Serikali idhibiti uoneshaji wa video kwenye mabus ya abiria

Ng'oa tv zote tupia usb charger na wi-fi kila mtu afaidi kimpango wake sasa mimi unaniwekea bongo movie yaani ikianza tu bora niangalie shamba la mkonge nje huko
 
Juzi natoka Bukoba kwenye basi la Complex imewekwa muvi naona vipigo mtu anapikwa hadi wanamnyofoa figo, maini, utumbo na damu inasambaa pwaaaa! Mbele yangu alikuwepo abiria na vitoto vya kati ya miaka 4 na 6...hiki kidogo kiliangua kilio kabisa, miliumizwa sana na kitendo hiki! Jamani sumatra tuondolee huu upuuzi!
 
Ungemwambia konda atoe aweke picha nzuri lakini pia kila mtu ana mapenzi yake humo ndani ya gari wapo wanaozipenda tuu hata mtu ambae hajawah ona tv ataburudika vilivyo.
 
Katika kipindi cha mwezi huu nimekuwa na safari nyingi za kutembelea mikoa mbali mbali (route ya Dar to Morogoro, route ya Arusha to Dar, route ya Mwanza to Dar, route ya Dar to Tanga etc).

Kitu kimoja kilichonisitua ni uoneshaji holela wa video show kwenye mabus bila kuzingatia maadili ya nchi yetu. Sinema zenye kuonesha mambo ya mapenzi na ngono na zile zenye kuonesha mauaji ya kutisha zinaoneshwa holela tu bila kujali tofauti za umri wa abiria.

Kuna abiria wanaokuwa wanasafiri na watoto wadogo au na watoto wao wakubwa au wakwe. Kwenye baadhi ya mabus, wameenda hatua mbele zaidi, wanao esha sinema kutoka west africa zilizoondolewa sauti za lugha ya kiingereza na kuwekewa sauti zao kwa kiswahili, sinema hizi zinahamasiaha ngono. Sinema hizi ni aibu tupu.

Naiomba serikali ifuatilie jambo hili, hizi video za kwenye mabus ni aibu tupu!
Kwa uzoefu wangu wa kusafiri na mabasi fanya hivi,

Ukiwa na route ya Moshi, Arusha to Nairobi basi panda Tahmeed luxury 2×1 Free wi-fi kila siti na screen yake usisahau tu headphone zako.

Dar to Dodoma panda Kimbinyiko au Shabiby luxury na Dar to Tanga Tahmeed pia wapo.

Ukiweza kumentain kupanda mabasi ya aina hii utapunguza kero kwani hata zile public screen huwa zinawekwa movie za Hollywood za ukweli.

Nilikuwaga sielewi ni kwa nini kuna binadamu kila aendapo yeye ni VIP treatment lakini sasa hivi naelewa maana yake.

Fanyia kazi ushauri wangu utaufurahia usafiri wa bus.
 
Ni nyie mnaosafiri na luxury bus, mi nikija dar napandaga mwenyewe fuso za makebich na miwa, labda niangalie konokono, nikirud bus ninalopanda hata kama lingekua na hzo video hutaona hata kitu, likiingia kwenye shimo au tuta lazma uende juu mpk kwenye roof ukirud kiti kishapata mtu au kimehama upo chini. Viti vyote ni mobile Yan unatoka dar umekaa nyuma ukifka lushoto upo kwa dereva.
 
Hizo movie zao ni chanzo kikuu cha kuharibu maadili ikiwezekana waondoe hata TV zenyewe kuliko kutuharibia watoto na kutuvunjia heshima na tunaosafiri nao.
 
Yaan mie wanachonikera ni kuweka Bongo movie tu, huwa nakereka sana tena unakuta wanazo mbili kila zikiisha zinajirudia,

Nyambaff kabisa kuna siku nikamwambia konda kama huna kitu cha kuonesha zima screen Nashukuru kuna abiria waliniunga mkono!
 
Kunawapumbavu flan bus flan, route flan walichomeka kiflash chao kumbu kina porn humo humo iliwekwa kimakosa, mara paap!! huwez amin nlkuwa nasafiri na mama, nilikwazika sn, hata msamaha hawakuomba,
Kama sijakosea ni basi la kwenda Mtwara. Mm nilimfuata dereva baada ya kufika akaniambia eti flash ziko mbili zinafanana. Ila abiria walikwazika
 
Nakuunga mkono kbs nakumbuka mwezi wa nane nilitoka Moshi tu dar nikapanda bus moja hivi jamaniiii jamanii nilikaa na baba mmoja kwenye siti mpk nilikuwa naogopa hata kumuangali, coz ni mzee wa makamo na zile picha walizokuwa wanazioneshaa mh?!!! Langu rohoni
 
Umeongea bongee la point aseee....lakini pia mle wanapanda watumishi wa Mungu na watu wa rika mbalimbali...kweli huwa inakera sanaaa
 
Moja ya kero yangu kwenye mabasi ya kisasa ni hizo movie na muziki duh sijawahi kufurahia naona zengwe tupu,nilipanda bus toka Mbeya—Dar utadhani ni niko kwenye kigango cha kanisa fulani ni Bahati Bukuku,Rose Mhando,Nyuki ikabidi nimuambie konda ananikera kama vipi azime tu sio wote tunapenda ayo manyimbo.
 
Wanafanya makusudi ili kuwazuga abiria Kwamba dereva anapokuwa Kwenye mwendo kasi abiria wasistukie na kumuonya Au kumkemea!
Yani Siku hizi ndo mtindo wao wanaweka tv tena kwa sauti kubwa kabisa Kama basi lililobeba wahuni wanaoenda picknick !
Lengo Lao ni kutaka kuwafanya abiria wazongatie kuangalia tv badala ya mwendo wa usalama wa dereva!
Sumatra wanatakiwa kutoa zuio kabisa !
 
Katika kipindi cha mwezi huu nimekuwa na safari nyingi za kutembelea mikoa mbali mbali (route ya Dar to Morogoro, route ya Arusha to Dar, route ya Mwanza to Dar, route ya Dar to Tanga etc).

Kitu kimoja kilichonisitua ni uoneshaji holela wa video show kwenye mabus bila kuzingatia maadili ya nchi yetu. Sinema zenye kuonesha mambo ya mapenzi na ngono na zile zenye kuonesha mauaji ya kutisha zinaoneshwa holela tu bila kujali tofauti za umri wa abiria.

Kuna abiria wanaokuwa wanasafiri na watoto wadogo au na watoto wao wakubwa au wakwe. Kwenye baadhi ya mabus, wameenda hatua mbele zaidi, wanao esha sinema kutoka west africa zilizoondolewa sauti za lugha ya kiingereza na kuwekewa sauti zao kwa kiswahili, sinema hizi zinahamasiaha ngono. Sinema hizi ni aibu tupu.

Naiomba serikali ifuatilie jambo hili, hizi video za kwenye mabus ni aibu tupu!

Hayo maadili ya nchi yenu yameandikwa wapi?
 
AISEE POVU MLIOMWAGA HAPA SI LA NCHI HII,, WENYE MABUS WAJE KUZOA POVU LAO
 
Watu wengi hapa naona wamelalia upande mmoja kwamba zile video si nzur Mara zinaboa n.k ila navoona walioweka TV hawana nia mbaya na Watu actually wanayaka entertainment sasa unakuta MTU Hana simu wala chchte at least hio screen inampa entertainment walau aburudike in short asiboreke sasa Kama MTU unaona shida the best way usiangalie tu waache ambao wako interested na hivo vitu,, japo si support uonyeshwaji wa X,, na kngne wakisema mchague cha kuangalia mabishano yake hayatoisha Hata Kama mnatoka dar to mwanza
 
Back
Top Bottom