Serikali: Idadi ya wagonjwa wa Corona nchini Tanzania imeongezeka na kufikia Sita(6)

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Wagonjwa wa Corona wafika 3 sasa Tanzania baada ya wawili zaidi kupatikana leo na mmoja kutoka Zanzibar.

Waziri mkuu Majaliwa athibitisha kwa kusema “Tuna ongezeko la wagonjwa wawili ambao wamethibitika kuwa na Corona Tanzania, mmoja kutoka Zanzibar yeye ni Mjerumani ana miaka 24 na tayari yupo kwenye uangalizi, na hapa DSM tuna Mmarekani mwenye miaka 61 amebainika kuwa na Corona pia”

Pia soma> Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza

=====

Watu 2 kutoka Zanzibar na Dar wenye asili ya Kijerumani, Kimarekani wagundulika na virusi vya Corona Dar na Zanzibar, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atangaza asubuhi hii. Asema shughuli za usafiri, maduka ziendelee ila elimu izidi kutolewa

" Dar es salaam kapatikana mmarekani mmoja wa miaka 61 na zanzibar kapatikana mjerumani mmoja"

=========


UPDATES : 19 MARCH 2020

#CORONAVIRUS: WAGONJWA TANZANIA WAFIKIA 6

Wagonjwa wawili wametangazwa leo na wote wamepatikana Jijini Dar

Mmoja Mwanaume (40), Mtanzania, aliyesafiri katika Uswizi, Denmark na Ufaransa

Mwingine Mwanaume (40), Mtanzania, aliyesafiri katika nchi ya Afrika Kusini

IMG-20200319-WA0031.jpg

Moja ya wagonjwa wa leo ni Mwana FA na Meneja wa Diamond.​
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametangaza ongezeko la wagonjwa wawili wa virusi vya corona Tanzania mmoja amekutwa Zanzibar na mmoja Dar es Salaam wote ni raia wa kigeni. Jumla wamefikia watatu.

“Tuna ongezeko la wagonjwa wawili ambao wamethibitika kuwa na corona Tanzania, mmoja kutoka Zanzibar yeye ni Mjerumani ana miaka 24 na tayari yupo kwenye uangalizi, na hapa DSM tuna Mmarekani mwenye miaka 61 amebainika kuwa na corona pia” - MAJALIWA
 
Back
Top Bottom