Serikali ianzishe kampeni dhidi ya korona phase two, isione aibu

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,311
7,494
Sisi wananchi tunaitaka serikali isikwepe majukumu yake ya kulinda afya za wananchi wake

Ni wajibu wa serikali kuwa wazi na kuanzisha kampeni ya kupambana na korona awamu ya pili

Tunaitaka serikali kupitia viongozi wa serikali kuu, mitaa, vyombo vya habari na viongozi wa dini kuhamasisha wananchi kuepuka misongamano mfano makanisani, misikitini, makongamano, semina, sehemu za burudani, michezo,na mikusanyiko ya kisiasa

Tunaitaka wizara ya afya iwape miongozo ya kupunguza maambukizi mashabiki wa mpira uwanjani,shuleni na vyuoni

Tunaitaka serikali kupitia wizara ya afya watoe vipeperushi na matangazo ya kutosha namna ya kijikinga na virusi vya korona

Tunaitaka serikali kupitia wizara ya afya kusisitiza uvaaji wa barakoa sehemu zenye misongamano

Wizara ya afya ifanye utafiti wa ugonjwa mpya wa korona waseme kirusi gani kwa sasa kipo nchini kwetu kama ni cha South Africa ama ni cha uingereza au ni kile cha mwanzo ili waweke mbinu na mikakati kwa wananchi ili kupambana nacho

Tunaitaka serikali kuacha mzaha mara moja kwenye afya za watu,na huku watu wanapukutika

Tuwapime watalii na wageni wanaoingia Tanzania ili kupunguza maambukizi mapya, tusipende hela kuliko afya za watu

Mnaangamiza Taifa kwa kukosa uzalendo wa kuwajali watu wengine

Uzalendo ni kuwajali wananchi wako tu,hakuna uzalendo zaidi ya huo
 
Duniani koote kuna korona isipokuwa tz tuu...alisikika mfalme juha mmoja wa jamhuri ya wadanganyika akiwahutubia wananchi wake huku akiwahimiza kutembea kifua mbele mat.koo nyuma!!!.
 
Back
Top Bottom