SoC02 Serikali ichukue hatua, Tunalishwa sumu kwenye vyakula tunavyotumia kwa kutokujua

Stories of Change - 2022 Competition

SOVIET UNION

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
455
1,283
Katika vitu ambavyo nchi nyingi wanakuwa makini navyo basi ni Ubora wa chakula wanacholishwa raia wao. Ndo maana suala la ku-export vyakula je ya nchi ni suala moja gumu sana, hasa kwenye ku-meet ubora wanaotaka.

Serikali yetu bado suala la ubora wa vyakula wanavyolishwa Watanzania ni la siasa. Katika vitu ambavyo vingetangazwa kwenye Gazeti la Serikali kwamba havipaswi kufanyiwa siasa ni suala la Afya za Watanzania.

Tumekuwa tunalishwa sana sumu si kwa vyakula kutoka nje ya nchi, hapana ni vyakula tunavyolima wenyewe sisi Watanzania Wazalendo, tunalishana sana sumu kwa makusudi na kwa kutokujua.

Tunalishwa sana sumu kupitia vyakula hivi:

1. Mayai tunayo kula mtaan:
Je, ni nani anafanya ufuafiliaji kujua kwamba mayai yanakidhi viwango na hayana shida? Wafugaji wengi wanatumia sana antibiotics kwenye kutibu kuku wao, na Dawa nyingi za antibiotics zina kitu kinaitwa EGGS WITHDRAW PERIOD, kwamba kipindi unawapatia kuku wako dawa yale mayai wanayotaga yanapaswa kutupwa, Sasa je ni nani mfugaji ana kuku wake 1000 anakusanya trei 27 kila siku na kweli akachome moto trei zake 27 na kwa muda wa siku 3 au 5 au wiki, ni nani? Yale mayai yanakuwa na vimelea vya dawa ndo maana ikashauriwa yasitumike kwa binadamu lakini nani anafanya hivyo? Anyooshe mkono, Tunalishwa sana sumu.

2. Kuku wa nyama, hawa pia hawapitwi mbali na madawa wanapewa sana madawa na kuna mfugaji akiona mafua yamezidi kwa kuku wake wa Broiler anawapa dawa siku 2, siku ya tatu wanachinjwa wakauzwe na kuku still wanakuwa na vimelea vya dawa. Nani kweli aache kwenda kuuza kuku wake kisa wako kwemye dozi?

3. Matunda na Mbogamboga: Hapa ndo kubaya zaidi, hizi mboga zinapigwa sana madawa na mbaya zaidi mkulima anapiga dawa leo na kesho yake anazichuma kupeleka sokoni, na Watanzania bila kujua unaenda kununua kumbe unaunua sumu, Matunda hasa tikitiki maji na Tango zinapigwa mno madawa. Je, kuna anayezingatia? Nyanya zinapigwa mno madawa na mkulima anaweza piga dawa leo na kesho kutwa nyanya zikachumwa na kuingizwa sokoni. Pia hapa kuna suala la Mbolea, mboga zinapigwa over mbolea na hakuna anayejali.

4. Nyama tunazokula hasa za Ng'ombe ubora unazingatiwa? Zile Ng'ombe zinazokufa ndani ya Malori huwa zinateketezwa kwa moto? au huchinjwa usiku wa manane na kuingizwa mtaani? nani anafuatilia?

5. Nafaka kama mahindi huwa yanahifadhiwa kwa dawa, na mara nyingi mtu anayekuja kununua anaenda anapepeta tu na kwenda kusaga na ndio maana hapa inashauriwa mtu asile Dona, labda uandae mwenyewe nyumbani kwako kwa kuosha yale mahindi tofauti na hapo unakula sumu.

Kama ni mteja wa matunda kutoka nje ya nchi utaona yana lebo ya kusaidia kutrack na kujua hili chungwa ni kutoka shamba la fulani, Sisi hatuna hicho kitu, kuku watu wanawachinjia majumbani kwao na wateja wanaenda kuchukulia huko huko na hakuna mkaguzi wa kukagua hao kuku kabla hawajachukuliwa kupelekwa sokoni.

Mayai yanaenda kuchukuliwa bandani na moja kwa moja kwa walaji nani ana sample kujua kama yanafaa kwa kuliwa? Zile Mboga za majani zinapimwa? jibu ni hapana.

Serikali ikiendelea kuchukulia kila kitu ni siasa na kuwa entertain wanyonge basi tutakuwa hatarini sana.

Serikali katika kitu ambacho haipaswi kuonea mtu haya ni suala la afya hasa ubora wa vyakula vinavyouzwa masokoni.

Si bure nowadays unakuta mtoto mdogo figo zimefeli, mtoto mdogo ana cancer, mtu mwili hau-respond dawa. Mwili unakuwa sugu dhidi ya dawa hasa antibiotics.


Serikali Ifanye nini?

Serikali inapaswa kuchukua hatua hasa kwa mifugo inayochinjiwa majumbani na kupelekwa sokoni, na kuwe na Sheria na utaratibu wa kupima vyakula ambavyo vinakuwa sokoni tiyari na pale inapogundulika kuwa na sumu basi muuzaji awajibiswe.

Pia vyakula visiingie sokoni bila kuwa vimechukuliwa sample na kupimwa kama vinafaa kwa matumizi au la.

Kuwe na lebo za kutambua matunda na mboga ni za kutoka kwenye shamba la nani, hii ni pamoja na mayai.

Na Sisi Watanzania kama una nafasi basi zalisha baadhi ya vyakula vyako mwenyewe hata kwa 40%, hii inaweza kukusaidia kiasi fulani. Vyakula ya sokoni sio salama kwa sababu ya usambazaji holela ambapo hakuna mamlaka ya kukagua kabla ya kuingizwa sokoni.

IMG-20220710-WA0026.jpg

Picha: Kutoka gazeti la Daily National Kenya
 
Basi acha kula chakula.

Kila kitu kina madhara
Kula vizuri
Fanya mazoezi
Mkumbuke muumba wako
 
Basi acha kula chakula.

Kila kitu kina madhara
Kula vizuri
Fanya mazoezi
Mkumbuke muumba wako
Madhara yanatakiwa kupunguzwa au hili nalo linahitaji hisani ya Watu wa Marekani? Sio kuacha kula ni hatua zichukuliwe, Haya mambo Impact zake ni za baadae, Kuna siku utakumbuka hiili andiko
 
Basi acha kula chakula.

Kila kitu kina madhara
Kula vizuri
Fanya mazoezi
Mkumbuke muumba wako
Mungu kwenye vitu vya makusudi huwa hayupo hapo, yaani ujilishe sumu makusudi then useme kumkumbuka Mungu wako?
 
Umegusia mambo ya msingi msana mkuu,unapozungumzia chakula unazungumzia Uhai, ni andiko zuri Sana limegusia Nyanja muhimu ktk Maisha ya mwanadamu,ingawa utekelezaji wake naona ni mgumu Kwa hizi inchi zetu za Africa.

Lakini kila kitu kinawezekana tukiamua kuweka Nia ya dhati,hakuna kitu kinacho shindikana Chini ya jua.

Nakupa kongole mkuu .
 
Umegusia mambo ya msingi msana mkuu,unapozungumzia chakula unazungumzia Uhai, ni andiko zuri Sana limegusia Nyanja muhimu ktk Maisha ya mwanadamu,ingawa utekelezaji wake naona ni mgumu Kwa hizi inchi zetu za Africa.

Lakini kila kitu kinawezekana tukiamua kuweka Nia ya dhati,hakuna kitu kinacho shindikana Chini ya jua.

Nakupa kongole mkuu .
Watu wengi hatujali kama kawaida yetu, ishu kama hii ni hadi tupate Msaada au tuwe tunatangaziwe kwenye TV waafrica tuna matatizo sana, Sumu tunazo jua ni zile kama za panya za kuua dakika hio hio. Ila vyakula tunavyo kula vingi havifai vina eitjer madawa kwa wingi au mbolea ilio pitiliza.
 
Back
Top Bottom