mserekale
Member
- Jul 4, 2019
- 79
- 103
Kutokana na wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana ni vyema serikali ikafanya mikakati ya makusudi kukabiliana na hili tatizo.
Haya ni mawazo yangu binafsi kuhusu nini kifanyike;
1. Kudhibiti bidhaa za nje(massive importation of goods).Bidhaa za nje kwa kiasi fulani zinachangia kuua soko la ndani hivyo kuwakosesha vijana wetu ajira na fursa za kujiingizia kipato.
Katika hili serikali ni vyema ikaweka mikakati madhubuti ya kudhibiti bidhaa zinazotoka nje ya nchi ambazo zinawezekana kutengenezwa hapa nchini kwetu kwa mfano bidhaa za samani(furnitures) kama vile makabati, viti vya kukalia, masofa n.k
Kwa kufanya hivyo itasaidia kuinua soko la ndani na vijana wetu watahamasika kujiajiri kwenye shughuli hizo za mikono.
2. Kuongeza fursa na nafasi za ajira serikalini. Kuna haja ya serikali kuwaajiri vijana ili walitumikie Taifa katika sekta ambazo zina upungufu wa watumishi ambao unaweza kuchangiwa na masuala ya kustaafu, vifo, kufukuzwa kazi ama upungufu wa wataalamu katika sekta husika.
3. Vijana wapewe elimu ya kilimo, biashara na ujasiriamali. Kuna haja ya serikali kuanzisha masomo ya kilimo, ujasiriamali na biashara mashuleni kama masomo ya ziada ili elimu watakayoipata kwenye masomo hayo iwasaidie kujiajiri nje na taaluma walizosomea.
4. Serikali ifanye jitihada ya kuwekeza katika viwanda vya kusindika mazao na matunda ili vijana wajiajiri kwenye sekta ya kilimo.
5. Serikali ifanye jitihada za kutafuta masoko ya wakulima ili vijana watakaojiajiri kwenye kilimo wapate sehemu ya kuuza mazao yao.
Kama kutakuwa na mawazo mengine tofauti na haya naomba tuyashirikishe katika uzi huu lengo likiwa ni kuisaidia serikali kukabiliana na changamoto ya ajira kwa vijana.
Asanteni na karibuni kwa mawazo zaidi juu ya nini kifanyike.