Serikali ifanyie kazi tafiti za watalaam - Vibindo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ifanyie kazi tafiti za watalaam - Vibindo

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kamachumu Town, Jul 16, 2012.

 1. K

  Kamachumu Town Guest

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SERIKALI imetakiwa kuzifanyiakazi tafiti mbalimbali za kitalaam ili kuondoavikwazo vya biashara ambavyo vinachangia kwa kiasi kikubwa mfumuko wa bei hivyokuyafanya maisha ya wananchi wa kawaida kuwa magumu.

  Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti waShirikisho la Wafanyabiashara Ndogondogo (Vibindo), Gaston Kikuwi alisema hivisasa mfumuko wa bei unatisha na sababu kubwa inayochangia hali hiyo ni umemeusio wa uhakika na miundombinu duni ya barabara.

  Kikuwi alisema wakulima wanauza mazao yao kwa bei ya chini sana shambanilakini kutokana na uduni wa barabara wenye magari wanatoza bei kubwa yausafirishaji hivyo kuyafanya mazao kuuzaa kwa bei ya juu kwa walaji jamboambalo linachangia ugumu wa maisha.

  "Hata tafiti mbalimbali za benki ya dunia zinabainisha hivyo na uleuliozinduliwa hivi karibuni na taasisi ya BEST-AC unabainisha vitu kama ubovuwa barabara, ukosefu wa maji, umeme usio wa uhakika na vitendo vya rushwavinavyokwaza biashara na uwekezaji" alisema Kikuwi.

  Alisema Kikuwi kuwa utafiti wa miaka minne wa taasisi hiyo umebaini kuwahata maji ambayo awali hayakuwa kero katika biashara na uwekezaji siku zakaribuni yamekuwa tatizo kubwa ambalo linatishia ustawi wa biashara na uwekezajinchini.

  "Hivi sasa maji sio huduma tena ni biashara, wazalishaji wanalazimikakuyanunua katika malori ingawa mabomba wanayo viwandani kwao lakini hayatoihuduma" alisema na kuongeza kuwa mambo hayo na mengine yanaongeza gharamaza uzalishaji hivyo kuchangia mfumuko wa bei.

  Mkurugenzi wa Shirikisho la Wafanyabiashara Wenye Viwanda (CTI), alisemawakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo ya BEST-AC hivi karibuni kuwa serikaliinapaswa kuchukua hatua za makusudi kukabili hali hiyo ili kuleta nafuu katikasekta ya biashara nchini na kuzuia uwezekano wa kukimbiwa na wawekezaji.

  "Utafiti wa karibuni wa benki ya dunia unaitaja Tanzania kuwa ni mojakati ya maeneo magumu kuwekeza ukiacha hii ya Best-AC na wakati mwingitunashika nafasi za chini katika nchi ambazo zina mazingira rafiki kwabiashara" alisema Kilindu.
   
Loading...