na hali yenyewe hii?shikamoo ujamaa
 
Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
15,077
2,000
Wakati akifanya ziara nchini za kuwaaga watanzania mwaka 2015 aliwahi tamka kwamba ameajiri walimu wengi katika sekondari na tatizo analoliacha ni upungufu wa walimu shule za msingi na walimu wa sayansi masekondarini. Alisema kwamba hata ajiri tena walimu wa arts katika sekondari na walimu hao watapelekwa shule za msingi, katika hotuba yake alitolea mfano nchi ya kenya mtu mwenye mastars kufundisha darasa la awali, na akasema kwamba hayo ndio maendeleo.

Sasa hii serikali hii inashindwa nini kuwaajiri hao walimu wa arts wakafundishe shule za msingi ambako kuna upungufu mkubwa wa walimu. shule nyingi za msingi zilizopo vijijini zina walimu watatu hadi watano.

Naishauri serikali iwaajiri walimu hao katika shule zetu za msingi baadala ya kuwaacha mitaani wakizurula tu bila kazi.
Sasa na wale wa diploma na certificate wataenda wapi??? Au ndio ubinafsi??
 
Jenerali Ambamba

JF-Expert Member
Sep 8, 2014
3,311
2,000
Ni kweli mkuu, nakumbuka JK alisema kuanzia sasa (Mwaka Jana) Serikali itaanza kuajiri walimu wa degree Shule za msingi, hili naliunga mkono sana, Magufuli afuate ushauri huu, please...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom