SoC02 Serikali ianzishe Shirika la Umma la Usafirishaji wa abiria kwa njia ya barabara mikoani

Stories of Change - 2022 Competition

Bushmaster

JF-Expert Member
Jan 18, 2022
479
974
  • Usafirishaji ni kitendo cha kutoa bidhaa au kupeleka watu kutoka sehemu moja hadi nyingine, kitendo hicho kinaweza kufanywa kwa kutumia njia mbalimbali za usafiri( mode of transport) kama kwa njia ya maji,barabara,reli, na anga
  • Usafirishaji ndio tendo pekee ambalo humaliza machakato mzima wa uzalishaji, kwa sababu hukutanisha soko na bidhaa kwa pamoja ( watu (soko) hufuata bidhaa au bidhaa hufuata soko kwa kutumia usafiri)
Kwa miaka mingi usafirishaji wa abiria kwa umma kwa umekua ukifanywa na shirika la reli Tanzania (TRC) ambapo watu na mizigo wamekua wakisafirishwa katika maeneo yote ambayo reli imepita.​
Ambapo mwaka 1948 shirika la reli la Afrika Mashariki lilianzishwa na kuitwa Shirika la reli na Bandari za Afrika mashariki (EAR&H).​
Baada ya kuvunjika kwa Afrika ya Mashariki,shirika la reli la Tanzania lilipewa jukumu la kusimamia usafirishaji kwa njia ya reli (railway transport services), usafirishaji kwa njia ya Maji ( Marine transport services) na usafirishaji kwa njia ya barabara ( road transport services)​
Mwaka 1990 sera ya ubinafsishaji ilipoanzishwa shirika la reli la Tanzania lilibinafsishwa kwa shirika la reli la India RITES,pamoja na majukumu yake yote yakawa chini ya mashirika binafsi ikiwemo usafirishaji wa abiria kwa njia ya barabara ( road tarnsport services)​
Mwaka 2011 shirika la reli la Tanzania lilichukuliwa tena na serikali,kwa jukumu la usafirishaji wa abiria na mizigo kwa njia ya reli,huku usafirishaji wa abiria na mizigo kwa njia ya barabara ukibaki kwa watu na mashirika binafsi. ( source website trc)​
trc1.jpg
source:google
Mwaka 2014 UDART ilianzishwa kutoka shirika la usafirishaji la Mkoa wa Dar Es Salaam (UDA),likiwa kama shirika la umma linatoa huduma ya usafiridhaji wa abiria katika mkoa wa Dar Es Salaam na maeneo jirani

UDART limekua likijiendesha kwa mafanikio makubwa sana,ambapo mwaka 2017 UDART ilishinda tuzo kama mradi bora na endelevu wa usafirishaji (THE BEST SUSTANAIBLE TRANSPORTATION PROJECT) na kuifanya Tanzania kua nchi ya kwanza ya kiafrika kushinda tuzo hii.

udart award
udarts2.jpg

(source: www.udart.co.tz)

Kuna haja sasa serikali ikaanzisha shirika la umma la usafirishaji wa abiria kwa njia ya barabara (Tanzania Road transport Corporation-TARTCO au Tanzania Road transport service-TARTS) hadi mikoani
Kupatikana kwa shirika la umma la usafirishaji wa abira kwa njia ya barabara kama ilivyo katika usafirishaji wa njia ya anga,kutakua na faida nyingi kama ifuatavyo:-
  • Uhakika wa usafiri, (Reliability) huduma za usafiri hasa mkoa hadi mkoa kwa sasa sio za uhakika,kuna baadhi ya njia au routes zinakua na huduma za usafiri kwa kipindi fulani pekee,hicho kipindi kikipita usafiri unakata mfano routes za MWANZA-MBEYA,TABORA-MBEYA,lakini kama kutapatika kwa shirika la umma la usafirishaji wa abiria kwa njia ya barabara ni wazi changamoto hiyo itapungua.
  • Kuwafikia wengi ( Accessibility) kutokana na kua maneneo mengi yanakosa huduma za usafiri au usafiri kua wa msimu,ni dhairi kua endapo shirika hili litaanzishwa basi huduma hii ya usafiri itawafikia wengi.
  • Itazuia Upandishaji wa nauli kiholela,ni wazi kwamba katika kipindi hiki nauli za usafiri zimepanda kwa sababu ya kupanda kwa mafuta ni wazi pia kipindi cha mwisho wa mwaka nauli zitapanda zaidi,lakini kupatikana kwa shirika la umma la usafirishaji abiria kwa njia ya barabara tatizo la upandhishaji wa nauli kiholela linaweza kukoma
  • Kukuza Soko la bidhaa nchini,ni wazi kwamba usafirishaji ndio kikomo cha mchakato mzima wa uzalishaji, ambapo bidhaa itafika sokoni ama itamfikia mlaji au Mlaji ataifuta bidhaa huko ilipo, hivyo kupatikana kwa shirika la usafirishaji kwa njia ya barabara ni wazi kua soko la bidhaa mbali mbali nchini litakua na uchumi utakua pia.
  • Ajira, kuwepo kwa shirika la umma la usafirishaji abiria kwa njia ya barabara,itaongeza ajira kwa wananchi,ambapo watu mbali mbali wataajiriwa mfano, madereva,wakatishaji tiketi,n.k hivyo kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
  • Ufanyikaji wa tafiti (Research) za usalama barabarani, kwa sasa tafiti nyingi za usalama barabarani zinafanyika kupitia magari au mashirika ya watu binafsi, mfano tafiti za electronic ticket,ving'amuzi,ambapo wamiliki wa mashirika hayo wanazuia kwa makusudi malengo yaliyokusudiwa ( pre determined goals) ili kuzuia mabadiliko katika sekta ya usafirishaji, wanafanya hivyo ili kuendelea kuapata faida kubwa kuliko ubora wa huduma wanayotoa, lakini kupatikana kwa shirika la umma la usafirishaji kutawezesha tafiti hizo kufanyika na kuleta malengo yaliyokusudiwa.
  • Kupunguza gharama za usafiri,kupatikana kwa shirika la umma la usafirishaji ni dhairi kabisa gharama za usafiri mikoani zitapangua,kama jinsi UDART ilivyopunguza gharama za usafiri ndani ya mkoa wa Dar Es Salaam,lakini pia shirika litaongeza ushindani katika sekta nzima ya usafirishaji,maana kadri huduma au bidhaa inavyopatikana kwa wingi hata bei yake hupungua,na vile vile huduma (bidhaa) ikipatikana kwa uchache bei ya bidhaa hiyo itapanda,hivyo kupatikana kwa shirika la umma la usafirishaji bei ya usafiri itapungua na kuongeza ushindani katika sekta ya usafirishaji abiria kwa njia ya barabara.
  • Kukuza pato la taifa,kupitia usafirishaji serikali itaweza kupata mapato ambayo yatasaidia kupeleka huduma kwenye sekta nyingine,mfano afya,elimu,umeme,ulinzi n.k. kuongezeka kwa pato la taifa serikali itaweza kutatua pia changamoto mbalimbali ambazo zinatokana na kipato duni mfano umasikini ambao unasababishwa na ukosefu wa barabara bora za kupitisha mazao kwenda kwenye soko, vile vile umasikini ambao unasababishwa na ukosefu wa elimu au fikra bora,serikali itaweza kuwekeza katika elimu na hatimae umasikini wa namna hiyo utaondoka.
Ahsanteni,

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom