Serikali ifanye kazi kwa kufuata utaratibu sahihi na si kufata itikadi ama imani fulani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ifanye kazi kwa kufuata utaratibu sahihi na si kufata itikadi ama imani fulani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lyimo, Oct 18, 2012.

 1. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Imefikia wakati sasa hii serikali yetu tunayosema sikivu iwe inatekeleza majukumu yake kwa uhalisia na kuachana na mambo ya propaganda. Swala la kupandikiziana chuki za kidini limechochewa pia na serikali hii iliyopo madarakani ili tu Chama tawala kufanikisha kushika dola.

  Tumeshuhudia wanasiasa wakinadi vyama vyao kwa kusema hawa wanafata mfumo wa dini hii wakati si kweli, kumbe walikuwa wanapanda mbegu ambayo hawataweza kudhibiti mavuno yake. Tulishuhudia propaganda ya kuingiza majambia na IGP Mahita hata kuonyesha kwenye TV na kusema ni wameyakamata kutoka kwenye makontena waliyoagiza CUF kwaajili ya kuleta machafuko wakati wa uchaguzi, wakati huo CUF ilikuwa na nguvu kiasi cha kuleta hofu kwa CCM kuweza kuendelea kujitwalia dola.

  Baada ya hapo hatukushuhudia kiongozi ama mwanachama yeyote wa CUF aliyehukumiwa kwa hilo wala kushtakiwa (Kumbe ilikuwa propaganda tu ambayo iliweza kuwaogofya watu na kuipigia kura CCM). Tumeshuhudia swala la DC Igunga lilivyogeuzwa la kidini ili kufanya chama kingine kichukiwe na kundi fulani, kumbe chuki ile haikuishia igunga tu.

  Tumeshuhudia majengo ya ibada yakitangaza tumchague fulani kwasababu kadha wa kadha ambazo ni za kidini, lakini Serikali hii sikivu na wanausalama wake hawakuona kuwa hilo litakuja kuwa tatizo. Kwasasa tuna vyombo vya habari vinavyopandikiza chuki za kidini waziwazi, ila hakuna hatua yoyote iliyofanyika kuvidhibiti. Mifano hai ipo mingi ila kwasasa haitusaidii tena maana imepigiwa kelele za kutosha pasipo hatua zozote kuchukuliwa.

  Swala Jumuia ya Uamsho na mihadhara ya Kiislamu lilishapigiwa kelele siku nyingi kwa kuonekana kinatoka nje ya majukumu yake na kuingilia kazi zilizopaswa kufanywa na wanasiasa huku ikipandikiza chuki. Ilifikia wakati hata Katibu Mwenezi wa CCM Taifa Ndugu Nape NNauye alipendekeza jumuia hii ifutwe na mrajisi wa serikali ya Zanzibar kwani kuwepo kwake kunahatarisha amani na umoja wa kitaifa, ila swala hili lilipokelewa kwa mtizamo tofauti sana.

  Sasa hali imeshakuwa si ya kuweza kuidhibiti kirahisi ndiyo serikali inastuka, imechelewa sana kwani kurejesha amani haitakuwa kazi ndogo tena. Tumepiga kelele sana kuhusu uchochezi unaopandikizwa na radio IMAAN, ila serikali sikivu imeziba masikio. Pale madhara yatakapokuwa hayawezekani kudhibitiwa ndiyo itastuka.

  Tunaomba serikali na vyombo vya usalama mtekeleze majukumu yenu kwa kufuata sheria na kanuni zinazoongoza nchi, na tuache kuweka mbele mambo ya itikadi zetu ama imani zetu. Vilevile tunaomba vyombo vya usalama viache kutumika na vyama vya siasa kwani sasa imedhiirika kuwa madhara yake ni makubwa na yanachangia si tu kuhatarisha amani bali pia kudhorotesha maendeleo ya Taifa letu.
   
Loading...