Serikali ianzishe ligi ya timu za mikoa (football academy kwenye kila mkoa)

lloydsam

Member
Nov 8, 2015
42
55
Binafsi nimekuwa na wazo hili kwa kipindi kirefu sana, na nina imani suala hili litasaidia kukuza fani ya michezo hapa nchi na hata kuongeza pato la Taifa.

KWANZA KABISA
• Serikali itoe tamko la kuanzishwa kwa Timu ya mkoa Mf. Kilimanjaro FC, Dar City, Moro FC, Mbeya City, Dodoma FC, Arusha FC n.k

PILI
• Serikali iwape maeneo timu hizi za ili ziweze kujenga Viwanja vyao vya Mpira, pia wapewe sehemu ya reserve maeneo hayo hayo kwa ajili ya kuja kujenga viwanja vingine vya michezo mbalimbali siku za usoni kama vile Viwanja vya basketball & Netball, Swimming Pools, Futsal na Boxing Stadium..

KILA MKOA
• Uanze kutenga fungu la michezo kila mwezi ikusanyapo mapato yake, Pesa zitakazotumika kubusti ujenzi wa kiwanja cha mpira ili kianze kukusanya viingilio na kuendelea kujitegemea..

Kadri timu itakavyokuwa inafanya vizuri, itazidi kujikusanyia mashabiki zaidi Mkoani mwake na kupata support kubwa kutoka kwa Wanachi wake kwa kuuza jezi na kuuza zaidi Ticket wakati wa mechi haswa watakapokuwa wanacheza na timu itakayokuwa inafanya vizuri wakati huo..

Pesa zitakazokuwa zinakusanywa na Viwanja hizi, ndo zitakazokuwa zinatumika kuwalipa Wachezaji, Makocha na Wote watakaokuwa wanahusika na Timu hiyo ya mkoa.. Na ikitokea watakuwa wanakusanya pesa nyingi basi waanze kusajili makocha wa kimataifa ili wachezaji wao wawe katika levo ya Kimataifa, hususani na kununua Vifaa vya kisasa kabisa vya mazoezi kwa ajili ya Timu yao.

KAMATI NZIMA YA TIMU HIZI
• Iwe imetoka kwenye huo huo mkoa, ikimaanisha Wachezaji wote wa Timu nzima wawe wazawa wa mkoa huo, sambamba na Makocha wao.

Yaani Timu zote ziwe za wazawa wa Mikoa husika

PIA
• Kila timu iwe na Academy ndogo ya kukuza wachezaji chipkizi kabla ya kuhamishiwa Timu kubwa ya Mkoa.

Hii itasaidia kuongeza nafasi za Wachezaji wakubwa kwa wadogo watakaokuwa na ndoto za kuchezea Timu zao za Mkoa.

FAIDA YA KUFANYA HIVI
• Serikali itakuwa imesaidia kukuza Vipaji vya Wachezaji wa Nchini kwetu kana kwamba, Kama watakuwa wanacheza vizuri haswa mpira wenye hadhi ya Kimataifa basi Serikali itaweza kuanza kufaidika kwa kuanza kuuza wachezaji wake Katika timu za Club za hapa Nchini kama vile Simba, Yanga & Azam na hata nje ya Nchi kama vile Kenya, Congo, Nigeria, Misri na hata nje kabisa ya Africa..

• Kwa kuwa serikali ndiyo iliyokuwa inawalipa na kuwakuza ktk kipindi chote hicho, basi inaweza kuchukua hata zaidi ya 50% ya Pesa atakayokuwa analipwa Mchezaji huyo baada ya kuuzwa kwenye Club kubwa.

• Serikali itakuwa imeanza kukusanya pesa nyingi kutoka ktk Stadium za Timu hizo na kuongeza pato la Taifa..

• Pia serikali itakuwa na wachezaji wengi Professional wa Timu ya Taifa.

• Serikali itakuwa imesaidia kuboresha Umoja na Undugu ktk kila Mkoa hapa Nchini maana watu watazidi kupendana huku wakijikuta wakitoa support kubwa kwenye Michezo ndani ya mikoa wanayotoka.

• Kama Ligi hii ya Mikoa itaanza kufanya vizuri, basi Nchi yetu inaweza kujikuta ikipata Watazamaji na mashabiki kutoka sehemu mbali mbali za Nchi jirani na kuweza kuwa Ligi pendwa Africa nzima hapo baadae..

PESA ITAKAYOKUWA INAKUSANYWA NA (TFF) KWENYE MAUZO YOTE YA JEZI & TICKET
• Itatumika katika ujenzi wa Viwanja vya kisasa au kubust michezo mingine kwa kuanza kutengenezea Stadium zao (Mf. Viwanja vya Basketball vya kisasa & Swimming Pools za mikoa ili kutoa vijana watakaoanza kutuwakilisha kwenye maahindano ya OLYMPIC Duniani.

Yapo mengi ila tuishie hapa kwa leo.
 
Ligi ya taifa ngazi ya mkoa ilikuwepo,sema ilikuwa tofauti na mapendekezo yako hawa wachezaji wa timu za ligi kuu walikuwa wanarudi kuchezea mikoa yao wakichanganyika na wazawa wa mikoa hiyo kuunda timu ya mkoa wanaenda kupambana na mikoa mingine.
sikumbuki waliifuta mashindano hayo lini na yalijulikana kama taiga cup.
 
Back
Top Bottom