Serikali ifikirie namna ya kuwasaidia wanavyuo ambao wengi wao walikuwa wamepanga vyumba, bila kufanya hivyo mali zao watazikuta nje

Akilitime

JF-Expert Member
Dec 27, 2017
581
757
Vyuo vingi nchini havina hostel za kuwaacomodate wanafunzi wote, hivyo wengi wao huishia kutafuta vyumba mitaani (wale tuliosomea UDSM MIAKA ILE TUNALIFAHAMU BALAA HILI)

Wakati serikali ikitangaza 30 za kukaa nyumbani, ndicho kipindi ambacho wanafunzi hawa walikuwa wanarejea vyuoni kutoka likizo, wengi wao wakiwa wanasubiri hela ya kujikimu ili kuweza kulipia/kurenew kodi za magetto yao(kama wanavoita wao)

Sasa kwa hall kama ya Dar es salaam Ni mwenye nyumba yupi ambaye atakubali nyumba yake iwe na wapangaji ambao mda wao wa Kodi umeisha?

Nakumbuka kipindi kile Kodi ikiisha ukapitisha siku mbili tu, hayo maneno utakayonyeshewa kutoka kwa Landlord asee utatafuta hela usiku huo huo ukalipe.

Serikali endapo itaongeza siku za hawa wanafunzi kuendelea kukaa nyumbani basi iangalie namna ya kuwasaidia ili vitu vyao huko mitaani vibaki salama.

Zile familia zenye uwezo ndo zitapinga uzi huu, lakini wenzangu na Mimi wakulima wataelewa ninachoongea.

#serikali ya wanyonge
 
Labda serikali ya kenya inaweza kuwasaidia sio hii ya kulala kwenye mawe na kunywa kahawa watu wakitaabika
 
Wanafunzi wengi wanafurahia likizo hii iwe ndefu, sema shauri kitu kimoja.... boom liendelee kutoka kila muda ukifika ili walipe hizo kodi zao.

Nimewaza wewe ni mmoja wa hao Landlords.
 
Mimi sio Landlord wa wanafunzi
Wanafunzi wengi wanafurahia likizo hii iwe ndefu, sema shauri kitu kimoja.... boom liendelee kutoka kila muda ukifika ili walipe hizo kodi zao.

Nimewaza wewe ni mmoja wa hao Landlords.
 
Akilitime, Sasa unadhan kuna wakuja kuwalipia kodi??

Au unataka hii serikali ya awamu ta tano ijee iwatolee vitu vyenu kwenye Mageto

Kitu kidogo kama hich ndo cha
kushilikisha serikali!!?

Huwezi ongea kikubwa na mwenye nyumba, si anaona janga lililopo?!

Nyie wasomi wa leo, kudadafua vtu
Vidogo hiv mnakwama hiv kazi mtaziweza kweli!?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom