Serikali ifanye nini ili uchumi wetu uipiku Kenya na mataifa yenye uchumi mkubwa kuliko sisi?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,503
2,046
Kama inavyojulikana ni kwamba Tanzania ina kila sababu ya kupiga hatua kiuchumi kutokana na mahali ilipo. Hata hivyo mimi nilitarajia baada ya kuachana na siasa za kijamaa huenda tungeanza kuyapiku kiuchumi mataifa mengi yanayotuzunguka na hata yaliyo mbali.

Ndipo najiuliza kama taifa tufanye nini kitusaidie kufikia haya matamanio yangu? Natamani sana siku moja Tanzania iongoze uchumi wa Africa.
 
CCM under MagufuliJP tulikuwa na speed ya hatari. Hata wao waliona kabisa speed yetu wakaanza chuki. Ila kwasasa na speed ya mama. Tusahau kabisa tutanyonywa. Mshindani wako unatakiwa kuweka urafiki wenu kwa akili ila sisi tumekwemda mazima. Tutapigwa hatari sana
 
Sasa kama wachumi wenyewe ndio hao kina mwigulu unategemea kuna hatua yoyote ya kupiga? Kiufupi wenzetu wamewekeza kwenye brain na sio hawa wapiga ramli na kuvaa scarf, hakuna capialist yoyote aliyeendelea bila shule belive me, ndio maana Bakhresa kasomesha watoto kwenye the best Universities duniani, angekua juha angeamini mali ni kama upendeleo tu zitajisimamia na kujiendesha zenyewe bila akili.
 
Tumchague Kagame kuwa Rais TZ. Ndani ya miaka 20 amefanya makubwa kwa Rwanda, akiwa Rais Tanzania ndani ya miaka mitano atafanya miujiza. Utani.

Kama kanchi kadogo hako kana tuuzia magari, kiwanda cha mobile phones, kakuza utalii, kaongeza elimu, afya, makazi kwa watu wake, technologia, mazingira mazuri ya biashara, uwekezaji, accomodation, usafi na usalama nchini kwake. Amezibiti urasimu, rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma, (Tax regime) kodi zinazoeleweka, zenye uhalisia, zinazochochea ukuzaji wa biashara na uwekezaji.

Imagine angefanyaje na resources zote za Tanzania ilizonazo zaidi ya mara mia moja ukilinganisha na Rwanda.

Gas, utalii, fukwe, bandari, mazao, rasilimali watu, madini, samaki, mifugo, ardhi, strategic location (tumezungukwa na nchi nane), vyanzo vya maji, Amani na utulivu.

Tunahitaji visionary and serious leaders.
 
... kwa CCM hii; hata umlete Malaika Jibril awe mwenyekiti wa chama na mkuu wa nchi nothing will happen; soon he will be corrupt as long as amezungukwa na majambazi yale yale ya miaka nenda miaka rudi mengine yamezeekea humo! Mbaya zaidi, wanarithisha nafasi zao kwa vizazi vyao na makuwadi wao wa kuwalinda for life! So, is a kind of vicious circle very difficulty to exit from!
 
Kama inavyojulikana ni kwamba Tanzania ina kila sababu ya kupiga hatua kiuchumi kutokana na mahali ilipo. Hata hivyo mimi nilitarajia baada ya kuachana na siasa za kijamaa huenda tungeanza kuyapiku kiuchumi mataifa mengi yanayotuzunguka na hata yaliyo mbali.

Ndipo najiuliza kama taifa tufanye nini kitusaidie kufikia haya matamanio yangu? Natamani sana siku moja Tanzania iongoze uchumi wa Africa.
Nasema hivi hilo haliwezekani kamwe!!nchi inayoongozwa na sifa za ukada wa chama ndio unaonekana una akili sana, na sio uwezo wa kiakili!!mtu mwenye uwezo lakini hana chama/yupo chama kingine ni marufuku kutoa mchango wake kwenye kujenga nchi!!
 
Kama inavyojulikana ni kwamba Tanzania ina kila sababu ya kupiga hatua kiuchumi kutokana na mahali ilipo. Hata hivyo mimi nilitarajia baada ya kuachana na siasa za kijamaa huenda tungeanza kuyapiku kiuchumi mataifa mengi yanayotuzunguka na hata yaliyo mbali.

Ndipo najiuliza kama taifa tufanye nini kitusaidie kufikia haya matamanio yangu? Natamani sana siku moja Tanzania iongoze uchumi wa Africa.
tukiacha kuweka politics kwenye kila kitu an interest binafsi labda tutasonga mbele
 
Kwanza tuwatoe warafi wa keki ya taifa serikalini. Amini nakuambia kuna watu wanakula mema ya hii nchi na ukiwaambia issue za kuachia ngazi, wapo tayari kuua na kukupoteza kabisa
 
Kama inavyojulikana ni kwamba Tanzania ina kila sababu ya kupiga hatua kiuchumi kutokana na mahali ilipo. Hata hivyo mimi nilitarajia baada ya kuachana na siasa za kijamaa huenda tungeanza kuyapiku kiuchumi mataifa mengi yanayotuzunguka na hata yaliyo mbali.

Ndipo najiuliza kama taifa tufanye nini kitusaidie kufikia haya matamanio yangu? Natamani sana siku moja Tanzania iongoze uchumi wa Africa.
Angalia %ya access to electricity
IMG-20210724-WA0031.jpg
 
Back
Top Bottom