Serikali ifanye uhakiki wa uraia katika sekta ya umma

Duterte

JF-Expert Member
Nov 19, 2016
1,062
1,127
Wasalaam wandugu,

Rejea kwenye kichwa cha habari hapo juu.

Kwa heshima na taadhima naiomba Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano iangalie hili suala ya Uraia katika sekta ya umma. Kama uhakiki wa vyeti feki umefanyika kwa mafanikio ni muda muafaka wa kulitupia jicho hili suala la URAIA.

Binafsi nimeshawahi kukutana na Raia wa nchi jirani wakifanya kazi katika mashirika ya umma kwa kufoji taarifa zao za URAIA. Asilimia kubwa huwa wanatumia majina Kama JOHN MICHAEL MARY ELIZABETH etc na kukwepa kutumia majina yao halisi Kama John Njoroge au Mary Jean-Pierre Nkurubwinza.

Naamini nia ya serikali kuisafisha sekta ya UMMA ni njema, ili kuweza kuwapatia ndugu zetu Watanzania wenye sifa na wanaostahili kulitumikia Taifa letu kikamilifu.

Nawakilisha hoja.

TANZANIA kwanza SIASA baadae.
 
Hujasikia kuwa NIDA wanazunguka katika sekta za umma?
Unadhani walikuwa wanafanya nini kama si kuhakiki uraia?
Wameshafanya tayari na waliothibitika tumepewa vitambulisho vya uraia.
Ile fomu ilipitia ofisi kama 5 hivi ikiwemo ofisi ya uhamiaji, serikali za mitaa, mwajiri, RITA na NIDA.
 
Na waliofoji URAIA wamechukuliwa hatua gani mkuu!?
 
Na waliofoji URAIA wamechukuliwa hatua gani mkuu!?
Ile fomu inapita katika ngazi tofauti, mimi nilichukulia ofisini, wengine waliichukua ofisi za serikali za mitaa, kwakuwa inakuwa inafuata chronological order hivyo ofisi moja inapitia taarifa za ofisi nyingine, mwisho kabisa NIDA hupitia taarifa zote wakiona kuna walakini unaitwa ukarekebishe taarifa pale ukijichanganya wakijua wewe si Mtanzania unapigwa pingu kama mtuhumiwa ,ukionekana innocent safi kama umedanganya unashtakiwa.
 
Shukrani kwa maelezo mkuu. Tukiweka pembeni UZANDIKI binafsi nafikiri Tanzania tuliyoililia wazalendo kwa muda mrefu imewadia.
 
Back
Top Bottom