Serikali ibadili sera ya ajira kwa INGO's

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,824
2,381
Kenya waliamua kubadili sera ya ajira na kushinikiza mashirika ya Kimataifa yaajiri kwanza wazawa kabla ya kuanza kufikiria watu wa nje. Nchi hiyo ilijikuta ina wakimbizi wakihudumiwa na wageni, ina mashirika ya fedha ya Kimataifa yakiajiri wageni nk.

Baada ya kuona hilo ni tatizo ikaamua na kusimamia sera ya kuajiri kwamba Wakenya wapewe kipaumbele na kutishia kufunga mashirika yasiyofuata utaratibu huo.

Leo hii mitandao mingi ikitangaza nafasi za kazi kwenye mashirika hayo huandika locals only lakini kwa Tanzania hawaweki hizo specifications.

Huko makambini na mijini haya mashirika yamejaza wageni watupu. Serikali lazima ije na sera na isimamie hali hii, si tu kwenye mashirika bali makampuni na viwanda.
 
Wazo zuri, pole ushauri wangu tu vijana wakitanzania inabidi tuondokane na woga wakutafuta nchi za wenzetu
 
Tatizo letu Tanzania sio hiyo Sera inayoongoza INGOs hapa tatizo ni sisi watanzania ktk suala zima la Management tumefeli.

Nakumbuka miaka ya nyuma ni sisi wenyewe tulioua mashirika yetu ya Umma kwa kuwa na very poor management mpaka tumeingiza Sera ya ubinafisishaji.

Nidhamu yetu ktk management iko chini sana na hakuna tajiri yoyote atakubali pesa ichezewe tu na management members.
 
Back
Top Bottom