Serikali ifike uamuzi wa kutoa ruzuku kubwa katika mafuta

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Kutokana na kupanda kwa mafuta sasa serikali inatakiwa kuja na matazamo mbadala katika swala la ongezeko la Bei ya mafuta,isipokuwa makini itashindwa kukontroo bei za bidhaa nchini kwakuwa imeshindwa kukontroo bei ya mafuta!.

Kiukweli hapo Serikali ahina chakufanya zaidi yakuweka rudhuku katika wafanyabiashara kwa maana ya kuondoa kodi au kupunguza.

Na isipofanya hivyo leo sukari ipo katika Tsh 2850/= itafika 3400 je bidhaa nyingine itafikia kiasi gani?. Leo Jiji la Dar es salaam mafuta ni 3000+ basi jua hakuna kitu kitakaa stable everything now will be unstable kuanzia chakula,usafiri wa umma,school basi,Kila bidhaa sasa ni wakati wa serikali kuweka mkono mpaka chini.

Tusikae kwa kuangalia Uganda,Rwanda,Burundi wanauzaje mafuta hawa wote mafuta yanapita katika bandari zetu kwanini tufanye comparison? Kwani Serikali ikitoa baadhi ya kodi kwa kipindi hiki itakuwaje na ikabana matumizi yasiyokuwa ya lazima?

Haya ni maoni tu!
 
Sio kwa hawa kenge walio madarakani hawana uwajibikaji, madhali hili suala wao haliwaumizi, hawawezi kujiumiza kukusaidia wewe. Suaka hapa serikali ingebana bajeti, kupunguza matumizi yasiyo na msingi kisha kusaidia mwanachi wa kawaida, lakini nasema hawawezi, nasisitiza hawawezi abadani wa asilan.
 
Tuna wapinzani wa hovyo sana mana wakati huu ndio ulikua wakati wa kuwaunganisha watanzania badala ya kuhangaika na kupinga Royal tours.

Hivi Mtu anashindwa kutembea Kwa miguu kutoka Manzese mapaka Magomeni mapipa Tena asubuhi. Mtu anatoka saa kumi na Moja anasubiri gari mpaka saa Moja badala ya kutembea Kwa mguu umbali wa KM 3 kisa ni mjini . Ndio maana wanaongeza tozo mana wanajua mtanunua tuu.

Paki magari waone tamaa yao ya kuweka matozo hailipi. Wao wanaongeza magari ya kifahari na misafara na masafari na vikao na seminar halafu wanaweka tozo badala ya kufuta seminar ,magari ya kifahari, safari zisizo na umuhimu na vikao na makamati ya kipuuzi ya bunge na ujinga Mwingine huku wananchi wakionhezewa tozo na Bei za bidhaa kupanda.
 
Back
Top Bottom