Ncha Kali
JF-Expert Member
- Sep 19, 2019
- 14,497
- 26,986
Ndugu zangu!
Kwa masikitiko makubwa, nimepokea taarifa hizi kutoka kwa mdogo wangu, mmoja wa wahanga.
Kaitwa ofisi ya msajili na kufahamishwa kuwa anatakiwa kuondoka mara moja chuoni hapo, kwamba kuna waraka umetoka TCU kwa kile kilichoitwa hakuwa amekidhi sifa za kudahiliwa katika ngazi ya shahada kwenye chuo/kozi hiyo.
Ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza, semista ya pili sasa na ni mnufaika wa bodi ya mikopo. Ni ajabu kusikia kuwa kote huko na muda wote huo walijiridhisha na sifa zake, na mkopo amekuwa akipata tangu aanze masomo yake!
Kama mzazi nimeshindwa kuelewa hili na nimechukulia kama ‘uonevu’ kwa wanafunzi. Mbaya zaidi ‘anayewafukuza’ hatoi maelekezo ya kutosha zaidi ya kile anachokiita ni maelekezo kutoka TCU kwamba amepokea majina hayo kutoka huko.
Ombi langu kwa serikali kupitia TCU, wapitie upya uamuzi huu ili kujiridhisha na sifa za kila mwanafunzi.
Mmoja huyu ninayemfahamu ni mimi ndiye nilihusika kumwelekeza namna ya kufanya maombi ya kujiunga na Chuo, kila kozi ilikuwa na vigezo vya kutimiza (cutoff points, sifa zote zimeainishwa kwenye guidebook ya TCU).
Bila kufikia pointi husika mfumo wenyewe uliweza kugoma automatically, kijana huyu alitimiza kila kilichohitajika!
Hii sasa ni kitu gani?
Nini kimebadilika, watoto wasionewe, haki itendeke.
Wasalaam;
Ncha Kali.